Hizi ndizo sababu 10 ziliozo fanya wema sepetu akutwe na haya.soma zaid.
Imevuja! Kuyeyuka au kuharibika kwa ule ujauzit
wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ‘Madam’
hivi karibuni kumetajwa na daktari kuwa ni
matokeo ya tabia yake ya kukaidi ushauri wa
kitaalam, Amani lina cha kuwapa wasomaji wak
Hayo yalisemwa na mtu wa karibu we Wema
(jina lipo) akizungumzia masharti ambayo dakta
aliyepata kumtibu mrembo huyo aliyasema.
Lakini pia, daktari mwingine wa jijini Dar, Dk.
Fadhili Emily naye ameibuka na kuliambia Amani
kuwa, Wema ana sababu 8 za mimba zake
kuyeyuka akiwa anajua au hajui.
DAKTARI WA KWANZA
Mtu huyo wa karibu na Wema alisema mimba
ambayo staa huyo aliifanyia shoo kwenye
mitandao mbalimbali ya kijamii na kuyeyuka
Februari, mwaka huu, ilitokana na sababu ya
kugoma kutii masharti ya kitabibu.
SABABU YA KWANZA
“Vipimo vya kitabibu vilisema kuwa Wema
alitakiwa kupumzika kwa muda mrefu ili kuilinda
mimba hiyo kwani ilikuwa katika hatihati ya
kutoka kama mhusika atakuwa ni mzururaji. Sas
Wema akiwa mjamzito alikuwa hakosi viwanja.”
USHAHIDI
Februari, mwaka huu, akiwa mjamzito, Wema
alihudhuria tukio la uzinduzi wa Video ya Lupela
iliyozinduliwa na Alikiba Salehe kwenye Hoteli y
Slipway, Oysterbay jijini Dar.
SABABU YA PILI
“Ilifika wakati, Wema alitakiwa kupewa bed rest
(mapumziko ya kitandani) ili kulinda mimba yak
Hilo nalo likawa gumu kwake kukubaliana nalo.
Ndiyo ikawa sababu ya mimba kutoka.”
SABABU YA TATU
“Sababu ya tatu, aliambiwa na daktari wake
asifanye kazi ngumu, jambo ambalo lilikuwa
likimshinda. Yeye si mtu wa kukubali kukaa tu
muda wote. Hilo nalo lilichangia.”
Wema SepetuWema akiwa na mama yake mzazi
SABABU NYINGINE 5
Naye Dk. Fadhili, akizungumza na gazeti hili
Jumatatu iliyopita, alisema sababu tatu ambazo
zinadaiwa zilichangia mimba ya Wema kuyeyuka
ni za kweli, lakini akasema Wema bila kujijua au
akijua, mimba zake kadhaa zimeshatoka kwa vil
wanawake wengi wenye matatizo ya kutoshika
mimba, hushika na kutoka bila wenyewe kujijua
na pia akaanika sababu za hali hiyo kumtokea
mwanamke.
Lakini akasisitiza kuwa kuharibika kwa mimba ni
tatizo ambalo linaweza kumkumba mwanamke
yeyote, si Wema tu.
SABABU ZA KIMAUMBILE
“Sababu za mimba kutoka zenyewe zinatajwa
kwamba ni tabia ya kurithi, yaani vinasaba
ambavyo si vya kawaida. Kwa hiyo, kiumbe
kinakuwa katika hali ambayo kwa asili mimba
haiwezi kukua. Kama mtoto akizaliwa basi
atakuwa na matatizo ya kimaumbile na kiakili.”
SABABU YA MUUNGANO
“Sababu nyingine ni kukosekana kwa yai
lililorutubishwa. Katika kuumba, yai la
mwanamke hukutana na mbegu ya mwanaume
na zoezi la kiumbe kukua huanzia hapo kwa yai
kujitenga mara mbili. Upande mmoja
hutengeneza kondo la nyuma na kifuko cha
kutunza maji na sehemu ya pili hutengeneza
kiumbe au mtoto.
“Huwa inatokea sehemu ya kondo la nyuma
inaendelea kukua wakati sehemu ya mtoto
haikui. Katika hali kama hii, kama mama
hajafanya vipimo kujua maendeleo ya mtoto,
uwezekano wa mimba kutoka kabla ya kufikisha
wiki 24 ni mkubwa.
“Lakini hili la muunganiko nasema pia kwamba,
kwa mwanamke ambaye mimba yake inahofiwa
kutoka, ni hatari kuendelea kukutana kimwili na
mwanaume wake kwani uwezekano wa kutoka n
mkubwa.”
KUHUSU IDRIS
Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba
walikuwa wakiendelea ‘kukutana’, lakini kipindi
cha ujauzito wake, Wema na Mbig Brother, Idris
Sultan uhusiano wao ulikuwa umekolea.
SABABU YA POMBE
“Sababu nyingine inayochangia kuharibika kwa
mimba ni unywaji wa pombe kupita kiasi kwa
mama mjamzito au kuvuta sana sigara,” alisema
dokta huyo.
SABABU YA MAGONJWA
Sababu nyingine alizitaja kuwa ni magonjwa
yanayoshambulia mwili wa mama na kiumbe
wake tumboni kama vile malaria na kaswende.
SABABU YA KUTOA MIMBA
Daktari huyo alisema kuwa, mwanamke kutoa
mimba mara kwa mara kunachangia kuharibika
au kushindwa kunasa mimba baadaye.
“Lakini si lazima awe anatoa mimba mara kwa
mara, mwanamke anaweza kutoa mimba mara
moja tu ikiwa katika mazingira ya ukuaji salama.
Hilo linaweza kuwa tatizo kubwa la mimba
kutoka siku za usoni,” alisema.
USHAHIDI
Katika mahojiano na gazeti damu moja na hili,
Risasi Jumatano mwaka jana, Wema alikiri
kuwahi kutoa mimba moja tu ya aliyekuwa staa
wa filamu za Bongo, marehemu Steven
Kanumba.
WEMA ASAKWA
Mpaka juzi Jumanne, gazeti hili lilikuwa
limetimiza siku saba za kumsaka Wema kwa ajili
ya kupata vielelezo vyake kufuatia madai au
maelekezo hayo ya daktari lakini bila mafanikio
kwani hapokei simu na hata alipotumiwa ujumbe
mfupi, nao hakuujibu
Chanzo:Swahili five.
0 comments :
Post a Comment