Hekta 5000 za mashamba ya mkonge tanga zimefutwa hati zake.soma zaid.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa John Pombe Magufuli amefuta hati
ya mashamba ya Mkonge, yenye hekta zaidi ya
5000 yaliyokuwa yametelekezwa na kuwa mapori
ambayo hayaendelezwi kufuatia malalamiko ya
wakazi wa zaidi ya 2000 wa kijiji cha Kibaranga
kuhangaikia maeneo ya kilimo na kusababisha
migogoro ya mara kwa mara baina yao.
Akizunguza na wananchi wa kijiji cha Kibaranga
katika mkutano wa hadhara,waziri wa
ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi
Mheshimiwa William Lukuvi amesema hili ni
shamba la tano kufuntwa na Mheshimiwa rais
katika mkoa wa Tanga kufuatia wawekezaji
waliopewa hati ya kuyaendeleza kushindwa
kutekeleza makubalino.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga
Martin Shigella amesema serikali mkoa wa Tanga
imepewa jukumu la kugawa ardhi hiyo
watahakikisha kuwa wanaweka utaratibu
utakaowezesha kuwa kila mwananchi apate
shamba na hati ili yaweze kuwaendeleza
wananchi.
Kufuatia hatua hiyo mwenyekiti wa kamati ya
bunge inayoshughulikia ulinzi na usalama
Mheshimiwa Adad Raja amesema watahakikisha
wawekezaji matapeli hawaruhusiwi kujimegea
ardhi kwa manufaa yao na badala yake
mashamba hayo yaendelezwe na wananchi
waliokabidhiwa ili yaweze kuwapa manufaa.chanzo ITV.
0 comments :
Post a Comment