Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, May 14, 2016

Kukomesha rushwa kunahitaji ushirikiano kutoka kwa wadau wote wapinga rushwa.soma zaid.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amesema mkutano wa kimataifa uliojadili jinsi ya
kupambana na rushwa duniani ni kiashiria
kwamba tatizo la rushwa ni kubwa sana na
linataka juhudi za pamoja kukabiliana nalo.
Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati
akizungumza na Waziri wa Nchi wa Uingereza
anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa,
Justine Greening walipokutana kwenye mkutano
huo uliofanyika Lancaster House, jijini London,
Uingereza.
Waziri Mkuu ambaye alihudhuria mkutano huo
kwa niaba ya Rais John Magufuli, alimweleza
Greening kwamba viongozi wa Serikali wa
Awamu ya Tano wameamua kupambana na kila
ovu linalotokana na janga la rushwa na pia
wameamua kuwajibika na kuachana na tabia ya
kufanya kazi kwa mazoea.
“Sasa hivi nchi yetu ina utamaduni mpya wa
kufanya kazi na tumeamua kufanya kazi na siyo
tena kwa mazoea, tumeamua kuweka utamaduni
mpya wa kupiga vita rushwa ili kuleta uwajibikaji
na uwazi miongozi mwa watu wetu,” alisema.
Alipoulizwa ni kitu kimechangia kufanya Tanzania
ing’are kimataifa katika vita hii, Waziri Mkuu
alijibu kwamba Tanzania imetumia mambo
manne ambayo ni kuzuia rushwa isitolewe au
kupokewa, kampeni za kuelimisha jamii, kufanya
mapitio ya sheria na kuwepo kwa utashi wa
kisiasa.
“Serikali inachukua hatua za kuanzisha
mahakama maalumu ya mafisadi ambayo
inatarajiwa kuanza kazi mwezi Julai mwaka huu,”
alisema Waziri Mkuu.
Greening alipongeza hatua zinazochukuliwa na
Serikali katika kupambana na rushwa na kwamba
ndiyo maana Tanzania ilipewa mwaliko maalumu
wa kushiriki mkutano huo kwa vile baadhi ya
mataifa yanaziona juhudi zinazofanywa na
Serikali.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top