Sakata la Naibu Spika kuendelea leo bungeni.soma zaid.
KATIBU wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah leo
ataeleza kinachoendelea kuhusu kusudio la
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutaka
kumwondoa madarakani Naibu Spika, Dk Tulia
Ackson (pichani).
Kambi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Taifa, Freeman Mbowe katika
migomo yake dhidi ya vikao vinavyoongozwa na
Dk Ackson, iliwasilisha kusudio hilo kwa Ofisi ya
Spika wa Bunge wiki iliyopita kwa maelezo kuwa
haina imani naye.
Kwa mujibu wa Dk Kashillilah, ataeleza
kinachoendelea leo baada ya kumaliza kupitia
taratibu zote na kujiridhisha kuhusu kila hatua
inayopaswa kufuatwa kuhusu suala la aina hiyo.
“Nitaeleza kinachoendelea kesho (leo) baada ya
kujiridhisha kuhusu taratibu zinazopaswa
kufuatwa kuhusu suala hilo,” alisema.
Katika kusudio hilo lililowasilishwa na Mbunge wa
Simanjiro, James ole Millya, Kambi hiyo ya
Upinzani ilieleza mambo sita yaliyoisukuma
kuona kuwa Dk Tulia hafai kuendelea kushika kiti
cha Naibu Spika.
Mambo hayo ni upendeleo kwa wabunge wa
CCM, kusimamia maslahi ya Serikali badala ya
umma, kutokuwa mwanasiasa, jambo
linalomfanya akose uzoefu wa kuendesha vikao
vya Bunge, ubabe, unyanyasaji kwa wabunge wa
upinzani na kusimamia fedha za Mfuko wa Bunge
zirudishwe kwa Rais.
Millya alisema walipeleka kusudio hilo kwa Ofisi
ya Spika kwa kuzingatia ibara ya 85(4) ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inayozungumzia hatua za kuchukua ili
kumwondoa madarakani Naibu Spika.
Ibara hiyo inasema, “Naibu Spika atakoma kuwa
Naibu Spika na ataacha kiti cha Naibu Spika
ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka
ya Naibu Spika kwa azimio la Bunge.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa ili hoja hiyo ijadiliwe
bungeni italazimika kujadiliwa na Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka
ya Bunge ambayo nayo inahitaji theluthi moja ya
saini za wabunge wote.chanzo habar Leo.
0 comments :
Post a Comment