Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Wednesday, March 23, 2016
IMF yafurahishwa na utendaji wa serikali ya Magufuri.

IMF yafurahishwa na utendaji wa serikali ya Magufuri.


UJUMBE wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
umeridhishwa na juhudi zinazofanywa na Serikali
ya Rais John Magufuli katika kuongeza juhudi za
kupambana na rushwa. Hali hiyo itabadili
mtazamo wa awali kwamba utawala bora
ulishapotea nchini, kama ilivyoonekana katika
tafiti nyingi zilizofanyika.
Aidha, ujumbe huo unaunga mkono malengo ya
uchumi yaliyomo katika mwongozo wa Bajeti ya
mwaka 2016/2017 uliochapishwa, ambayo
yamezingatia uhalisia katika ukadiriaji wa
mapato.
Hayo yalielezwa katika taarifa ya shirika hilo,
iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Dar es
Salaam baada ya kumalizika kwa ziara ya
ujumbe huo ulioongozwa na Mkurugenzi Msaidizi
na Mkuu wa IMF nchini, Herve Joly. Ujumbe huo
pia ulifanya tathmini ya nne ya Mpango wa
Ushauri wa Sera za Uchumi (PSI), ulioidhinishwa
na Bodi Tendaji ya IMF mwaka huu.
Ilieleza taarifa hiyo kuwa “ujumbe umeridhishwa
na juhudi zinazofanywa na serikali katika
kuongeza juhudi zaidi za kupambana na rushwa,
hali ambayo itabadili mtizamo wa awali kwamba
utawala bora ulikwishapotea nchini kama
ilivyoonekana kwenye tafiti nyingi zilizofanyika.”
Tangu aingie madarakani Novemba mwaka jana,
Rais John Magufuli na serikali yake
imejipambanua kwa kupambana na rushwa na
ufisadi kwa kuwachukulia hatua wakwepa kodi na
watendaji wa serikali ambao ni wala rushwa,
kuwapeleka mahakamani na kuwasimamisha kazi
kupisha uchunguzi.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa mwongozo wa bajeti
ya Tanzania kwa mwaka 2016/17 umezingatia
kupunguza kwa kiasi kikubwa nakisi ya bajeti na
matumizi ya kawaida ili kutoa fursa ya kuongeza
matumizi ya maendeleo. “Changamoto kubwa
katika kukamilisha bajeti ni kuhakikisha kuwa
matumizi yanaendana na mapato halisi.
Majadiliano yataendelea katika wiki chache zijazo
ili kufikia muafaka juu ya mfumo mzima wa sera
za uchumi ambazo zitapelekwa kukamilisha
mapitio ya nne ya mpango wa PSI,” ilieleza
taarifa hiyo.
Mapitio hayo ya mpango wa PSI na majadiliano
chini ya kanuni ya nne ya mkataba ulioanzisha
IMF, yanatarajiwa kujadiliwa na Bodi Tendaji ya
IMF mwaka huu. Majadiliano chini ya mpango wa
PSI pia yamelenga kwenye utekelezaji wa bajeti
ya mwaka 2015/2016 na mipango ya bajeti ya
mwaka 2016/2017.
Katika taarifa hiyo, Joly alisema mwenendo wa
uchumi umeendelea kuimarika kwani makadirio
yanaonesha kuwa Pato la Taifa kwa mwaka jana
lilikua kwa asilimia saba, huku shughuli zilizokua
kwa kasi ni ujenzi, mawasiliano, huduma za
kifedha na uchukuzi. “Mfumuko wa bei
umeendelea kubakia kwenye kiwango cha
tarakimu moja muda wote wa mwaka 2015 na
kufikia wastani wa asilimia 5.6, japokuwa
thamani ya Shilingi ilishuka kwa kiasi kikubwa
katika nusu ya mwaka,” alisema Joly.
Alisema majadiliano na serikali chini ya kanuni ya
nne ya mkataba wa IMF yalijikita kwenye namna
ya kuendeleza ukuaji wa uchumi kwa kiwango
cha juu unaozingatia utekelezaji wa vipaumbele
