Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, January 17, 2017

Leo Lema anatarajiwa kufikishwa mahakani.soma zaid

Arusha. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Augustino
Rwezile, leo, anatarajia kuwasomea hoja za awali
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na
mkewe, Neema katika kesi inayowakabili ya
kumtukana Mkuu wa mkoa huo, Mrisho Gambo.
Hoja hizo ilikuwa wasomewe Novemba 15, 2016
lakini zilikwama kusomwa kutokana na Lema
kuugua ghafla na Wakili wa Serikali, Elizabeth
Swai kumuomba hakimu kutumia busara ya
Mahakama kuisogeza mbele kesi hiyo kutokana
na hali ya mbunge huyo.
Lema bado anasota rumande kwa siku 76 tangu
Novemba 2, mwaka jana baada ya kukosa
dhamana katika kesi inayomkabili ya tuhuma za
kutumia lugha ya uchochezi dhidi ya Rais John
Magufuli.
Kutokana na sababu hiyo, Hakimu Rwezile pia
amwahirisha kesi ya kuhamasisha maandamano
ya Ukuta inayomkabili mbunge huyo na ile ya
kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Gambo
unaodaiwa kuwa na matusi hadi leo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top