Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, May 14, 2016

Vigogo wa sukari wampigia magoti mkuu wa wilaya wa kinondoni.soma zaid.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi
amefichua kuwa amekuwa akipigiwa simu na
baadhi ya wafanyabiashara vigogo wenye nia ya
kutaka kupunguza makali ya operesheni
inayofanywa na wilaya yake dhidi ya waficha
sukari.
Kwamba simu hizo amekuwa akipigiwa hadi usiku
wa manane na huku wengine wakimtumia ujumbe
mfupi wa simu wa maandishi (SMS). Amekemea
wafanyabiashara hao na kutaka waache mara
moja mchezo huo, kwani vyombo vya dola
vinaendelea kuwafuatilia.
Hapi alisema hayo jana wakati akizungumzia
suala la Uadilifu kwenye Mkutano wa Shirikisho la
Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini na
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
CCM wanaotokana na shirikisho hilo.
Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya alibainisha
kwamba amekuwa hapokei simu hizo na SMS
hizo za wafanyabiashara wakubwa kutokana na
sababu mbalimbali. “Sababu ya kwanza sina
sababu ya kuzipokea, lakini pili nahofia
nikizipokea nitarekodiwa na wafanyabiashara hao
na sauti yangu itasambazwa kwenye mitandao,
kuonesha nipo pamoja nao.
“Wakati mwingine mpaka usiku wa manane
wanapiga simu na kutuma meseji na wengine
wanajitambulisha. Lakini huwa namuonyesha
mke wangu na kumwambia sina sababu ya
kuzipokea, kwani naweza nikapokea lakini katika
mazungumzo yetu nikasema neno ‘sawa’, kisha
neno hilo linaweza kusambazwa katika mitandao
kuonyesha kwamba nia yetu ni moja ya kuficha
sukari”, alisema Hapi.
Alisema hao wafanyabiashara wanaoficha sukari,
wanaleta madhara makubwa kwa jamii na
uchumi wa nchi, kama vile kuua viwanda vya
sukari nchini. Alisema wafanyabiashara hao
wamekuwa wakiweka ‘oda’ katika viwanda vya
sukari kuchukua bidhaa hiyo, lakini hawaendi
kuichukua kwa madai ya kwenda kuichukua siku
za baadaye, lengo likiwa kuificha. Hapi
aliwaomba wakazi wa wilaya ya Kinondoni,
kuendelea kuisaidia serikali kufichua watu wote
walioficha sukari.chanzo habar leo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top