Naibu waziri Dr.Hamis Kigwangara ametoa msaada wa ukarabati wa sule jimboni kwake.soma zaid.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla
amepokea ombi la kusaidia ukarabati wa jengo
la shule ya Msingi Iyombo Itima iliyopo Kata ya
Budushi ambayo iliezuliwa na upepo mkali
katika kipindi cha mvua za masika hali
iliyopelekea wanafunzi kusomea nje.
Dk. Kigwangalla ambaye yupo ziarani katika
jimbo lake hilo kwa ajili ya kuwashukuru
wananchi kwa kuweza kumchagua ili
awawakilishe Bungeni, ambapo katika ziara yake
hiyo ya kushukuru katika Kata hiyo, Diwani
Omary Maganga alimuomba Dk. Kigwangalla
kuweza kusaidia ukarabati wa jengo hilo ili
kuwaondolea adha ya wanafunzi kusomea juani.
Hata hivyo, Dk. Kigwangalla alipokea ombi hilo
na kuahidi kutoa kiasi cha Sh. Milioni tatu kwa
ajili ukarabati huo ambao utaenda sambamba na
ukarabati wa sakafu katika moja ya madarasa
ya shule hiyo baada ya kushuhudia hali hiyo
baada ya kutembelea.
Dk. Kigwangalla yupo jimboni kwa ziara hiyo ya
kuwashukuru wananchi ambapo anatembelea
Kata mbalimbali za Jimbo na kutoa shukrani
hizo ikiwemo kutoa misaada na michango
aliyowaahidi.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akielekea
katika jengo lililoezuliwa na upepo la shule ya
Iyombo Itima iliyo Kata ya Budushi, Jimbo hilo la
Nzega Vijijini.
Jengo hilo linavyookena baada ya kuezuliwa na
upepo
0 comments :
Post a Comment