Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Thursday, June 15, 2017
Roma,Mr.Blue, Darassa na Snura kupiga shoo kali Dar Live Idd mosi.soma zaid

Roma,Mr.Blue, Darassa na Snura kupiga shoo kali Dar Live Idd mosi.soma zaid

Shoo ya Dar Live sasa Naye Meneja na Mratibu wa Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, Juma Mbizo alisema baada ya R.O.M.A kufanya yote hayo ya kijamii, mashabiki wake wote waliommis jukwaani watarajie shoo ya nguvu katika Sikukuu ya Idd Mosi. “Shoo itatambulika kama Nishushe Dar Live ambapo Roma akiwa na wasanii kibao wakiongozwa na Mr. Blue wataliamsha dude ndani ya Dar Live na kugonga nyimbo zake zote zinazobamba. “Nikukumbushe tu mara ya mwisho kwa R.O.M.A kupiga shoo ya kihistoria ilikuwa mwaka jana katika Mkesha wa Mwaka Mpya ambapo alipanda jukwaa moja na mkali, Darassa na kuzoa kijiji. sasa safari hii jibu utatoa mwenyewe akishuka jukwaani,” alisema Mbizo. WENGINE SASA Mbizo aliongeza listi kuwa mbali na Mr.Blue na R.O.M.A mashabiki wategemee jukwaa kufunikwa na wakali wa Hip Hop kama Darassa na Stamina huku Snura akiwarushia vyura jukwaani. Shoo ya watoto nayo ndani Mbizo aliongeza kuwa, mbali na shoo hizo pia pazia la burudani litafunguliwa Sikukuu ya Idd Mosi mapema kuanzia saa 2:00 asubuhi kwa kundi la sarakasi lisilo na mpinzani Bongo, Wakali Dancers pamoja na wakali wa nyimbo za Asili, Makhirikhiri kutoka Tanzania ambao wataliamsha kwa kutoa burudani kwa watoto. “Kutakuwa na michezo mingi ya watoto kama vile kubembea, kuteleza, kuogelea, kucheza ndani ya ndege na mingine mingi. “Katika kunogesha burudani kwa watoto, kwa mara ya kwanza mkali wa vichekesho anayebamba katika Kipindi cha Ze Comedy, Bambo atakuwepo kuvunja mbavu za watoto wote watakaojitokeza huku akigawa zawadi ndogondogo kwa watakaotoka chicha. Zanzibar Stars kuibuka Baada ya kupotea kwa muda, kundi kongwe la Muziki wa Mwambao, Zanzibar Stars linatarajiwa kuibuka kwa mara ya kwanza ndani ya Dar Live likiwa na vichwa hatari kama Bi. Mwanahawa, Sabaha Mchacho, Jokha Kassim, Mosi Suleiman, Ally Jay, Zubeda Mlamali na wengine kibao. Mtonyo sasa! Mbizo alimaliza kwa kutaja kiingilio kwa siku hiyo kuwa, burudani kwa wakubwa itakayoanza saa 2:OO usiku itakwenda kwa shilingi 7,000 huku watoto ikiwa shilingi 3,000 tu!

Wednesday, June 14, 2017
no image

Mtoto afariki ndani ya Gari baada ya Mama yake kwenda kula raha na mpenzi wake.soma zaid

MTOTO wa miaka nane alifariki jana Jumapili huko Bumula, katika Kaunti ya Bungoma nchini Kenya, wakati mama yake alipomwacha katika gari lililofungwa. Mwanamke huyo na mpenzi wake wanasemekana walikwenda katika chumba cha nyumba ya wageni karibu na soko la Mateka na kumwacha mwanawe ndani ya gari likiwa limezimwa na kufungwa kabisa madirisha. Mkuu wa Polisi wa Mateka Julius Barasa alisema mwanamke huyo alitambuliwa kama Christine Nasimivu. “Walimwachia chupa tatu za soda lakini mtoto alifariki kutokana na kukosa hewa safi,” alisema afisa huyo wa polisi. Polisi waliwaokoa wawili hao kutoka kwa wananchi wenye hasira ambao walikuwa wanataka kuwanyonga. Wawili hao walikamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi cha Bumula wakati mwili wa mtoto ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya Bungoma. Joseph Lupao, afisa mwangalizi wa watoto, aliwashutumu wawili hao kwa kumwacha mtoto peke yake ndani ya gari. “Hii ni ajabu na jambo bay asana – mtoto amefariki kutokana na uzembe. Wanapaswa kushitakiwa mahakamani,” alisema. Kulingana na tovuti ya Kidsandcars.com, watoto ambao huachwa ndani ya magari hufariki kutokana na joto la gari. Tovuti hiyo inaeleza kwamba ndani ya gari joto huongezeka kwa haraka linapokuwa limefungwa, na linaweza kufika hata nyuzi joto 125 ndani ya dakika chache. Joto hilo linasababisha joto la mwili wa mtoto kupanda na kufika zaidi ya nyuzi joto 40, na kusababisha kifo. Tovuti hiyo inasema kwamba mwili wa mtoto hupata joto kwa haraka mara tatu hadi tano zaidi ya ule wa mtu mzima.
Rais Magufuli akutana na Boss wa ACACIA leo Ikulu  kampuni imekubali kulipa deni lote wanalodaiwa na serikal.soma zaid

