Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Friday, May 5, 2017
Mwanajeshi mmoja wa Kimarekani ameuwawa  nchini Somalia na kundi la Al- Shababi. Soma zais

Mwanajeshi mmoja wa Kimarekani ameuwawa nchini Somalia na kundi la Al- Shababi. Soma zais

Mwanajeshi mmoja wa Kimarekani ameuwawa
nchini Somalia wakati wa operesheni ya pamoja
na jeshi la Somalia dhidi ya wanamgambo wa
kundi la itikadi kali la Al Shabab. Taarifa
zinaongeza kusema wanajeshi wengine wawili wa
Kimarekani pia wamejeruhiwa na kwamba kikosi
cha wanajeshi hao kilikuwa kinaendesha shughuli
ya kutoa ushauri na kusaidia katika opereresheni
hiyo sambamba na jeshi la taifa la Somalia.chanzo DW swahili.

Mauaji ya kutumia risasi yametokea wilayani Rufiji. Soma zaid

Mauaji ya kutumia risasi yametokea wilayani Rufiji. Soma zaid

Mtu mmoja Aitwae Amri Chanjale (55),
mkazi wa kitongji cha Makaravati katika
Kijiji cha Umwe Kusini wilayani Rufiji
ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa
nyumbani kwake.
Tukio hilo limetokea jana saa 1.30 usiku
baada ya watu wasiojulikana kufika kwake
na kutekeleza shambulio hilo.
Marehemu huyo ambaye pia ni
mwanachama wa CCM ameuawa ikiwa ni
baada ya siku tano kuuawa kwa
Mohammed Malinda ambaye nae alikuwa
ni mwanachama wa chama hicho.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM
wilayani Rufiji, Musa Nyeresa
amethibitisha kuuawa kwa mwanachama
huyo kwa kupigwa risasi.chanzo jamii forums.

Thursday, May 4, 2017
Tume ya uchaguzi yamteua Catherine Ruge kuwa Mbunge wa viti maalum Chadema. Soma zaid

Tume ya uchaguzi yamteua Catherine Ruge kuwa Mbunge wa viti maalum Chadema. Soma zaid

KUHUSU UTEUZI WA CATHERINE NYAKAO RUGE KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 04 Mei, 2017 imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Dkt. Elly Marco Macha. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Dkt. Elly Marko Macha kufariki dunia na hivyo kuwepo nafasi wazi. Imetolewa leo tarehe 04 Mei, 2017 na:- Kailima, R.K MKURUGENZI WA UCHAGUZI

Kauli ya Rais Magufuri yaleta neema Tanesco.soma zaid

Kauli ya Rais Magufuri yaleta neema Tanesco.soma zaid

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) Mkoa wa Ilala limekusanya Sh2 bilioni
kutoka katika taasisi za Serikali zilizokuwa
zinadaiwa na shirika hilo.
Deni hilo limekusanywa tangu Rais John Magufuli
atoe agizo la kulitaka shirika hilo kuwakatia
umeme wadaiwa sugu.
Akizungumza leo Meneja wa Tanesco Mkoa wa
Ilala, Athanasius Nangali amesema wadaiwa sugu
walikuwa wanadaiwa jumla ya Sh 7 bilioni.
Taasisi za Serikali zilikuwa zinadaiwa Sh 6 bilioni
na sasa wamelipa Sh 2 bilioni na zimebaki Sh 4
bilioni.
"Tumeingia mkataba na taasisi za serikali wa
namna ya kulipa madeni yao na makubaliano ni
kuwa watamaliza deni lililobaki mwezi huu hadi
mwezi ujao," amesema.

Kigogo asimamishwa kazi kwa kupora hekari 4,000.za aridhi. Soma zaid

Kigogo asimamishwa kazi kwa kupora hekari 4,000.za aridhi. Soma zaid

Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
amemsimamisha kazi Afisa Mipango
Miji wa Lindi, Castory Manase Nkuli
baada ya kunyang`anya ardhi ya vijiji
vya Ruvu na Mchinga hekari 4000 na
kumilikisha kampuni ya Azimio
Housing Estate kinyume cha sheria.
View attachment 504370
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William
Lukuvi akimsimamisha kazi Ndugu
Castory Manase Nkuli Afisa Mipango
Miji kwa tuhuma za kumilikisha ardhi
kinyume cha sheria
Waziri Lukuvi aligundua hayo baada ya
kuona utaratibu wa umilikishaji wa
ardhi haukufuatwa na badala yake
kuonekana kuwa na mianya ya rushwa
kwa kuwa ardhi hiyo imehamishwa
kutoka ardhi ya kijiji hadi kumilikishwa
kwa kampuni ya Azimio ambapo
kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo
itoke kwa idhini ya Rais.
Afisa Mipango Miji huyo aligundulika
kuwa na kosa la kughushi kwa
kujifanya ni Afisa ardhi baada ya
kuandika barua na kuisaini kwa niaba
ya Afisa ardhi wakati yeye ni Afisa
Mipango Miji ili kuimilikisha kampuni
ya Azimio Housing Estate ambalo pia
ni kosa kisheria.
“Kama nyie hamna uwezo wa
kumfukuza kazi basi mie
namsimamisha kazi kuanzia leo hafai
kuwa mtumishi wa serkali” alisema
Lukuvi huku akiagiza eneo hilo lirudi
na kuwa mali ya serikali. Sasa hiyo
ardhi lazima irudi itakua mali ya
serikali kuanzia leo”.
Akithibitisha makosa hayo Kaimu
Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji
kutoka Wizara ya Ardhi Bi Immaculate
Senje amesema kwamba utaratibu wa
umilikishaji wa ardhi hiyo haukufuatwa
ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo
hilo itoke kwa idhini ya Rais na baada
ya Tangazo la Serikali na kuridhiwa na
wana kijiji.
Chanzo: Bongo 5
Mh. Waziri Lukuvi hilo likampuni la
Azimio Housing Estate nalo ni
lakunchunguzwa kwa kina sana,
Limekaa kidili

Tuesday, May 2, 2017
Rais wa Afrika kusini Jacobo amezomewa akihutubia nakushindwa kuhutubia siku ya wafanyakazi. Soma zaid

Rais wa Afrika kusini Jacobo amezomewa akihutubia nakushindwa kuhutubia siku ya wafanyakazi. Soma zaid

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
ashindwa kumalizia hotuba yake katika
maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi nchini
humo,baada ya wafanyakazi wanaotaka ajiuzulu
kuanza kumzomea.
Mvutano mkubwa uliibuka kati ya wanaomuunga
mkono Rais Zuma na wanaompinga hali
iliyomfanya Rais Huyo kuondoka.

Monday, May 1, 2017
Watoto wa vigogo ndio wanaoishi vyeti feki.

Watoto wa vigogo ndio wanaoishi vyeti feki.

Mtoto wa masikini hawezi kukugushi vyeti feki wanaogushi vyeti feki ni watoto wa vigogo.rais magugu amesema.

Back To Top