Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, October 5, 2016

Wanasheria wa CUF wakishirikiana na Tundu Lissu watalajia kufungua kesi mahakamani dhidi ya Prof Lipumba soma zaid

Kufuatia mgogoro uliopo katika Chama cha
Wananchi (CUF) baina ya uongozi wa chama
hicho na Profesa Ibrahim Lipumba waliyemfuta
uanachama, viongozi wa CUF wamepanga
kwenda mahakamani ili wapate suluhu ya
kisheria.
Jopo la Mawakili wa CUF wakiongozwa na
Mwanasheria Tundu Lissu linataraji kufungua
mashitaka mahakamani dhidi ya Lipumba na
kundi lake wiki ijayo.
Kwa madai kuwa Lipumba amevamia ofisi za
chama hicho na kuikalia kinyume cha sheria
pamoja na kuharibu baadhi ya mali za chama
hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, Julias
Mtatiro wakati akizungumza na mtandao wa heura blog
kwa njia ya simu, amesema mawakili hao
watakutana siku ya Ijumaa au Jumamosi ili
kuandaa mashitaka na kwamba yatafunguliwa
rasmi mahakamani kuanzia wiki ijayo.
“Mawakili watakutana Ijumaa hii au Jumamosi
ili wiki ijayo waanze kufanya hiyo kazi ya
mahakamani,” amesema Mtatiro.
Hata hivyo, Bodi ya Wadhamini ya CUF hapo
jana ilitoa tamko la kutaka kuchukua hatua za
kisheria dhidi ya Lipumba ili alipe gharama za
hasara, ilizodai kuwa Lipumba alizisababisha
baada ya kuvamia Mkutano Maalumu wa Taifa
wa CUF uliovurugika Agosti 21, 2016 katika
Ukumbi wa Blue Pearl , Ubungo Plaza.
Bodi hiyo ilidai kuwa hasara iliyosababishwa na
Lipumba kwa kuvuruga mkutano huo ni Milioni
600, na takribani milioni 50 kwa kuvamia ofisi
ya chama hicho iliyopo Buguruni jijini Dar es
Salaam na kufanya uharibifu wa mali za chama
hicho zenye thamani ya fedha hiyo.
Bodi hiyo ilisema itachukua hatua za kisheria
zaidi kwa mujibu wa katiba ya chama hicho
kurejesha chini ya himaya yake, mali za chama
ikiwemo jengo la ofisi ya chama hicho kutoka
mikononi mwa Lipumba.
Aidha, baada ya bodi hiyo ya wadhamini kutoa
tamko la kumshitaki na kutomtambua Prof.
Lipumba. Upande wa Lipumba ulidai kuwa bodi
hiyo haina baraka na mamlaka ya kuamua jambo
lolote juu ya Lipumba.
Abdul Kambaya, aliye karibu na Lipumba
ameuambia mtandao wa Modewjiblog.com kuwa
maamuzi ya kikao cha bodi hiyo hayakuwa halali
kwa kuwa akidi ya wajumbe halali haikutimia.
Ndipo mtandao huu ulipomuhoji Mtatiro zaidi juu
ya ufafanuzi wa malalamiko hayo.
Mtatiro amefafanua kuwa, kikao cha bodi ya
wadhamini kilichoketi juzi, kilikaliwa na
wajumbe halali 6, na kwamba wajumbe 3
hawakuhudhuria, ambapo wawili ni wafuasi wa
Lipumba wakati 1 hakuhudhuria kutokana na
kupata udhuru ya safari kwa siku hiyo.
“Idadi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini iko 9,
waliofanya kikao 6 akidi hii ni halali na
angekuwepo yule mmoja aliyepata dharura ya
safari wangekuwa saba, Lipumba amebaki na
wajumbe wa bodi wawili tu,” amesema.
Mtatiro amesema maamuzi yoyote
yatakayotolewa na bodi hiyo ni halali kwa kuwa
akidi ya wajumbe wake ingawa pungufu lakini
inatambulika na kuruhusiwa kisheria.
Pia kumekuwepo na tuhuma kutoka upande wa
Lipumba kuwa miongoni mwa sababu ya
mgogoro wa chama hicho, ni masilahi binafsi
baina ya upande wa Zanzibar na Bara kwa madai
kuwa Zanzibar inanufaika na ruzuku za chama
hicho kuliko Bara.
Mtatiro amefafanua kuwa, upande wa Bara ndio
unaofaidi ruzuku za chama hicho kuliko Zanzibar
na kusema kuwa Baraza Kuu la Uongozi la CUF
linatoa asilimia 70 ya ruzuku ya chama hicho
Bara kwa kuwa ina wilaya nyingi za kichama.
Na kwamba Zanzibar inapokea ruzuku ndogo ya
asilimia 30 kwa sababu ina idadi ndogo za
wilaya.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top