Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, July 17, 2016

NEPAD yahimiza viwanda barani Afrika.soma zaid.

Kikao cha NEPAD kikiendelea
Dkt. Ibrahim Mayaki, Mkurugenzi Mtendaji
wa Mpango wa Maendeleo Afrika
KIGALI, Rwanda: Afrika inahitaji juhudi
za pamoja ili kukuza sekta ya viwanda
ambayo itasaidia kwa kiasi kubwa
kunyanyua uchumi wa bara la Afrika na
hatimaye kupunguza umaskini na kuleta
maisha bora.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa
NEPAD, chombo cha utendaji cha Umoja
wa Afrika, Dkt. Ibrahim Mayaki wakati wa
Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali
wa Nchi za Umoja wa Afrika zilizopo
kwenye mpango huo wa maendeleo barani
Afrika.
Kwenye upande wa ajira na viwanda kwa
mfano, Dkt. Miyaki alisema kuwa bara la
Afrika kwa sasa ndilo lenye vijana wengi
kuzidi mabara mengine duniani hivyo
kuna nguvu kazi kubwa ambayo
isipotafutiwa mpango mahsusi wa ajira
kutazidisha umasikini barani humo.
Viwanda vya Afrika vikiongezeka, ajira
kwa vijana zitapatikana, uzalishaji
utaongezeka na biashara ndani ya Afrika
itashamiri.
“Changamoto kubwa barani Afrika ni
biashara, ambapo nchi haziuziani bidhaa
zake, miundombinu hafifu na umasikini
uliokihiri” alisema na kuongeza kuwa
wakati muafaka umefika kwa Afrika
kuweka mikakati endelevu ya pamoja
baina ya nchi za Kiafrika ili kuhakikisha
changamoto hizi zinatafutiwa ufumbuzi.
Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa
Mpango wa Maendeleo Afrika (NEPAD)
uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa
Umoja wa Afrika Jijini Kigali Rwanda,
wajumbe walielezwa kuwa biashara ina
nafasi kubwa ya kuchochea ukuaji wa
uchumi wa viwanda barani Afrika iwapo
misingi imara ya kuendeleza biashara na
viwanda itazingatiwa.
Akizungumzia hali halisi nchini Tanzania,
Mhe. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
ambaye alimwakilisha Mhe. Rais Magufuli
kwenye mkutano huo, alisema “NEPAD pia
wametambua kwamba biashara ya ndani
barani Afrika inaendelea kuwa na jukumu
kubwa katika ukuaji wa uchumi na
viwanda vya nchi zetu za Kiafrika”.
Hivi karibuni Waziri Mahia alitangaza
Bungeni kuwa Wizara yake sasa inaweka
mikakati madhubuti kwa ajili ya
utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje
yenye muelekeo wa uchumi wa viwanda
(Economic Diplomacy of Industrialization)
ambao utazingatia dhamira ya Serikali ya
Tanzania kunyanyua sekta ya viwanda.
“Nimewaelekeza wasaidizi wangu
wamualike maalamu wa Kamisheni ya
Uchumi ya Umoja wa Mataifa ili aje
kutuelezea umuhimu wa agenda hii ya
biashara na uchumi wa viwanda nchini
kwetu” alisema Waziri Mahiga.
Alimalizia kuwa “ili utekelezaji wa
mkakati wa Diplomasia ya Uchumi wa
Viwanda ufanikiwe, ni muhimu Serikali
nzima na nchi kwa ujumla kuwa thabiti
kwenye kutekeleza sera za viwanda na za
uchumi na kuzingatia misingi ya kufanya
biashara iliyoelezwa hapa na wataalamu”.
Akielezea umuhimu wa Afrika kukuza
viwanda kwa ajili ya kujikwamua
kiuchumi, Katibu Mtendaji wa Kamisheni
ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa Dkt.
Carlos Lopez alisema kuwa japokuwa
Afrika imechelewa kufanya mapiduzi ya
viwanda ikilinganishwa na yale ya Ulaya
miaka 200 iliyopita, bado Afrika ina nafasi
kubwa ya kunyanyua uchumi wake kupitia
viwanda na biashara ya ndani baina ya
nchi zake.
Kilele cha Mkutano wa 27 wa Wakuu wa
Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika
unatarajiwa kufunguliwa tarehe 17-18 Julai
ambapo Wakuu hao wanatarajiwa
kupitisha ajenda kadhaa ikiwemo
uchaguzi wa Kamishna na Kauli Mbiu ya
mwaka huu ambayo ni Haki za Binadamu,
Haki za Wanawake.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki
17 Julai 2016.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top