Hiki ndio kilichosemwa na mashirika16 ya kutete makundi ya watu yenye uhitaji maalumu.soma zaid.
Zaidi ya mashirika 16 ya kutetea makundi yenye
uhitaji maalumu yakiwemo ya watoto na
wanawake yametoa tamko la kupinga vitendo vya
ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kutumia
mitandao ya kijamii na simu za mkononi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewajijini Dar es
Salaam imesema kumekuwa na ongezeko kubwa
la vitendo vya ukatili vinavyohusisha watoto na
wanawake katika mitandao ya kijamii na simu za
mkononi huku sheria ya makosa ya mtandao
ikionekana kutokuwa na nguvu.
Taarifa hiyo pia imeitaka jamii kuacha tabia ya
kuvunja haki ya makundi hayo pale ambapo haki
zao zimekwishakuvunja, huku wakiitaka serikali
kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote
anayetumia mitandao ya kijamii na simu za
mikononi vibaya .
0 comments :
Post a Comment