Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, May 14, 2016

RC simiyu atoa siku tano kuchunguzwa kwa watumishi sita wa halmashauli y Bariadi.soma zaid.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka
amemwagiza Kamanda wa Takukuru Mkoa wa
Simiyu kuwaongeza katika kesi ya watumishi sita
wa Halmashauri ya Bariadi kwa matumizi mabaya
ya madaraka baada ya tuhuma za ujenzi wa banio
la umwagiliaji wa Kijiji cha Kungulyambeshi na
kusababishia serikali hasara ya shilingi milioni
600 ambapo kukamilika kwa mradi huo ni bilioni
1.4 .
Kufuatia agizo la siku tano la Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Antony Mtaka kwa Mkurugenzi Mtendaji
na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Ponsiano Nyami
la kuwapatia taaarifa za miradi yote ya maji
iliyojengwa chini ya kiwango na hivyo kufanya
ziara ili kujiridhisha katika ujenzi wa Bwawa la
umwagiliaji Kasoli , mradi wa banio la maji na
mradi wa maji Zanzui ambao ulikuwa
ukilalamikiwa kutotoa maji na wananchi.
Mkuu huyo ameonekana kukasirishwa na mradi
huo ambao kukamilika kwake utatumia shilingi
bilioni 1.4 ambapo hadi sasa umetumia milioni
587 huku akishangazwa na ujenzi wa mfereji wa
mita 500 kwa shilingi milioni 70 na hivyo kutoa
maagizo kwa Kamanda wa Takukuru.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top