Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Friday, April 22, 2016
Donard Trump asalimu amri ahidi kubadilika.soma zaid.

Donard Trump asalimu amri ahidi kubadilika.soma zaid.

Mgombea wa urais nchini Marekani kwa tiketi ya
chama cha Republican Donald Trump ameahidi
kubadilisha sifa zake katika mkutano wa faragha
na viongozi wa Republican.
Mfanyibishara huyo ambaye yuko kifua mbele
katika kuwania urais kupitia chama hicho alitoa
ujumbe wake kupitia wasaidizi wake ,kulingana
na chombo cha habari cha AP.
Kuimarika kwake katika mchujo huo kufikia sasa
kumekuwa na ishara miongoni mwa viongozi wa
chama hicho kwamba matamshi pamoja na sera
zake huenda zisiwavutie wapiga kura.
Majimbo matano yanapiga kura siku ya Jumanne
kumchagua mgombea wao wa urais.
Bwana Trump ana uongozi mkubwa wa idadi ya
wajumbe lakini huenda asipate wajumbe 1,237
anaohitaji kushinda mchujo huo bila ya mkutano
wa wanachama.
Wasaidizi wamewaambia viongozi wa chama
kwamba amekuwa akibadilisha sifa zake na
kwamba hatua hiyo imeanza kufua dafu.chanzo bbc swahil.

Siku zote mapenzi sio bifu la kudumu.hiki ndicho alichokifanya ney wa mitego.soma zaid.

Siku zote mapenzi sio bifu la kudumu.hiki ndicho alichokifanya ney wa mitego.soma zaid.

Mahakama ya wilaya ya Nyamagana,Mkoani
Mwanza jana ilimhukumu miaka miwili jela mzazi
mwenzie na msanii Nay Wa Mitego, Siwema
Edson kwa makosa ya kimtandao,msanii huyo
anafikiria kuahirihisha shoo yake kwa mwisho wa
mwezi huu ili aende Mwanza kumsaidia mama
watoto wake huyo.
‘’Inabidi niondoke hivi karibuni ilibidi nisubiri
nimalize shoo lakini kwa ajili ya kumpambania
kwa ajili ya kwenda kujua ‘situation’ ya kule ikoje
na pia wapi pa kuanzia,mwisho wa mwezi huu
nina shoo mjini Sumbawanga lakini inabidi niende
kwanza Mwanza nikafight suala la huyu bibie
halafu nijue inakuwaje kama nita’cancel’ shoo au
itakuwaje lakini hadi sasa hivi nawasiliana na
ndugu zake kila mtu amekuwa kama amepagawa
hivi hakuna anayejua wapi kwa kuanzia unajua
kimekuwa ni kitu ambacho hakuna mtu aliyekuwa
anategemea’’Alisema Nay Wa Mitego.
chanzo clouds.

Kutoka bungeni# waziri mkuu elimu ni nguzo mhimu katika maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla.soma zaid.

Kutoka bungeni# waziri mkuu elimu ni nguzo mhimu katika maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla.soma zaid.

Bunge la 11 limeendelea tena leo April 22 2016,
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amehutubia bunge
kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali
na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za
ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2016/2017.
Katika kitengo cha huduma ya Jamii Elimu,
Waziri Majaliwa amesema ‘ Kwa kutambua
umuhimu wa Elimu kama nyenzo imara ya
maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Serikali imeanza
kuboresha na kuimarisha elimu ya awali, msingi,
sekondari, ufundi na elimu ya juu.’
‘ Baada ya kuanza utekelezaji wa mpango wa elimu
bila malipo, kumejitokeza changamoto kadhaa,
ikiwemo miundombinu kama madarasa, mabweni,
maabara, nyumba za walimu na vyoo ‘ ;-Waziri
Mkuu Majaliwa
‘ Napenda kuwahakikishia wananchi kwamba
Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto
hizo na jitihada kubwa zimewekwa‘ ;-Waziri Mkuu
Majaliwa
‘ Nitumie nafasi hii kuwashukuru wadau walioanza
kuchangia madawati katika maeneo mbalimbali,na
niwasihi wengine waendelee kuunga mkono Serikali
yao ‘ ;- Waziri Mkuu Majaliwa
‘ Kuanzia leo hii, nawaagiza Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wote waliokamata mbao ndani ya
Halmashauri zao kuzitumia kutengeneza madawati
na siyo kuzipiga mnada ‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa
‘ Hali ya urejeshaji wa mikopo iliyotolewa
hairidhishi, Hivyo naagiza Bodi ya mikopo ya Elimu
ya Juu kufuatilia urejeshaji wa mikopo hiyo ili
fedha hizo zitumike kuwakopesha wanafunzi
wengine‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa

Mauaji ya kikatiri yatokea wilaya ya geita muuguzi wa zahanati  akwakatwa mapanga.soma zaid.

