Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, January 11, 2017

Kutoka Arumeru mkoan Arusha Edwaed Lowassa kayasema haya.soma zaid

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa
amesema uwezekano wa vyama vya upinzani
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kushinda katika uchaguzi wilayani
Arumeru, mkoani Arusha ni mdogo.
Amesema hali hiyo inatokana na uamuzi wa
vyama hivyo kila kimoja kusimamisha mgombea
udiwani katika Kata ya Matevesi, kinyume na
makubaliano.
Lowassa alisema hayo katika kampeni za
kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo.
Alisema kilichofanywa na vyama vya upinzani ni
kugawa kura, wakati upinzani ulikuwa na nafasi
kubwa ya kushinda.
Alisema vyama vinavyounda Ukawa vya
Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, kila kimoja
kimesimamisha mgombea udiwani katika kata
hiyo, kwa hali hiyo uwezekano wa kushinda ni
mdogo sana, hivyo kukipa mwanya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kushinda kiti hicho.
Akizungumza katika kampeni za Chadema
zilizofanyika katika Kitongoji cha Ematasia,
Lowassa alisema vyama hivyo tayari
vimeshafanya kosa la kiufundi, linaloweza
kusababisha vyama hivyo ‘kuangukia pua’ katika
uchaguzi huo na kuiwezesha CCM kuibuka na
ushindi asubuhi na mapema.
Alisema CCM ina nafasi kubwa ya kushinda
katika uchaguzi huo, kutokana na kuwa na
uhakika wa kura zake, kutokana na kutokuwa na
upinzani wa chama kingine chenye mrengo wake,
kama ilivyo kwa vyama hivyo vya Ukawa,
ambavyo viko katika hatari ya kugawa kura.
“Nyie tayari mmeshafanya makosa makubwa ya
kiufundi kwa kila chama cha Ukawa kusimamisha
mgombea wake, hapo ndipo CCM wanaposhindia,
kwa hiyo mwendelee mkijua mna kazi kubwa
kushinda,” alisema Lowassa.
Katika hali ya kushangaza Lowassa alijikuta
akimuombea kura mgombea wa CCM, Julius
Savoyo aliposema wananchi wa kata hiyo
wanapaswa kumpa kura na kumuweka
madarakani mgombea aliyeshinda katika
uchaguzi uliopita wa mwaka 2015, pasipo kujua
diwani aliyeshinda wakati huo na kutenguliwa na
mahakama ni wa CCM.
“Wananchi wa kata hii hamna kazi ngumu katika
uchaguzi pamoja na makosa yaliyofanywa na
vyama vya Ukawa, hakikisheni mnamrejeshea
udiwani yule aliyeshinda wakati ule ili aendelee
na kazi yake,” alisema Lowassa.
Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa
kampeni za CCM, Katibu wa Siasa na Uenezi wa
CCM Mkoa wa Arusha, Shaaban Mdoe alisema
kitendo kilichoonekana na Lowassa kuwa ni kosa
kusimamisha wagombea wa vyama vya Ukawa ni
utabiri mzuri wa ushindi kwa CCM, kama
alivyosema tena katika kampeni za uchaguzi wa
Urais mwaka juzi.
Hata hivyo, Mdoe alisema suala la Ukawa kwa
sasa halipo tena, bali ni Ukiwa na ndiyo maana
kila chama cha muungano huo, kinajaribu bahati
yake kutokana na kuvunjika kwa ndoa hiyo ; na
wa mwisho kuondoka katika ndoa hiyo, alikuwa ni
Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James
Mbatia.
Mdoe alisema kitendo cha Lowassa kumnadi
mgombea wa CCM, si bahati mbaya bali ni ukweli
uliopo ndani ya moyo wake, kwa kuwa hata
akijifungia chumbani kwake peke yake, anakubali
kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Rais John
Magufuli.

     
     

0 comments :

Post a Comment

Back To Top