Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, May 17, 2016

Serikal imetenga Sh.bilion 39 kukomesha foleni Dar.sima zaid.


WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
imeomba kuidhinishwa Sh trilioni 4.8 kwa ajili ya
mwaka ujao wa fedha ambazo kati ya hizo, sekta
ya ujenzi imetengewa sehemu kubwa ya fedha
zitakazojenga barabara ikiwemo kuondoa
msongamano katika Jiji la Dar es Salaam.
Licha ya sekta ya ujenzi ambayo imetengewa Sh
trilioni 2.1, kwa upande wa uchukuzi, miongoni
mwa maeneo ambayo bajeti imeyapa kipaumbele,
ni pamoja na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
lililotengewa Sh bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi
wa ndege zaidi ya tatu.
Kwa upande wa reli, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa,
katika kuwasilisha Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya wizara hiyo, alisema Sh bilioni 9.5
zimetengwa kwa ajili ya usanifu wa kina na
kuanza ujenzi wa reli ya Standard Gauge.
Fedha za ndani Akiwasilisha makadirio ya
mapato na matumizi, Profesa Mbarawa alisema
sekta ya ujenzi imetengewa Sh trilioni 2.2 kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa
fedha za ndani kutoka mfuko mkuu serikalini na
mfuko wa barabara.
Alisema katika mfuko wa barabara, wanatarajia
kukusanya Sh bilioni 832.3 zitakazotumika
kufanya kazi za matengenezo ya barabara nchini.
Alisema katika ujenzi wa barabara kuu,
zimetengwa Sh bilioni 16.5 kwa kufanya
upembuzi yakinifu kwa kilometa 3,184 .
Alisema Sh 29,773,307,730 watatumia kwa ajili
ya barabara za mikoa kwa kutumia mfuko wa
barabara kwa kukarabati kilometa 584.30 kwa
kiwango cha changarawe na kilometa 36.9 kwa
kiwango cha lami. Msongamano Dar Alisema
katika kuondoa msongamano katika jiji la Dar es
Salaam, Sh bilioni 38.9 zimetengwa kwa ajili ya
kuendelea na ujenzi wa barabara za kilometa
111.85.
Alitaja barabara hizo kuwa ni mzunguko wa
Kawawa-Msimbazi- Jangwani/ Makutano ya
Twiga, Tabata Dampo-Kigogo, Kimara Kilungule-
External na Mbezi Malambamawili- Kinyerezi-
Banana. Pia alisema fedha hizo zitatengeneza
barabara ya Tegeta–Wazo Hill- Goba-Mbezi,
Goba-Mbezi Mwisho, Tangi Bovu-Goba, Kimara
Baruti- Changanyikeni na kwingineko.
Barabara nyingine Alisema katika mwaka ujao wa
fedha, Sh bilioni 30 zimetengwa kwa ajili ya
ujenzi wa barabara za mikoa na madaraja katika
mikoa yote nchini. Alisema kwa upande wa
miradi ya barabara na madaraja itakayojumuisha
ujenzi wa njia ya Express ya Dar es Salaam-
Chalinze-Morogoro yenye kilometa 200 na Dar es
Salaam -Chalinze kilometa 128, imetengewa Sh
bilioni 12.6 kwa ajili ya upembuzi yakinifu pamoja
na nyaraka za zabuni kwa ushirikiano na sekta
binafsi.
Alisema katika ujenzi wa madaraja makubwa,
katika mwaka huu wa fedha zimetengwa Sh
bilioni 47.2 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa
madaraja ya Kirumi (Mara), Sibiti (Singida) na
Sukuma (Mwanza).
Madaraja mengine na mikoa yake kwenye
mabano ni Kilombero (Morogoro), Kavuu (Katavi),
Mbutu (Tabora), Momba (Songwe/Rukwa),
Simiyu (Simiyu) Lukuledi II (Lindi) pamoja na
daraja jipya la Wami (Pwani).
Waziri Mbarawa alisema wizara yake pia
imetenga Sh bilioni 17.9 kwa ajili ya barabara ya
Kyaka-Bukene mkoani Kagera, yenye kilometa
170. Mbarawa alisema kati ya barabara na
madaraja hayo, jumla ya kilometa 712.40
zitajengwa kwa kiwango cha changarawe na
kilometa 63.8 kwa kiwango cha lami pamoja na
ujenzi wa madaraja 15. ATCL kufufuka?
Akizungumzia ununuzi wa ndege, Waziri Mbarawa
alisema fedha hizo; Sh bilioni 500 zitanunua
ndege zisizopungua tatu. Hata hivyo, alisema
idadi kamili ya ndege zitakazonunuliwa na bei ya
kila ndege itajulikana baada ya uchambuzi wa
suala hilo kukamilika. Vilevile alisema wametenga
Sh bilioni 200 kwa ajili ya utekelezaji miradi
mbalimbali katika Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege.
Reli, bandari Alisema serikali inatarajia
kuwasilisha bungeni sheria mpya ya Tazara
kuboresha utendaji wake. Vilevile alisema,
watakamilisha usanifu wa kina wa njia ya reli
kati ya Tanga-Arusha na upembuzi yakinifu wa
usanifu wa awali wa ujenzi wa reli hiyo ya
standard gage.
Alisema reli ya Arusha-Musoma pamoja matawi
yake kwenda Engaruka na Minjingu, zimetengewa
Sh bilioni 9.7. Akizungumzia ujenzi na upanuzi
wa Bandari ya Dar es Salaam, alisema
wametenga Sh bilioni 342 kuimarisha na
kuongeza kina cha gati namba 1 hadi 7, kujenga
gati jipya na kukamilisha jengo la huduma kwa
wateja.
Kuhusu Shirika la ReliTanzania (TRL), alisema
mwaka huu wa fedha wamepanga kusafirisha
tani 537,500 za mizigo na abiria 541,000 na
wakati huo huo kuendelea kukarabati mabehewa
ya abiria na mizigo.
Mawasiliano, TTCL Kwa upande wa sekta ya
mawasiliano, Waziri Mbarawa alisema Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL) inatarajia kuongeza
idadi ya wateja wa huduma mbalimbali za simu
kutoka 74,790 wa mwaka jana hadi 815,000
ifikapo mwaka 2018. Pia wanatarajia kuanzisha
na kuendesha mtandao wa kisasa wa simu za
kiganjani na kuboresha mtandao wa data na simu
za waya au mezani ili kuleta ufanisi kwa wat

0 comments :

Post a Comment

Back To Top