Baadhi ya vijana wa kenya wapewa silaha kwa lengo la kuvuruga amani wakati wa uchaguzi mkuu.soma zaid
Serikali ya Kenya leo imetoa taarifa ya kutisha
kuhusu idadi ya makundi ya vijana wanaopewa
silaha kwa lengo la kuvuruga amani wakati nchi
hiyo inapojiandaa kwa uchaguzi mkuu baadae
mwaka huu. Joto la kisiasa linazidi kupanda
nchini humo, na ripoti hiyo inasema kuwa baadhi
ya wanasiasa wameanza kutumia mbinu za
kuwatisha wapinzani wao na kuvuruga mikutano
ya kampeini za uchaguzi. Riopoti hii inatolewa
kufuatia cheche za maneno ambazo zimetanda
katika muda wa wiki moja iliyopita baada ya
serikali kuwapokonya walinzi wao, Gavana wa
Jimbo la Mombasa, Ali Hassan Joho na
mwenzake wa Jimbo la Kilifi, Amason Kingi
katika ukanda wa Pwani.chanzo DW swahili.
0 comments :
Post a Comment