Breaking News
Loading...

Advert

Monday, May 9, 2016

Katibu wa utumishi na Nidhani ya walimu( TSD)wilaya ya muleba ajinyonga.soma zaid.

Katibu wa Tume ya Utumishi na
Nidhamu ya Walimu (TSD ) Wilaya ya Muleba,
Manase Mkumbo amekutwa amefariki dunia kwa
kujinyonga shambani mwake katika Kijiji cha
Kyamyorwa wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Francis Isack
amesema Mkumbo alijinyonga usiku kuamkia leo.
Amesema kabla ya tukio hilo alituma ujumbe wa
maandishi kwa simu akimjulisha mwanae aliye
masomoni kuwa amekata tamaa na maisha.
Isack amesema Mkumbo aliondoka Muleba
kwenda kukagua mashamba yake kijijini ambako
aliandika ujumbe huo na kununua kamba ya
katani na kujinyonga.
Ujumbe huo ulipomfikia mtoto wake aliutuma
tena nyumbani katika Kitongoji cha Bugombe
wilayani Muleba ndipo wakaanza kufuatilia kwa
kuwa alikuwa amewaaga kuwa anaelekea
shambani ambako walikuta mwili wake
umetundikwa.
“Inasikitisha mtu alibakiza mwaka mmoja astaafu
na kupata mafao yake lakini anaamua kujiondoa
na kuacha hasara na simanzi kwa familia,”
amesema Isack.
Amesema taratibu za kusafirisha mwili wa
marehemu kwenda kwao mkoani Singida
zinaendelea.chanzo mwananch.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top