Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, May 17, 2016

Bajeti ya zanzimbar leo itawasilishwa katika bunge la zanzibar.soma zaid.

WAZIRI wa Fedha Mipango na Uchumi, Dk Khalid
Salum Mohamed leo atawasilisha bajeti ya
Serikali kwa mwaka wa fedha 2016-2017,
iliyoweka kipaumbele katika kuimarisha sekta ya
elimu na miundombinu kwa kutumia fedha za
makusanyo ya kodi.
Akitoa muhtasari na muelekeo wa bajeti hiyo Dk
Salum alisema Serikali inakadiria kutumia Sh
bilioni 841.5 kwa kazi za kawaida na Sh bilioni
395.9 kwa shughuli za maendeleo. Aidha alisema
mkazo umewekwa katika makusanyo ya kodi
huku taasisi zenye majukumu hayo zikitarajiwa
kukusanya Sh bilioni 482.4 kutoka katika vyanzo
vya ndani.
Alisema Bodi ya Mapato ya Zanzibar itakusanya
Sh bilioni 237.4 na Mamlaka ya Mapato (TRA)
itakusanya Sh bilioni 188.8. “Bajeti ya mwaka
huu serikali haitopandisha kodi ya aina yoyote na
badala yake itajikita katika kuimarisha usimamizi
na utendaji wa ndani katika makusanyo ya kodi,”
alisema Dk Salum.
Alisema mikakati ya serikali ni kubana matumizi
na kuwa makini katika kutumia fedha za bajeti
kwa mujibu wa uwezo wa Serikali katika kufanya
makusanyo ya fedha, ambapo mkazo umewekwa
katika kulipa madeni ya walimu na viinua
mgongo.
Dk Salum alisema kwa mara ya kwanza Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, inatarajia kufaidika na
fedha za kodi ya mapato inayotokana na
watumishi wa Serikali ya Muungano waliopo
Zanzibar, inayotarajiwa kufikia Sh bilioni 21.0.chanzo habar leo

0 comments :

Post a Comment

Back To Top