Kwa hili Tanzania na afrika mashariki kwa ujumla hatuna budi kumshukuru mungu.soama zaid.
Watu karibu 250,000 wametakiwa wahame
kutokana na wasiwasi wa kutokea kwa
mitetemeko zaidi ya ardhi nchini Japan, shirika
la kutoa misaa limesema.
Naoki Kokoawai, mshauri wa Shirika la Msalaba
Mwekundu la Japan, ameambia BBC kwamba
makundi zaidi ya matabibu yanatumwa maeneo
ya kusaidia waathiriwa.
Mitetemeko miwili mikubwa ilitikisa kisiwa cha
kusini magharibi cha Kyushu wiki iliyopita na
kuua watu 42.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imetahadharisha
kwamba kuna uwezekano mkubwa wa
mitetemeko zaidi huenda kutokea siku chache
zijazo.
Watu zaidi ya 1,000 walijeruhiwa na miundo
mbinu mingi kuharibiwa.
Wafanyakazi karibu 30,000 wa uokoaji
wanasaidia kutafuta manusura. Polisi wamesema
watu 11 bado hawajulikani walipo, kwa mujibu
wa shirika la utangazaji la serikali la NHK.
"Bado kuna watu ambao hawajulikani walipo.
Tunataka kufanya juhudi zaidi na kuwaokoa
watu,” Waziri Mkuu Shinzo Abe aliambia Bunge
mapema Jumatatu.
Tetemeko la pili laikumba Kumamoto, Japan
Tetemeko la ardhi latikisa Kumamoto Japan
Amesema anataka kutangaza eneo lililoathiriwa
kuwa eneo la janga.
Mwanamke wa umri wa miaka 61 alipatikana
akiwa amefariki karibu na nyumba yake
iliyoporomoka eneo la Kumamoto mnamo
Jumapili, gazeti la Japan Times liliripoti.
Tetemeko la ardhi la nguvu ya 7.3 lilitokea karibu
na jiji la Kumamoto, ambalo lilikuwa limeathiriwa
na tetemeko jingine la nguvu ya 6.4 Alhamisi
usiku.
Mitetemeko hiyo miwili ilisababisha uharibifu
mkubwa.
Jeshi la Marekani limesema liko tayari kutoa
usaidizi wa ndege kusaidia juhudi za uokoaji.
0 comments :
Post a Comment