Zanzibar# waziri atoa siku 14 kwa halioharibu shamba lake.soma zaid.
Waziri asiye na Wizara Maalum wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar,Mhe. Said Soud,amewapa
siku kumi na nne walioharibu shamba lake
kujitokeza.
Waziri huyo amesema kuwa watu hao
wasipojitokeza atakusanya waganga wote nchini
ili kuwasomea albadir. Akaongeza kuwa yeyote
atakayejitokeza hatampeleka polisi.
Siku chache zilizopita,watu wasiojulikana
wamevamia na kuharibu shamba la Waziri huyo.
Katika hujuma hizo zilizotokea katika shamba
lililoko Mgelema Jimbo la Chonga Wilaya ya
Chake Chake , jumla ya mikarafuu 29 , minazi
16 pamoja na mashina 250 ya muhogo
yamengo’lewa na baadhi ya mengine kufyekwa
na kitu chenye ncha kali .
Katika tukio hilo mikarafuu michanga 15
imeng’olewa na kutupwa ndani ya shamba , na
mengine 14 iliyokuwa tayari kuzaa imekatwa na
kuachwa ndani ya shamba .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi , Said
Soud Said alivitaka vyombo vya ulinzi na
usalama kuhakikisha vinafanya uchunguzi wa
kina ili kuwabaini waliohusika na vitendo hivyo
vya kuhujumu mazao makuuya uchumi wa nchi .
Aidha alieleza kwamba , baadhi ya wananchi
wanalichukulia suala la siasa kama ni chuki au
fitina , na kuwashangaa wanaoendesha humuma
hizo kwani haziwezi kusaidia kutatua
changamoto za kisiasa .
0 comments :
Post a Comment