Breaking News
Loading...

Advert

Monday, May 9, 2016

Serikal ya ugiriki yapania kubana matumizi kama Tanzania inavyofanya sasa.soma zaod.

Wabunge nchini Ugiriki wamepitisha mpango tata
wa kupunguza malipo ya uzeeni na kupandisha
kodi licha ya upinzani mkali kutoka kwa umma.
Maelfu ya Wagiriki waliandamana kupinga hatua
hizo
Hatua hiyo ni ya kutimiza masharti ya
wakopeshaji wa kimataifa katika jitihada za
kupewa fungu jingine la fedha za mkopo
zinazohitajika kuuokoa uchumi wake.
Mageuzi hayo ambayo yalipingwa na wengi, na
kusababisha maandamano yaliyowahusisha
maelfu ya watu jana jioni, yalipitishwa na
wabunge wa chama cha serikali cha siasa za
mrengo wa kushoto cha Syriza katika bunge
lenye viti 300. Wabunge 153 wa Syriza na wa
muungano wa Independent Greeks walipiga kura
kuunga mkono mswada huo wa hatua za kubana
matumizi.
Kama ilivyotarajiwa vyama vyote vya upinzani
viliupinga mswada huo, ambao utapunguza
malipo ya juu kabisa ya pensheni nchini Ugiriki,
kuunganisha fedha za pensheni, kuongeza
michango na kupandisha kodi kwa wale wenye
mapato ya wastani na ya juu. Grigoris Kalomiris
ni mwanachama wa bodi ya chama cha
wafanyakazi wa umma.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top