Breaking News
Loading...

Advert

Friday, May 13, 2016

Rais maguful amefanya ziara ya kusitukiza uwanja wa ndege mwl.nyerere na kubaini dosari kadhaa.soma zaid.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya
Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana
na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja
dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo
cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere (Terminal One) Jijini Dar es salaam.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13
Mei,2016 alipofanya ziara ya kushtukiza katika
uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi
za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi
kazi kwa muda mrefu.
Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa wakitoa
maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa
mizigo na abiria katika uwanja huo,walikuwa
wakitoa taarifa zinazotofautiana kuhusu utendaji
kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha
Dkt. Magufuli aamue kuiagiza wizara husika kwa
kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua
mara moja.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara
hii ya kushtukiza mara baada ya kuwasili katika
uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere
akitokea Jijini Kampala nchini Uganda ambako
jana alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais
wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta
Museveni.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top