Breaking News
Loading...

Advert

Monday, June 6, 2016

Kasi ya Rais maguful imeivutia marekani sasa kutoa msaada wa dola 800m.soma zaid.

Uhusiano kati ya Marekani na Tanzania
unaonesha dalili za kuimarika licha ya nchi hiyo
kukatiza msaada wa awamu ya pili ya mradi wa
changamoto za milenia (MCC-2) kwa Tanzania.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mheshimiwa
Mark Childress amesema hayo baada ya
kukutana na kufanya mazungumzo na rais wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Bwana Childress alisema kuwa hivi karibuni
''kupitia shirika la misaada la Marekani, USAID
tunatarajia kutia saini mkataba wa zaidi ya dola
milioni 400 kwa ajili ya mwaka ujao.
''Aidha tumezungumza kuwa kutakuwa na dola
milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili
ya miradi mbalimbali na hii haihusiani na MCC.''
Alisema balozi Childress
"Ukweli ni kwamba tunayo mengi ya kufanya
pamoja katika sekta mbalimbali zikiwemo afya,
elimu na kilimo na tutafanya kila juhudi
kuhakikisha yanafanikiwa"
Rais Magufuli kwa upande wake alisema kuwa
serikali yake itaendeleza kuimarisha zaidi
uhusiano na ushirikiano na Marekani.
Aidha rais huyo alisema kwamba fedha za
msaada kutoka Marekani ni muhimu kwa
maendeleo ya Tanzania.
"Amekuja kutuhakikishia kwamba watatoa hela
kwa ajili ya Tanzania na anasema sasa hivi
watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba
mwingine tunaweza tukasaini hata kesho wa dola
milioni 410.
Rais Magufuli alisema ''Balozi anasema kutotoa
hela za MCC hakuna maana kupotea kwa urafiki
wa Tanzania na Marekani, urafiki wa Tanzania na
Marekani upo pale pale na sasa wanaongeza hela
nyingi zaidi katika kuonesha kwamba juhudi za
''Hapa kazi tu'' zinaendelea" Taarifa hiyo ya ikulu
ilielezea.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top