Mauaji ya kikatiri yatokea wilaya ya geita muuguzi wa zahanati akwakatwa mapanga.soma zaid.

Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo, mkuu wa
wilaya ya Geita Manzie Mangochie mauaji hayo
yametokea jana usiku baada ya wanaume watatu
kufika nyumbani kwa marehemu wakidai wana
mgonjwa na Misango alipotoka kuwasikiliza shida
yao, ndipo walipomvamia na kwa kutumia panga
nas kusababisha kifo cha muuguzi huyo.
By Rehema Matowo, Mwananchi Digital
Geita. Muuguzi wa zahanati ya Kagu wilaya ya
Geita mkoani hapa, Elizabeth Misango (54)
ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu
wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.
Japokuwa Jeshi la polisi linaendelea na
uchunguzi wa tukio hilo la kikatili mkoani hapa,
mashuhuda wanahusisha mauaji hayo na imani
za kishirikina.
Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo, mkuu wa
wilaya ya Geita Manzie Mangochie mauaji hayo
yametokea jana usiku baada ya wanaume watatu
kufika nyumbani kwa marehemu wakidai wana
mgonjwa na Misango alipotoka kuwasikiliza shida
yao, ndipo walipomvamia na kwa kutumia panga
nas kusababisha kifo cha muuguzi huyo.chanzo mwananch.

Sakata la lugumi ineterprises vigogo wahaha.soma zaid.

Sakata la lugumi ineterprises vigogo wahaha.soma zaid.