vya serikali bila kusababisha athari za kiuchumi.
Hata hivyo, mabadiliko makubwa ya kimfumo
yanahitajika ili kuboresha mfumo mzima wa
kiuchumi na kuongeza tija katika uzalishaji na
uwekezaji.
“Kumekuwa na mtazamo sawa wa maoni kwenye
maeneo ya vipaumbele vya maboresho ya
kiuchumi na jinsi serikali itakavyochangia katika
kuwezesha uchumi endelevu na unaoongozwa na
sekta binafsi,” aliongeza Joly. Alisema uboreshaji
wa sekta ya kilimo inayoajiri idadi kubwa ya watu
utasaidia kuongeza kipato cha watu wa vijijini na
hiyo kuchangia kupunguza umasikini.
Aidha, utatoa fursa ya ajira kwa sekta nyingine
za uchumi na kukuza viwanda mbalimbali
ikiwemo vya kusindika vyakula. Kipaumbele
kingine ni kuboresha mazingira ya kufanya
biashara, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa
nishati na miundombinu bora ya usafirishaji na
upatikanaji wa ardhi na mitaji.
Aidha, kuendelea kuimarisha hali ya kifedha ya
Shirika la Umeme (Tanesco) na kulipa
malimbikizo ya madeni ya huduma za gesi na
umeme ni muhimu katika kuwawezesha
wawekezaji binafsi kuendelea kuwekeza kwenye
sekta ya nishati. “Tanzania inaweza kunufaika
kwa kiasi kikubwa na kukamilika kwa soko la
pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambalo
litasaidia kuvutia mitaji na kukuza ushinda na
kuongeza ufanisi,” alisema.
Wakati huo huo, mapato ya serikali kwa mwezi
huu yamefikia Sh trilioni 1.4, kwa mujibu wa
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam jana, Dk Mpango alieleza mchanganuo
wa fedha hizo kuwa ni mapato ya kodi (Mamlaka
ya Mapato Tanzania -TRA) ni Sh
1,283,274,000,000, mapato yasiyo ya kodi Sh
77,504,000,000 na mapato yatokanayo na vyanzo
vya Halmashauri Sh 43,490,000,000, kufanya
jumla ya Sh 1,404,268,000,000.
“Tunatarajia pia kupata mikopo na misaada ya
mifuko ya ‘Basket’ na miradi ya maendeleo
kutoka kwa washirika wa maendeleo shilingi
71,200,000,000,” alieleza Dk Mpango. Akieleza
mchanganuo wa matumizi, Dk Mpango alisema
yametumika katika kulipa mishahara ya
watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa,
watumishi wa Taasisi na Wakala za Serikali
pamoja na malimbikizo ya Sh 518,822,320 kwa
Taasisi na Wakala 24 na hasa sehemu kubwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili ambayo jumla ya
mishahara ni Sh 582,043,000,000.
Alitaja matumizi mengine ni kulipia posho ya
chakula kwa ajili ya vyombo vya ulinzi na
usalama, ruzuku ya vyama vya siasa, posho ya
madaktari wanafunzi 1,608, Wizara ya Afya
ununuzi wa dawa na vifaa tiba, mikopo ya
wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa semista ya tatu,
kutekeleza mpango wa Elimu bure na mapato ya
ndani kwa Halmashauri kwa ajili ya miradi na
uendeshaji wa ofisi.
Mengine ni madeni ya watumishi wasio walimu
katika Halmashauri, miradi ya umeme, Wakala wa
Umeme Vijijini, Mradi wa Umeme Kinyerezi I,
Mradi wa Kufua Umeme Makambako – Songea,
malimbikizo ya madeni ya makandarasi wa
barabara, miradi ya maji, Mfuko wa Reli, fidia
kwa wananchi kupisha mradi wa Kurasini Trade
and Logistic Hub, Mradi wa Ununuzi wa Dawa na
Vifaa Tiba (ORIO) na Mfuko wa Kuchochea
Maendeleo ya Jimbo.

