Anna makinda amewatumbua wakurugenzi 9 wa mfuko wa NHIF.soma zaid.
Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya ambayo Spika wa Bunge la 10,
Anne Makinda ni Mwenyekiti wake,
imewatumbua wakurugenzi 9 wa mfuko huo
kutokana na ufujaji wa mabilioni ya fedha za
umma uliobainika.
Uamuzi huo umeripotiwa kuwa umetokana na
usimamizi wao mbovu uliopelekea Mfuko kupata
hasara ya shilingi bilioni 3.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na gazeti
moja la kila siku, baadhi ya waliosimamishwa
kazi na Bodi ya NHIF na idara walizokuwa
wanazimamia kwenye mabado ni Grace Lekule
(Utawala), Raphael Mwamwoto (Uendeshaji),
Frank Lekela (Udhibiti Ubora wa Huduma) na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Michael Mhando.
Panga hilo pia limewapitia Yujin Mikongoti
(Mifuko ya Afya ya Jamii), Ally Othman
(Tehama), Rehani Athuman (Tafiti na Masoko),
Makala (Sheria) na Jackson Burula (Manunuzi).
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema kuwa
anafahamu kuwepo kwa mtikisiko huo na
kwamba majukumu yote alimwachia Mwenyekiti
wa Bodi, Anne Makinda.
“Nipo Muleba, ila majukumu yote tayari
niliyaacha kwa Bodi ya Mama Makinda. Yeye
atakuwa anajua kila kitu,” Waziri Mwalimu
ananukuliwa.
Taarifa hii imekuja ikiwa ni miezi michache
imepita tangu Mhasibu wa NHIF mkoa wa Mara,
Francis Mchati kusimamishwa kazi akihusishwa
na upotevu wa shilingi bilioni 3.
Mtuhumiwa alikabidhiwa kwa Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa ambayo inaendelea
na uchunguzi kwa hatua nyingine za kisheria.chanzo mpekuzi blog.
0 comments :
Post a Comment