Rais Magufuli akutana na Boss wa ACACIA leo Ikulu kampuni imekubali kulipa deni lote wanalodaiwa na serikal.soma zaid

Rais John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Profesa John L. Thorton Ikulu jijini Dar es salaam. Kampuini Hiyo imemuahidi Rais Magufuli kulipa Deni lote wanalodaiwa na Tanzania, Katika mkutano huo, uliohudhuriwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Paramagamba Kabudi na Balozi wa Canada hapa nchini, Ian Myles umemalizika kwa mafanikio makubwa ambapo pande zote zimekubaliana kukaa meza moja kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali katika sekta ya madini.

Bunge lapigilia msumari dhidi ya hawa watu.soma zaid

Bunge lapigilia msumari dhidi ya hawa watu.soma zaid

Bunge limeitaka Serikali kuchukua hatua
kali dhidi ya wote watakaothibitika
kuhusika kuliingizia Taifa hasara na
kuwakosesha Watanzania fursa ya
kufaidika na rasilimali za madini.
Hoja hiyo imetolewa leo Jumatano
bungeni baada ya kamati iliyoundwa jana
na Spika Job Ndugai kupata maoni ya
namna Bunge linavyoweza kuunga mkono
juhudi binafsi zinazochukuliwa na Rais
John Magufuli kukabiliana na udanganyifu
unaofanywa kwenye sekta hiyo.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa
Newala Mjini, George Mkuchika baada ya
kukamilisha taratibu zote, imetoa
maazimio matatu ambayo yamepitishwa
na Bunge.
"Bunge linamuunga mkono Rais John
Magufuli na lipo tayari kutoa ushirikiano
wa dhati kadri itakavyohitajika kuhakikisha
juhudi hizi hazipotei bure na sekta ya
madini inachangia maendeleo ya
wananchi na Taifa kwa ujumla," amesema
Mkuchika.
Kukubaliana na kinachofanywa na Rais
Magufuli maazimio matatu yametolewa
ambayo ni kumpongeza na kuunga mkono
kwa hatua anazochukua, kumhakikishia
ushirikiano wakati wowote atakapohitaji
na kushauri kuchukuliwa kwa hatua kali
za kisheria kwa watakaobainika kushiriki
kulitia taifa hasara kutokana na
kuidhinisha mikataba mibovu na wizi
uliofanywa.

Achoma moto nyumba baada ya mke wake kukataa kumfungulia mlango.soma zaid

Achoma moto nyumba baada ya mke wake kukataa kumfungulia mlango.soma zaid


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro
(ACP), Koka Moita, alisema mwenyekiti huyo
aliamua kuchukua mafuta ya petroli yaliyokuwa
kwenye pikipiki yake na kuichoma nyumba hiyo
kwa hasira kwa kile alichodai mkewe alionyesha
dharau.
“Kwa bahati nzuri hakuna vifo wala madhara kwa
binadamu yaliyotokea, lakini huyu Mwenyekiti
baada ya kufanya tukio hilo alifanikiwa kutoroka,
Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata katika Kijiji
cha Uswaa nje kidogo ya Kijiji cha Sawe akiwa
amejificha,” alisema Moita.
Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi
uliopindukia wa mtuhumiwa na wakati
anatekeleza kusudio lake alikuwa amelewa na
kumlalamikia mke wake kuwa alichelewa
kumfungulia mlango.
Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 6:00 usiku
katika Kijiji cha Sawe, Kata ya Masama
Mashariki, Tarafa ya Masama, Wilaya ya Hai.
Wakati huo huo, Shaban Juma, amefariki dunia
jana, baada ya kuangukiwa na mtungi wa zege
katika jengo la ghorofa 11 linalojengwa na
kumilikiwa na mfanyabiashara, Fredrick Shoo.
Mtungi huo ulianguka na kusababisha kifo, baada
waya ngumu inayotumika kupandishia mtungi huo
juu ya ghorofa kukatika katika ghorofa ya nane.
Jengo hilo refu kuliko yote katika mji wa Moshi,
linajengwa na Kampuni ya Wachina katika
Barabara ya Market Road.

