Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, October 6, 2016

NBS na shilika lisilo la kiserekali la marekani ICP ina mpango wa kufanya utafiti ili kubaini maambukizi mapya ya Ukimwi.soma zaid

Babati. Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) na shirika lisilo la kiserikali la
Marekani la ICAP, ina mpango wa kufanya utafiti
ili kubaini watu wenye maambukizi mapya ya
virusi vya ukimwi (VVU) na kujua maendeleo ya
wanaotumia dawa za kufubaza virusi hivyo
(ARV).
Akizungumza na wataalamu wa afya wa wilaya
za Mkoa wa Manyara mjini hapa, Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano wa ICAP, Mihayo
Bupamba amesema watatumia mikoa ya
Manyara, Singida na Dodoma kufanya utafiti
huo.
Bupamba amesema wanalenga kufanya utafiti
kwa kaya 16,000 nchi nzima ili kuangalia namna
ya kuwasaidia waathirika na wanakusudia kutoa
elimu kwa wanaotumia ARV.
Amesema hadi sasa watu wanaoishi na virusi
vya ukimwi katika Bara la Afrika wamefikia
milioni 25.8 na hiyo ni idadi kubwa kwa nchi
zinazoendelea.
Bupamba amesema lengo lingine la utafiti huo ni
kuisaidia Serikali isiendelee kupoteza nguvu kazi
ya Taifa. “Wapo watu wanaoishi na virusi vya
ukimwi na wanaendelea vizuri na kazi za ujenzi
wa Taifa kwa kuzingatia masharti ya madaktari
na sisi ICAP tumeona ni vizuri kuendelea kutoa
elimu kupitia utafiti huo, ”amesema.
Ameongeza kuwa: “Tunataka kufahamu uelewa
wa wananchi juu ya ugonjwa huu na kupata
maoni ya wahusika na utafiti huu utahusisha
rika zote bila kubagua na kwa mara ya kwanza
hata watoto ambao hawajawahi kushirikishwa
watapimwa”.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top