Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wametakiwa kufuata sheria na kanuni wakati wa kutumbua majipu.soma zaid.
MAKAMU wa Rais, Samia Hassan Suluhu
amewataka wakuu wa mikoa na wa wilaya,
kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa
umma wanapotaka kufukuza kazi watumishi
wanaokwenda kinyume. Samia alisisitiza jana
kuwa hajawahi kupinga utumbuaji majipu kama
ambavyo alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya
habari.
Hata hivyo, aliwaambia wakuu hao wa mikoa na
wilaya kwamba mwenye mamlaka ya kutumbua
majipu ni Rais pekee, kwa kuwa anateua, anaajiri
na kufukuza. Alisema hayo juzi alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
juu ya agizo lake la kutaka mifugo iliyo ndani ya
hifadhi za Taifa (Tanapa) ihamishwe.
Alisema wakuu wa mikoa na wilaya nchini,
wanapaswa kuhakikisha wanapotaka kuwajibisha
watumishi wa umma wanafuata sheria, kanuni na
taratibu za utumishi wa umma.
“Rais pekee ndiye ana mamlaka ya kuteua,
kutengua na kuajiri; Lakini sijapinga utumbuaji wa
majipu bali nasisitiza kila RC (Mkuu wa Mkoa) na
DC (Mkuu wa Wilaya) afuate sheria kanuni na
taratibu za utumishi wa umma,” alisema.
Makamu wa Rais alisisitiza mifugo inayotoka nje
ya nchi iliyomo kwenye hifadhi za taifa,
kuhakikisha inaondolewa ifikapo Juni 30.chanzo habar leo.
0 comments :
Post a Comment