Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, October 6, 2016

Mswada wa masharti ya uwalimu yaja.soma zai

Serikali inakamilisha Muswada wa Sheria
utakaoweka wazi sifa za walimu wakiwamo wa
vyuo vikuu, msingi na sekondari nchini.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Elimu,
Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,
Profesa Joyce Ndalichako katika kongamano la
kujadili hali halisi ya elimu nchini lililoandaliwa
na walimu wastaafu.
Profesa Ndalichako alisema serikali pia
inaandaa mpango wa kuanzisha chombo
maalum cha kitaaluma kitakachosimamia walimu
kwa mujibu wa sheria.
Alisema muswada huo utakapokuwa tayari
utawasilishwa bungeni.
Alisema pamoja na mambo mengine, utataja
sifa za mwalimu mkuu na mkuu wa chuo
kuondoa dhana kwamba ualimu ni kazi ya
walimu mazoea.
“Ni lazima kuwe na sheria inayoweka wazi sifa
ya mwalimu mkuu wa chuo kikuu na sifa za
kuweza kujiunga na chuo cha ualimu.
“Siyo kuweka tu sheria zisizojieleza hali ambayo
imesababisha taifa kuwa na wasomi wasiokuwa
na sifa.
“Ili tuweze kufikia katika mpango wa kutoa elimu
bora ni lazima tuchukue hatua zinazostahiki kwa
manufaa ya taifa ingawa unapochukua hatua
Watanzania wengi wanalalamikia suala hili ila
ukweli utabaki kuwa ukweli.
“Nchi haiwezi kuendeshwa na walimu wasiokuwa
na sifa kwa sababu kitakachozalishwa pia
kitakuwa ni mtihani na aibu kwa nchi.
“Kama kuna mwalimu yeyote ambaye anajijua
hana sifa na amekalia kiti hicho kwa zaidi ya
miaka 10 atambue kuwa hicho kiti atakiacha.
“Serikali hii ya awamu ya tano hatutaki kuwa na
walimu wasiokuwa na sifa, bora kujiengua
mwenyewe,”alisema Profesa Ndalichako.
Waziri alisema changamoto kubwa inayoikabili
wizara yake ni utekelezaji wa mipango endelevu
ya wizara ambayo ni mizuri lakini utekelezaji
wake ni mdogo kutokana na kuingiliana kwa
mipango ya maendeleo endelevu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top