Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, May 14, 2016

Bomoa bomoa yaleta simanzi na vilio kwa wakazi mafisa mkoani morogoro.soma zaid.

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limelazimika
kutumia mabomu ya machozi na maji ya
kuwasha kuwatawanya wananchi waliokusanyika
na kufunga barabara ya Morogoro-Dodoma
wakipinga kubomolewa nyumba zao za kuishi
katika eneo la Mafisa.
Wananchi hao wamelazimika kufunga barabara
hiyo ya Morogoro-Dodoma baada ya kudai kupata
taarifa kuwa nyumba zao wanazoishi
zingebomolewa siku ya jumatatu ili kupisha eneo
la uwekezaji.
Jeshi la Polisi likalazimika kutumia mabomu ya
machozi na maji ya kuwasha kuwatanya
wananchi hao ambao walijaribu kukabiliana na
askari hao kwa kurusha mawe, ambayo
yaliwajeruhi watu mbalimbali akiwemo mwandishi
wa habari wa kituo cha Mlimani TV Remmy
Yasint ambapo diwani wa kata ya Mafisa Daudi
Salumu amesema taarifa zilizotolewa kwa
wananchi juu ya kubomolewa nyumba zao sio
sahihi kwani zoezi la ubomoaji limewekewa zuio
na mahakama ya ardhi huku mbunge wa jimbo la
Morogoro mjini Abdulazizi Abood akishauri
serikali kubadili matumizi ya ardhi kutoka eneo la
uwekezaji na kuwapa wananchi ambao tayari
wana hati miliki za viwanja hivyo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top