Saed Kubenea amepandishwa mahakamani kwa upotoshaji.soma zaid
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea
amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa
na mashitaka ya kuandika makala ya kupotosha
na kusababisha hofu kwa jamii.
Kubenea, ambaye ni mbunge kwa tiketi ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), alifikishwa mahakamani hapo jana
na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali,
Dereck Mukabatunzi mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu, Wilbard Mashauri.
Wakili Mukabatunzi alidai kuwa Julai 25, mwaka
huu katika Mtaa wa Kasaba, Manispaa ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam, Kubenea
alichapisha habari ya uongo inayoweza
kusababisha hofu na taharuki kwa jamii au
kuondoa amani.
Inadaiwa Kubenea alichapisha makala hiyo
kwenye gazeti la Mwanahalisi la Julai 25 hadi
31, mwaka huu, lenye namba 349 ISSN:
1832-5432 ikiwa na kichwa cha habari “Yuko
wapi atakayeiokoa Zanzibar”.
Baada ya kusomewa mashitaka, Kubenea
alikana kutenda kosa hilo na upande wa
Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo
umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa
ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya
awali.
0 comments :
Post a Comment