Mabasi yaendayo kasi sasa yatatoa huduma ya usafiri bure wiki nzima.soma zaid.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
ametembelea kituo cha Mabasi yaendayo haraka
cha Kamata Kariakoo leo Mei 11 na kueleza
kuwa, kuanzia jumatatu Mei 16, 2016, Mabasi
hayo yataanza kutoza nauli ‘kuchaji’ ambazo
zilitangazwa na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi
Kavu na Majini (SUMATRA).
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi hasa
wale wanaotumia barabara maalum ya mabasi
hayo yaendayo kasi kuacha mara moja kufanya
hivyo kwani ni kinyume na sharia ikiwemo
watembea kwa miguu, baiskeli, na zile za miguu
mitatu (Maguta), Waendesha bodaboda na
magari mengine wasitumie barabara hizo ili
kuepusha usumbufu kwa madereva wa mabasi ya
mwendo wa haraka.chanzo clouds radio.
0 comments :
Post a Comment