Jeshi ka Syria limesema litapunguza upigaji wake wa makombora katika eneo la mashariki ya Aleppo.
Jeshi la Syria limesema litapunguza upigaji
wake wa makombora katika eneo la Mashariki
la Aleppo linaloshikiliwa na waasi, ambako
mamia ya raia wameuawa wakiwemo watoto,
katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya
habari, jeshi hilo limesema limechukua uamuzi
baada ya mafanikio yaliyoyapata katika
operesheni zake ilizofanya Allepo.
Limesema upunguzaji huo wa mashambulizi ya
anga na mizinga utaruhusu wakaazi wa maeneo
hayo kwenda kuishi katika maeneo salama
iwapo watataka.
Mashambulizi hayo ya hivi karibuni yaliyokuwa
yakifanywa na serikali na kuungwa mkono na
Urusi yameshutumiwa vikali, Yalifanyika muda
mfupi tu baada ya kuvunjika kwa makubaliano
ya kusitisha mapigano.
0 comments :
Post a Comment