Katibu mkuu mpya Guterree ameahidi kuzua na kupambana na migogoro duniani kote.
Guterres kufanya mabadiliko ya kuzuia migogoro
Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa,
Antonio Guterres, amelitaka Baraza la Usalama la
umoja huo, kuchukua hatua zaidi kuzuia
migogoro duniani kote huku akiahidi kuimarisha
uwezo wa upatanishi wa umoja huo.
Guterres, Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno na
aliyekuwa mkuu wa shirika la kuhudumia
wakimbizi la Umoja wa Mataifa, amesema nafasi
nyingi za kuzuia migogoro zimepotezwa kwa
sababu hakuna uaminifu miongoni mwa mataifa
mbalimbali pamoja na kuwepo wasiwasi juu ya
uhuru wa nchi zao. Akilihutubia Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara ya
kwanza, tokea aupokee wadhifa huo kutoka kwa
Katibu Mkuu aliyemtangulia Ban Ki-moon,
Guteress ameahidi kufanya mabadiliko ndani ya
Umoja wa Mataifa.
Mwandiplomiasia huyo mwenye umri wa miaka
67, anatarajiwa kujihusisha zaidi katika migogoro
inayoendelea duniani kuliko mtangulizi wake,
ambaye jitihada za upatanishi aliwaachia zaidi
wajumbe wake maalum.
"Kinga lazima iwe kipaumbele chetu cha
kawaida. Ukweli ni kwamba, tukizuia migogoro
kutokea tunaweza kuepuka na mateso.
Tukiepusha migogoro tutaepukana na uharibifu.
Ni vyema zaidi kuzuia mgogoro, kuliko kuitikia,”
amesema Antonio Guterres.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa
Baraza hilo la Umoja wa Mataifa, kwa kiasi
kikubwa limekosa maafikiano juu ya vita ya
miaka sita vya Syria vilivyosababisha vifo vya
zaidi ya watu 310,000, wakati Urusi na China
wakiendelea kupingana na Marekani, Uingereza
na Ufaransa kuhusu mgogoro huo wa Syria.
Umoja huo pia umegawanyika juu ya mbinu
nyingine za kutumia katika migogoro na majanga
kama vile ya Sudan Kusini na Burundi, na baadhi
ya washirika wakitoa sababu ya kuwa na
wasiwasi juu ya uhuru wa nchi zao.
Guterres amelitaka Baraza la Usalama kutumia
kifungu cha sita cha mkataba wa Umoja wa
Mataifa, ambacho kinauruhusu umoja huo
kufanya uchunguzi na kupendekeza taratibu za
kutatua migogoro, ambayo hatimaye inaweza
kuhatarisha amani na usalama.
Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa, aliainisha
hatua anazozichukua kuimarisha uwezo wa
Umoja wa Mataifa wa kuzuia migogoro, na
kusema kuwa umoja huo umegawanyika kwa
sasa. Ameunda kamati ya utendaji, itakayokuwa
na kazi ya kuviunganisha vikosi vyote vya umoja
huo. Pia ameteua afisa mwandamizi,
atakayechanganisha uwezo wa Umoja wa
Mataifa wa kuzuia migogoro ili kupatikane hatua
imara zaidi.
Baaade wiki hii, Guteress atafanya ziara yake ya
kwanza kama Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa. Ataelekea mjini Geneva, Uswisi
kushuhudia mazungumzo ya amani kuhusu kisiwa
cha Cyprus kilichogawanyika kati ya upande wa
Ugiriki na Uturuki. Na, atarudi tena Geneva wiki
inayofuata kukutana na Rais wa China, Xi
Jinping, ambaye ushirikiano wake na Umoja wa
Mataifa umekuwa ukiongezeka siku za karibu.
0 comments :
Post a Comment