ACACIA waeleza usajili wao.soma zaid

ACACIA waeleza usajili wao.soma zaid

KAMPUNI ya uchimbaji madini ya Acacia, imesema kuwa inafanya kazi nchini kwa misingi ya sheria na Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana (CMSA) inatambua uwepo wake. Kauli hiyo imekuja baada ya juzi taarifa ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa mchanga wa madini katika makontena yalizuiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi, kubainisha kuwa kampuni hiyo haina kibali na inafanya kazi kinyume na sheria. Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo jana pia imesema kuwa Acacia itafanya mkutano na wanahisa wake kesho kutoa ufafanuzi zaidi juu ya sakata zima. Kampuni hiyo ilieleza kuwa migodi yake ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inaendeshwa kisheria. “Acacia inapenda kuthibitisha kwamba inaendelea kufanya kazi katika migodi yake mitatu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara. “Migodi hii yote inamilikiwa na kuendeshwa na makampuni ambayo yamesajiliwa Tanzania kisheria; Bulyanhulu Gold Mine Limited, Pangea Minerals Limited na North Mara Gold Mine Limited ambayo yana leseni maalumu kwa kila mgodi,” inasomeka sehemu ya taarifa katika tovuti ya Acacia ambayo gazeti hili iliiona jana. Taarifa hiyo iliendelea kueleza: “Kampuni hizi zinamilikiwa na Acacia ambayo imesajiliwa nchini Uingereza ingawa umiliki huu si wa moja kwa moja (indirectly owned). “Muundo huu ni wa uwazi, upo kisheria na huwekwa wazi katika taarifa zetu za hesabu za mwaka ambazo hukaguliwa kwa mujibu wa taratibu za kimataifa.” Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kwamba utaratibu huo wa umiliki uliwekwa wazi kwa CMA wakati Acacia ikijioredhesha katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) mwaka 2011. “Muundo huu ni sehemu ya taarifa ambayo ilipitishwa na CMSA kwa ajili ya kujiorodhesha DSE. Tangu kujisajili DSE kilichobadilishwa ni jina la Acacia kutoka African Barrick Gold Plc kuwa Acacia Mining Plc,” inasema taarifa hiyo. Katika hatua nyingine, Acacia wametangaza kufanya mkutano na wanahisa wake kwa mtandao kesho kutoa ufafanuzi zaidi juu ya sakata zima. Walipofuatwa DSE kutoa maelezo ni kwa vipi kampuni ambayo haina usajili kuweza kujiorodhesha na kuuza hisa, walisema wao si wasemaji kwa kuwa mchakato wa kujiorodhesha huongozwa na kusimamiwa na CMSA na hivyo kumshauri mwandishi awasiliane nao. Mwandishi alipowasiliana na Ofisa Habari wa CMSA, Charles Shirima, alisema mtu aliyekuwa akishughulikia suala hilo alikuwa safarini Dodoma na kumtaka mwandishi awasiliane naye leo.

Friday, June 2, 2017
Kada CHADEMA ameachiwa kwa dhamana leo baada kupandiswa mahakamani.soma zaid

Kada CHADEMA ameachiwa kwa dhamana leo baada kupandiswa mahakamani.soma zaid

Dar es Salaam. Mfanyabiashara Yericko
Nyerere amepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na mashtaka matano ya kutoa
taarifa za upotoshaji kupitia mtandao wa
Facebook.
Kwa mujibu wa kesi hiyo namba 184,
2017, Wakili wa Serikali, Elia Athanas
alidai kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard
Mashauri kuwa mshtakiwa huyo alifanya
makosa hayo kinyume na kifungu cha 16
cha Sheria ya Mtandao Namba 14 ya 2015
Ameachiwa kwa dhamana baada ya
kukamilisha masharti ya kuwa na
mdhamini mmoja ambaye amesaini bondi
ya Sh 10milioni.
Kesi imeahirishwa Juni 5, 2017
kusomewa maelezo ya awali (PH)
Chanzo: Mwananchi

Back To Top