Kesi ya tuhuma za wabunge watatu kupokea rushwa kusikilizwa julai 4 .soma zaid.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru), imekamilisha
upelelezi wa kesi ya rushwa inayowakabili
wabunge watatu katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu.
Wabunge hao wa CCM ambao ni wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC), ni Ahmed Saddiq
(Mvomero), Kangi Lugola (Mwibara) na
Victor Mwambalaswa (Lupa).
Mwendesha Mashtaka wa Takukuru,
Godliver Kiriani aliiambia mahakama ya
Hakimu Mkazi, Thomas Simba kwamba
upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na
aliomba ipangwe tarehe kwa ajili ya
kuanza kuwasomea washtakiwa maelezo
ya kesi inayowakabili.
Hakimu Simba alipanga kesi hiyo ianze
kusikilizwa Julai 4 baada ya washtakiwa
kusomewa maelezo ya awali.
Washtakiwa hao ambao hadi jana
hawakuwa na mawakili, wako nje kwa
dhamana baada ya kutimiza sharti la kila
mmoja kuwa na mdhamini mmoja
aliyesaini bondi ya Sh5 milioni.
Wabunge hao walipandishwa kizimbani na
Takukuru kwa mara ya kwanza Machi 31,
2016 na kusomewa mashtaka na wakili
wa Takukuru, Maghela Ndimbo.
Washtakiwa hao wanadaiwa kwa nafasi
zao za ujumbe wa LAAC, waliomba
rushwa ya Sh30 milioni kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro,
Mbwana Magote ili waweze kutoa
mapendekezo mazuri ya Taarifa ya
Hesabu za halmashauri hiyo za mwaka
2015/2016.
Wanadaiwa kutenda kosa hilo, Machi 15,
2016, kinyume cha kifungu cha 15 (2)
cha Sheria ya Takukuru, wakiwa katika
Hotel ya Golden Tulip, iliyoko eneo la
Masaki, wilayani Kinondoni, jijini Dar es
Salaam.chanzo jamii forums.
0 comments :
Post a Comment