Wizi wa mafuta ya ndege maafisa 3 wa polis zimamoto wasimamishwa kazi.soma zaid.

Wizi wa mafuta ya ndege maafisa 3 wa polis zimamoto wasimamishwa kazi.soma zaid.

Serikali imewasimamisha kazi Maafisa 3 wa
Jeshi la Kikosi cha Zimamoto kwa tuhuma za
kushiriki wizi wa mafuta ya Ndege na mmoja kati
yao kuiba mizigo ya wateja kwa kushirikiana na
wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport.
Akizungumza katika Ziara ya kushitukiza
aliyoifanya katika Viwanja vya Ndege vya
Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es Salaam Naibu
Waziri wa mambo ya ndani Mh.Mhandisi Hamad
Masauni amewataja walio simamishwa kazi ni
Khalfani Kisana na Mussa Mandauli ambao
walikamatwa na madumu 10 ya mafuta ya Ndege
wakiwa na gari la Serikali lenye usajiri STJ 2948
huku askari mwingine aliyejulikana kwa jina la
Abas Mwanza akishutumiwa kwa kosa la
kushirikiana na mfanyakazi wa Swissport |Lucas
Maganda kwa kosa la kuiba mzigo wa abiria.
Akiwa katika kiwanja hicho Mh.Masauni
amekagua utendaji kazi katika idara ya
Uhamiaji,Polisi na Jeshi la Zimamoto na kuagiza
viongozi wa idara hizo zilizopo chini ya Wizara
yake kufanya kazi kwa uaminifu na yeyote
atakayekiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.chanzo itv tanzania.

Ulipaji mishahara hewa kwa baadhi ya watumishi wa umma wasababisha upotevu wa fedha nyingi za serikali.soma zaid.

Ulipaji mishahara hewa kwa baadhi ya watumishi wa umma wasababisha upotevu wa fedha nyingi za serikali.soma zaid.

Serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi sio tu
kwa kuwalipa watumishi hewa,bali pia kutokana
na kulipwa bila kufanya kazi kwa watumishi wa
umma.
Mkurugenzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo
ya sekta za Umma,Emmanuel Malangalila
amesema hayo wakati akizungumza na wadau na
kuzinduliwa kwa mradi huo wa uimarishaji  jana mkoani
Morogoro,ambapo amesema kuanza kwake katika
mikoa 13 nchini kutasaidia kubaini malipo
hayo,sambamba na kuanza kulipa watumishi
kutokana na kazi walizofanya na kwa kuanzia
wataanza kwa majaribio kwa sekta ya afya katika
Mikoa ya Shinyanga na Mwanza na kusaidia
kuondoa matatizo ya upotevu wa fedha za Umma
huku Mratibu wa mradi huo Christina Malembeka
akisema wanaamini mradi huo utasaidia sekta za
Umma kwakuwa wanashirikiana na watendaji
mbalimbali ambao wao ndio watabainisha
changamoto zao na kuweza kutatuliwa.
Mshauri wa Utawala Bora na ushirikishwaji wa
wananchi Paul Chikira amesema mradi huo
unakusudia kuwafikia wananchi moja kwa moja
kwakuwa wataweza kushuhudia maendeleo yake
sambamba na uimarikaji wa sekta tofauti za
serikali ikiwemo elimu afya,kilimo na utawala
bora,huku Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Muhingo
Rweyemamu akimwakilisha Mkuu wa Mkoa
Dkt.kebwe Stephen Kebwe, akiagiza watendaji
wa Halmashauri kutekeleza kazi za Serikali za
kuhudumia wananchi kwa ufanisi na kufuata
mifumo imara iliyopo na kutoa ushirikiano kwa
mradi huo kwa kushirikisha wataalam wake.
Serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi sio tu
kwa kuwalipa watumishi hewa,bali pia kutokana
na kulipwa bila kufanya kazi kwa watumishi wa
umma.chanzo itv tanzania.

Baraki obama ampa ujasiri castro rais wa cuba kutoiogopa marekani.soma zaid.

