Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, May 14, 2016

Watanzania washauliwa kuzigeuza changamoto zilizopo kuwa fursa za kiuchumi.simo zaid.

Makamu wa rais Mh Samia Suluhu Hassan
amewataka watanzania kujenga utamaduni wa
kuzigeuza changamaoto zilizopo kuwa fursa za
kiuchumi kwani ni jambo linalowezekana.
Akizungumza wakati anazindua kituo cha kisasa
cha kutengeneza vipuri vya magairi yakiwemo
matairi kinachoendeshwa na kampuni ya Super
Doll katika jiji la Arusha Mh Samia amesema
kutengeneza bidhaa kulingana na mahitaji ni
ubunifu ambao uko ndani ya uwezo wa
watanzania wengi ambao ukitumika vizuri
matatizo mengi yatapata ufumbuzi.
Mkurugenzi wa kampuni ya Supper Doll Bw.Seph
Ally Seph amesema pamoja na bidhaa zao
kutengenezwa nje ya nchi zinazingatia mazingira
ya barabara za hapa nchini hasa zenye fursa za
kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo
ya utalii.
Licha ya Tanzania kuwa na magari mengi
ambayo ni moja ya nyenzo muhimu katika
kupambana na umaskini asilimia kubwa ya vipuri
yakiwemo magurudumu yanatoka nje ya nchi na
licha ya kuwepo kwa mipango mingi ya kufufua
kiwanda cha kutengeneza tairi cha General Tyre
utekelezaji wake bado ni mgumu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top