Uchakachuaji wa mbegu umelalamikiwa na wakulima mkoani Arusha.soma zaid.
Wakulima wa Kijiji cha King`ori wilaya
ya Arumeru mkoani Arusha
wamelalamikia baadhi ya
wafanyabiashara wanaochakachua mbegu
na kuwauzia wakulima mbegu feki
zinazochangia kuzorota kwa kilimo na
kuwakwamisha wakulima.
Wakulima hao Peter Kessy na Kanankira
Mbise wamesema kuwa mavuno machache
yaliyopatikana katika msimu huu wa
mavuno yamechangiwa kwa kiasi kikubwa
na mbegu feki ,mabadiliko ya hali ya hewa
pamoja na kupanda kwa bei ya pembejeo.
Wakizungumza katika shamba darasa
lililoandaliwa na kampuni ya Mbegu ya
Seedco wamesema kuwa tatizo la mbegu
feki ,dawa feki na mbolea feki limekua
likiwaumiza wakulima wengi kutokana na
uelewa mdogo walionao juu ya pembejeo
na matumizi yake.Diwani wa kata ya
King`ori Peter Kessy anapendekeza
kuwepo na vituo maalumu cha uuzaji wa
mbegu katika vijiji na kata ili kuepuka
tatizo la uchakachuaji wa mbegu
linalowaathiri wakulima wengi.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Mbegu ya
SEEDCO Kanda ya Kaskazini Daniel
Mwambugi amesema kuwa kampuni hiyo
inayosambaza mbegu bora za mahindi na
mboga mboga imekua ikiingia mikataba na
wasambazaji wa mbegu ili kuzuia
uchakachuaji pia kuna alama ya utambuzi
ambayo hutumika kutambua mbegu hizo
hivyo amewataka wakulima kuwa makini
katika ununuaji wa mbegu.
“Tunawashauri wakulima watumie mbegu
zinazoendana na hali ya tabia ya nchi
katika maeneo husika ili waweze kupata
mavuno bora ,tunazo mbegu za muda
mrefu na muda mfupi lakini pia
tunawahamasisha kutumia mbegu bora
ambazo ni Seedco ili waweze kuvuna kwa
wingi” Alisema Daniel
Meneja wa Seedco upande wa mbegu za
Mboga mboga Joyce Mbise alisema kuwa
kampuni hiyo imeanza kusambaza mbegu
hizo tangu mwaka jana hivyo ni fursa kwa
Watanzania kuchangamkia kilimo cha
mboga mboga ili waweze kukuza kipato
cha mkulima na kuboresha lishe ya
familia.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Mbegu ya
SEEDCO Kanda ya Kaskazini Daniel
Mwambugi akitoa maelezo juu ya Mbegu
za mahindi za kampuni hiyo
zinazostahimili ukame na kumuwezesha
mkulima kupata mavuno mengi katika
shamba darasa lilipo kata ya King`ori
wilaya ya Arumeru mkoani Arusha
Akiwaonyesha wananchi ambao ni
wakulima waliouthuria shamba darasa la
kampuni hiyo.Habari picha na Woinde
shizza,Arusha
0 comments :
Post a Comment