Hamphrey polepole atema cheche.soma zaid
Dar es Salaam.Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Hamphrey Polepole amesema kipindi cha
mwaka mmoja cha Rais John Magufuli
amefanikiwa kutatua kero mbalimbali zilizokuwa
zikilalamikiwa na wananchi wakati wa kampeni.
Miongoni mwa kero hizo ambazo Rais
amefanikiwa kupambana nazo ni vita dhidi ya
wala rushwa, ukwepaji wa kodi, wabadhirifu wa
mali za umma na uwajibikaji wa viongozi.
Polepole amesema hayo leo katika mkutano na
wanahabari uliofanyika kwenye Ofisi Ndogo za
CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam.
Amesema utekelezaji wa kero hizo kwa Serikali
ni msingi mmoja wapo wa kuhakikisha chama
hicho, kinarudi katika misingi yake ikiwamo kuwa
karibu na wananchi.
"Nawahakikishia Watanzania dhamira ya CCM ipo
pale pale ikiwa ni mkakati wa kutekeleza ilani ya
uchaguzi ya mwaka 2015-2020," alisema
polepole.
0 comments :
Post a Comment