Baraki obama ampa ujasiri castro rais wa cuba kutoiogopa marekani.soma zaid.


Rais wa Marekani Barack Obama ameeleza
matumaini yake kwamba hali ya Cuba
itaimarika, kwenye hotuba iliyopeperushwa moja
kwa moja kupitia runinga.
Kiongozi huyo wa Marekani, ambaye ndiye wa
kwanza kuzuru Cuba akiwa bado madarakani
katika kipindi cha miaka 88, alitoa hotuba hiyo
kutoka ukumbi wa Grand Theatre mjini Havana.
Bw Obama alisema alifika Cuba “kuzika masalio
ya Vita Baridi” na miongo mingi ya uhasama.
Alimwambia Rais wa Cuba Raul Castro kwamba
hafai kuiogopa Marekani na pia hafai kuogopa
“usemi wa watu wa Cuba”.
Obama na Castro wajibizana Cuba
Bw Obama alisema wakati umefika kwa Marekani
na Cuba kuacha nyuma yaliyopita na kusonga
mbele “kama marafiki na majirani na kama
familia, pamoja” kwa siku za usoni zenye ufanisi.
Amewataka raia wa Cuba kuacha nyuma vita vya
kifalsafa na kujieleza sio kwa kupinga Marekani
bali kwa kujieleza wao binafsi ama raia wa Cuba.
"Licha ya siasa hizi zote, watu ni wale wale na
Wacuba ni Wacuba,” alisema.
Aidha, amehimiza kuondolewa kwa vikwazo vya
kibiashara vilivyowekewa nchi hiyo na Marekani
miaka 54 iliyopita. Tamko hilo lilishangiliwa sana
na raia wa Cuba.
Ni Bunge la Congress pekee linaloweza
kuidhinisha kuondolewa kwa vikwazo hivyo.
Bw Obama alikamilisha ziara yake ya siku tatu
kwa kuungana na Rais Castro kutazama mechi
ya besiboli uwanja wa Latinoamericano mjini
Havana.
Tampa Bay Rays waliilaza timu ya taifa ya Cuba
4-1.
Baada ya kuondoka Cuba, Bw Obama ameelekea
Argentina siku ambayo inalingana na
maadhimisho ya miaka 40 tangu kutokea kwa
mapinduzi yaliyoingiza mamlakani utawala
dhalimu wa kijeshi.
Baadhi ya makundi yanapanga maandamano
kushutumu Marekani ambayo inadaiwa kusaidia
jeshi wakati wa mapinduzi hayo ya 1976.chanzo bbc swahil

Mamia ya watu wa mtaa wa buyombe mkoan mwanza waliandamana jana kupinga kuuzwa mlima  buyombe.soma zaid.

Mamia ya watu wa mtaa wa buyombe mkoan mwanza waliandamana jana kupinga kuuzwa mlima buyombe.soma zaid.

amia ya wakazi wa mtaa wa Buyombe Kata ya
Kahama jijini Mwanza wakiwa na silaha za
jadi,wameandamana kupinga vikali kuuzwa kwa
Mlima wao kunakodaiwa kufanywa na baadhi ya
watumishi wa idara ya ardhi na mipango miji ya
jiji hilo kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo
cha elimu ya biashara,kampasi ya Mwanza huku
baadhi yao wakionyesha hasira zao baada ya
kuanza kung’oa vigingi vyote pamoja na mabango
ya Chuo hicho.
Wakazi hao wanasema kuwa hawako tayari
kuchangia shilingi elfu hamsini kwa kila kaya kwa
ajili ya ujenzi wa shule yao ya msingi kwani zaidi
ya shilingi milioni mia sita zilizotokana na mauzo
ya mlima huo kwa chuo cha elimu ya biashara
kampasi ya Mwanza pamoja na wananchi
wengine zinatosha kabisa kugharimia
miundombinu ya huduma za kijamii kama vile
shule,zahanati,maji ya bomba na Barabara.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa
Buyombe,Emanuel Zambezi amesema madai ya
wakazi hao yana mantiki kubwa.chanzo itv.

