Meli za kivita za Nigeria zimeanza kuelekea Gambia.soma zaid
Nigeria imethibitisha kuwa meli ya yake
ya kivita inaelekea Gambia kama mazoezi
wakati nchi za kanda zinajianda
kuichukulia hatua za kijeshi Gambia.
Rais mteule Adama Barrow kwa saa yuko
Senegal na anatarajiwa kuapishwa kesho,
lakini Rais Yahya Jammeh anataka
matokeo ya mwezi uliopita yafutwe na
amekataa kuondoka madarakani.
Jana shirika la habari la Reuters liliripoti
kuwa mataifa ya magharibi mwa Afrika,
yalikuwa yana andaa kikosi cha pamoja
cha kuingilia kijeshi ikiwa Jammeh
hataondoka madarakani.
Sasa shirika la habari la AP limemnukuu
msemaji wa jeshi la wanamaji la Nigeria
akisema kuwa jeshi la wanahewa la nchi
yake linachangia wanajeshi 200 kwa
kikosi hicho cha pamoja.
Chanzo: BBC
0 comments :
Post a Comment