Donard Trump ashikilia msimamo wake.soma zaid.
Mgombea wa kiti cha urais wa chama cha
Republican nchini Marekani Donald Trump,
amesema mauaji ya watu 50 katika baa moja ya
wapenzi wa jinsia moja huko Orlando
inathibitisha msimamo wake kwamba waislamu
wapigwe marufuku kukanyaga ardhi ya
Marekani.
Trump amemkashifu mpinzani wake wa chama
cha republican Bi Hillary Clinton, kwa kutodadisi
sababu za mtu huyo kutenda mauaji hayo.
Upande wa Bi Clinton wakitoa risala za pole kwa
waathiriwa wa mkasa huo papo hapo wamemtaja
Trump kama mtoto anaejitweza ovyo kwa jinsi
anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza
binafsi.
Wakati huo huo Shirika la kijasusi la FBI
limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa
kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi
ya jinsia alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la
IS.
Fbi wameongeza kusema kuwa wamekuwa
wakimfanyia uchunguzi mtu huyo Omar Mateen
tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki
akiwa kazini .
Babake Mateen amesema anaamini kitendo
alichokifanya wanawe kilitokana na msukumo wa
hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya
jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.
Naye mkewe wa zamani Sitora Yusufiy,
amemwelezea Mateen kama mtu wa aliyekuwa
tabia za kigomvi na kutaka kupiga watu lakini
hakuwa na itikadi kali za kidini.
0 comments :
Post a Comment