Watumishi hewa 11 wasababisha afisa utumishi ilala kusimamishwa kazi.soma zaid.
Mei 2 2016 Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul
Makonda aliwaapisha wakuu wa idara na maofisa
utumishi wote lengo likiwa ni kuwataka kila
mtumishi kuwabainisha watumishi wao hewa
katika idara zao na atakayebainika kutoa taarifa
zisizo sahihi mkataba umfunge mwenyewe.
Leo May 09 2016 katika uchunguzi wa awamu ya
tatu wamekuja na ripoti ya watumishi hewa 39
walioisababishia Serikali hasara ya BILIONI 3.6.
Paul Makonda amemsimamisha kazi afisa
utumishi wa Manispaa ya Ilala, Gerac Phus kwa
kutowagundua watumishi hewa 11 ambao
walikuwa hawajulikani wapo idara gani.
0 comments :
Post a Comment