Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, April 12, 2016

Wafanyakazi wa NIDA waliositishiwa mkataba kulipwa fidia.soma zaid.


Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa nchini
(Nida) imesema itaanza kufanya malipo ya
madai ya wafanyakazi wake 597
waliokatishwa mkataba na mamlaka hiyo
hivi karibuni.
Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Modestus
Kipilimba, ilisema malipo hayo yataanza
kulipwa leo asubuhi kwenye ofisi za
mamlaka hiyo zilizopo katika jengo la
BMTL.
Malipo hayo yatafanywa kwa mgawanyo.
Mgawanyo wa kwanza utakuwa na kundi
la kwanza, pili na tatu, ambao watalipwa
kesho na mgawanyo wa pili, utakuwa na
kundi la nne na tano ambao watalipwa
keshokutwa.
Mgawanyo wa tatu utakuwa na kundi la
sita litakalo lipwa Alhamisi, mgawanyo wa
nne utahusisha kundi la 7 na 8
litakalolipwa Aprili 16 na kundi la tano
litajumuisha madereva na kada nyingine,
litalipwa Aprili 17.
Aidha, taarifa hiyo iliwataka wadai hao
kufika kwa wakati sambamba na kuwa na
vielelezo na nakala halisi za mikataba yao
ya kazi.
Awali, kulikuwa na malalamiko kutoka
kwa wafanyakazi hao walioandamana
baada ya tangazo la kufutwa kazi kuwa
malipo yanayotarajiwa kutolewa na Nida

0 comments :

Post a Comment

Back To Top