Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, January 12, 2017

Mwana sheria wa CHADEMA Tundu Lissu azungumzia kifungo cha mh.Lijualikali na mh.Lema.soma zaid


Tundu Lissu: Kabla Mhe. Lijualikali ajawa
Mbunge alikuwa diwani wa Ifakara mjini,
alipata kura nyingi sana.
Tundu Lissu: Hii Vita ni ya siku nyingi
toka mwaka 2012, kabla hajawa diwani
hakuwahi kuna kesi Polisi, baada ya kuwa
diwani amekuwa na kesi 6.
Tundu Lissu: Kesi zote hizi zimekuwa na
sura za kisiasa, wakati Uchaguzi wa 2015,
alikuwa na kesi 3.
Tundu Lissu: Mlimba na Kilombero
tumeshinda kote huko, mara baada ya
Uchaguzi Mkuu Vita na Mhe. Lijualikali
ikaanza rasmi.
Tundu Lissu: Wakati Mbunge wa
Kilombero akiwa wa CCM hakukuwa na
shida lakini baada Mbunge wa CHADEMA
kushinda kumekuwa na shida kubwa.
Tundu Lissu: Mhe. Lijualikali ni mfungwa
wa kisiasa, amefungwa kwa sababu ya
vita ya ccm na Upinzani.
Tundu Lissu: Mhe. Lema na Mhe.
Lijualikali ni wafungwa wa kisiasa,
wasifikirie kumfunga Lijualikali CCM
itapendwa Kilombero wasahau.
Tundu Lissu: Wasidhanie kumfunga
Lijualikali wanamuondolewa sifa za kuwa
Mbunge, Katiba ibara 67 .2 (c) inaeleza.
Tundu Lissu: Mara baada ya kupata
taarifa, tumeanza taratibu za kukata
rufaa,baada ya siku 3 tutakuwa
tushakamilisha taratibu za kukata rufaa.
Tundu Lissu: Kuhusu Lema hatuwezi
kukubali wakaendelea kumnyanyasa Lema
kwa sababu za kisiasa, wakipiga
danadana dhamana yake.
Tundu Lissu: Siku ya Jumamosi mimi na
M/kiti Taifa ,Mhe. Mbowe tutakwenda
kumtemebelea Lema gerezani na kuongea
na waandishi wa habari.
Tundu Lissu: Hata kama Mhe. Lijualikali
alimpiga kweli askari, ingawa tunajua sio
kweli, lakini haiwezi kumfutia sifa za
kugombea Ubunge.
Tundu Lissu: Haya masuala ya kukamata
wabunge kuwasafirisha usiku zaidi ya
500km ni mambo ya ajabu,shtaka lenye
dhamana lakini wanafanya siasa.
Tundu Lissu: Kuna wajinga wanadhani
kufungwa kwa Mhe. Lijualikali atapoteza
ubunge wake, washauri wao
wanawadanganya.
Tundu Lissu: Wanatumia Jeshi la Polisi
na watu kama wakina Lipumba katika
Vita hii ya kisiasa, mambo haya
yanaharibu sifa ya Nchi huko nje.
Tundu Lissu: Lengo lilikuwa kumfunga
Mhe. Lijualikali kabla ya Uchaguzi, Mhe.
Lijualikali ana haki ya kuchagua M/kiti wa
Halmashauri.
Tundu Lissu: Tuna Rais wa ajabu
haijawahi kutokea, mwaka 1963 tulipatwa
na njaa,Nyerere hakuona aibu kusema
tuna njaa.
Tundu Lissu: Rais huyu ni wa kwanza
kuwatakia Watanzania wenye njaa
hatowapa chakula, Nyerere hakuona aibu
kusema tuna njaa.
Tundu Lissu: Kwa suala la Kagera na
Njaa, tunapaswa kupinga haya kwa kila
Mwenye akili, Rais ameenda Kagera
kuwatusi Watanzania.
Tundu Lissu: Rais sio Chief Commander
tu, ni Chief Comforter, Rais anatakiwa
aongee vizuri ni Mfariji Mkuu tunapokuwa
kwenye majanga.
Tundu Lissu: Mbona Serikali iliomba
msaada na haikubeba msalaba wake
kwenye tetemeko Kagera,tukiendelea
kumnyamazia watu watahangamia.
Tundu Lissu: Tukiendelea kunyamazia
hizi kauli za Magufuli watu wetu
watahangamia, shime kwa kila Mwenye
akili timamu kuzipinga.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top