Mkurugenzi manispaa kigoma ujiji apewa siku moja kutoa maelezo kuhusu upotevu wa sh.bilion 2.46.soma zaid.

Mkurugenzi manispaa kigoma ujiji apewa siku moja kutoa maelezo kuhusu upotevu wa sh.bilion 2.46.soma zaid.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utumishi na utawala
bora Mh.Angella Kairuki ametoa siku moja kwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na
Mkoa kutoa maelezo ya matumizi ya shilingi
bilioni 2.46 zilizotolewa na Serikali katika mwaka
wa fedha 2014/2015 kwa ajili ya kugharamia
ujenzi wa nyumba za Walimu,Vyoo na usimamizi.
Waziri Kairuki ametoa maagizo hayo jana baada ya
kamati ya Bunge ya utawala bora na Serikali za
mitaa kutembelea Shule ya Sekondari Kirugu
kata ya majengo mjini kigoma na kukagua baadhi
ya vyumba vya Madarasa vilivyojengwa na
mpango wa maendeleo ya jamii TASAF awamu
ya pili ambapo ilibainika kuwa shule hiyo haina
Nyumba za Walimu,jengo la utawala,umeme na
vyoo havitoshelezi,ambapo amesema hali hiyo
inaonyesha jinsi fedha zilizotolewa na serikali
hazikutumika kwa malengo yaliyokusudiwa katika
mkoa wa Kigoma na kutaka taarifa hiyo
iwasilishwe haraka kwa Waziri wa TAMISEMI
Mh.George Simbachawene.
Katika taarifa yake kwa kamati ya Bunge,ambayo
pia ilitembelea miradi ya barabara na kituo cha
mabasi mjini Kigoma zilizojengwa kwa msaada
wa Benki ya Dunia,Afisa mtendaji wa mtaa wa
Katonyanga kata ya Majengo Kilinako Iddi
amesema baada ya TASAF kujenga madarasa
shule imebakiwa na changamoto za umeme,
maji,nyumba za walimu,jengo la utawala na vyoo
huku Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya utawala
bora na serikali za mitaa Mh.Jasson Rweikiza
akiiomba TASAF kusaidia miundombinu ya maji
katika shule hiyo.chanzo itv.

Hizi ni baadhi ya sentesi chache alizoziongea wazir wa Afya ummy nwalimu kuhusu huduma ya Afya ya wazee na watoto.soma zaidi

Hizi ni baadhi ya sentesi chache alizoziongea wazir wa Afya ummy nwalimu kuhusu huduma ya Afya ya wazee na watoto.soma zaidi

March 23 2016 Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekutana na
Baraza la Wazee wa Dar es salaam na kusikiliza
changamoto zinazowakabili katika jamii.
Katika kutatua changamoto zinazowakabili
wazee, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto imeonyesha
imedhamiria kutoa kipaumbele kwa wazee na
imesisitiza kusimamia Sera ya Serikali ya kutoa
huduma za afya bure kwa wazee. Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu amezungumza na
waandishi wa habari na kusema….
>>’kuhusu huduma kwa wazee hasa matibabu
tunataka kuwathibishia bado inabaki kuwa ni sera
ya Serikali na kwamba wazee Tanzania wanatakiwa
kupata matibabu bure, kuanzia gharama ya
kumuona Daktari, vipimo na Dawa. Naendelea
kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha
wanatekeleza Sera ya Serikali ya kutoa huduma za
afya bure ikiwemo kuanzisha dirisha la wazee‘.
>>>’ na kuonyesha kwamba nimedhamiria
nimeshaongea na watu wa bima ya afya mwezi
ujao tutatoa matangazo ambayo tutaweka katika
vituo vyote vya Serikali ‘Mzee kwanza, Mzee
alikuwa kama wewe na wewe utakuwa kama yeye,
tafadhali toa kipaumbele cha huduma kwa wazee’
tayari tumeshaaanza tunatafuta siku ya kuyazindua
ili kuendelea kuhamasisha kipaumbele kwa wazee‘.

Back To Top