*Milioni 500/- hazijulikani zilizopo, zabuni yake
ilitangazwa siku moja
*Taarifa ya polisi, CAG zatofautiana, kamati
yaahidi kumuona Spika
DODOMA
WAKATI sakata la ufisadi wa mkataba kati ya
Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd na Jeshi la
Polisi likiendelea kufukuta, imebainika Sh milioni
500 zilichotwa bila maelezo yoyote.
Habari za uhakika zilizopatikana mjini hapa jana,
zinasema upotevu huo umebainika baada ya
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CGA), kufanya ukaguzi wa taarifa za mapato na
matumizi ndani ya Jeshi la Polisi.
Taarifa hizo ziliwasilishwa juzi na Ofisa Masuhuli
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu
Inspekta Generali wa Polisi (D/IGP),
Abdulrahman Kaniki.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka
ndani ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC), vigogo hao walishindwa kutoa maelezo ya
kina kuhusu tofauti hiyo ya fedha, mbele ya
wajumbe wa kamati hiyo.
Chanzo hicho kiliiambia MTANZANIA mjini hapa
jana, kuwa wajumbe wote walitilia shaka
mkataba kati ya polisi na Kampuni ya Lugumi
ambao zabuni yake ilitangazwa kwa siku moja na
kesho yake ukasainiwa.
YALIYOBAINIKA
Chanzo chetu kinasema katika kikao na vigogo
hao, wajumbe wa PAC walihoji taarifa ya
utekelezaji wa mkataba huo na kuonyesha hofu
ya kuwapo ‘wingu la ufisadi’ ambalo linahitaji
majibu.
“Zabuni ilitangazwa Septemba 22, mwaka 2011
na mkataba kusainiwa Septemba 23, mwaka huo
huo, ndani ya siku moja mkataba ukasainiwa
jambo ambalo ni hatari.
“Jambo jingine linaloshtua, tangu wakati huo
mashine zote wanasema zipo, lakini hazifanyi
kazi na swali ambalo wajumbe wanahoji,
inakuwaje wanatoa zabuni bila kufanya ‘visibility
study’ ya kina ili kujua uwezo wa hii Kampuni ya
Lugumi kama ilishawahi kufanya kazi ya aina hii
ama la.
“Tumejipanga kwa kila hatua, tumemtaka
Makamu Mwenyekiti wetu Aeshi Hilaly,
awasilishe taarifa nzima kwa Spika wa Bunge,
Job Ndugai na mwishowe taarifa hii iwasilishwe
mbele ya Bunge ili umma ujue namna watu
wanavyotafuta fedha kinyume cha sheria,”
kilisema chanzo chetu.
Mbali na hilo, pia kamati imebaini tofauti ya
fedha zilizopo katika mkataba huo ambapo taarifa
ya Jeshi la Polisi inaonyesha walitoa Sh bilioni
37,163,940,127.7, wakati taarifa ya CAG,
inaonyesha zilizotolewa ni Sh bilioni
37,742,913,007, ikiwa na tofauti ya zaidi ya Sh
milioni 500.
“Katibu Mkuu na wenzake, walipotakiwa kutoa
maelezo ya kina kuhusu zilipo Sh milioni 500
walishindwa, wajumbe wakageuka mbogo na
kutaka suala hilo litolewe maelezo ya kina.
“Licha ya hali hii, PAC tulibaki tukijiuliza, hata
kama kulikuwa na ulazima wa kufunga mashine
hizi kwa dharura inakuwaje hazifanyi kazi?
Maana kuna kila dalili ya fedha za umma kuliwa
mchana kweupe,” kilisema chanzo chetu.
Pia kamati hiyo ilibani mkataba ulitolewa kwa
‘single source’ (yaani kampuni moja bila
kuishindanisha na nyingine), badala ya tenda
kushindaniwa na kampuni nyingi zaidi.
VIGOGO WAHAHA
Baada ya PAC kuendelea na kazi ya kuchambua
taarifa hiyo, kigogo mmoja ambaye anatajwa
kuhusika katika mkataba huo, amekuwa akihaha
kuomba nguvu ya wabunge wa Kambi ya
Upinzani, hasa wale wanaotokana na vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) ili wamnusuru.
“Ninamshangaa huyo waziri (jina linahifadhiwa),
anahangaika bure, eti anasema watu
hawampendi na wanamchukia, amefikia hatua ya
kusema PAC inatumiwa na wauza dawa za
kulevya.
“Sisi ni wajumbe ambao kila mmoja anajiweza,
hata siku moja hatuwezi kukaa kutegemea fedha
za watu, ila tunafanya kazi kwa masilahi ya nchi
yetu na si vinginevyo. Tumeridhika na posho
tunazolipwa na Bunge, hatuna haja ya kutumika
kwa mtu yeyote ila tunasukumwa na uzalendo
kwa Taifa letu,” kilisema chanzo chetu.
Katika kile kinachoonekana ni kama maigizo,
baada ya PAC kutaka mkataba na taarifa ya
utekelezaji wa mradi huo wa ufungaji wa
mashine za utambuzi wa alama za vidole katika
vituo vya polisi 108 nchini, sakata hilo limekuwa
likichukua sura mpya kila kukicha.
Uamuzi huo uliibua hisia miongoni mwa jamii
ambapo katika kipindi cha siku mbili baada ya
PAC kutaka ripoti hiyo, Kamati ya Bunge ya
Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, iliingilia kati
ambapo mwenyekiti wake, Balozi Adadi Rajabu,
alikiri kupokea mkataba huo.
UTATA
Kampuni ya Lugumi inadaiwa kupewa tenda na
jeshi hilo kwa ajili ya kufunga mashine za
kuchukua alama za vidole – ‘Biometric Access’
katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh
bilioni 37.
Hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo
14 pekee na tayari kampuni hiyo imelipwa Sh
bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya
fedha zote za mkataba.
Katika sakata hilo, inadaiwa Kampuni ya Lugumi
ilipewa zabuni hiyo ikiwa haina uzoefu wa kazi
hiyo.
“Wamepewa mkataba sawa, lakini mbona taarifa
zinaonyesha kuwa kampuni hii haijasajiliwa kama
Biometric Access Company na haijawahi kufanya
kazi zozote zinazohusu Biometric Access
Control?” alihoji mmoja wa wataalamu.
Chamxo mtanzania

Thursday, April 21, 2016
Askofu gwajima aibuka na kusema haya.soma zaid.

Askofu gwajima aibuka na kusema haya.soma zaid.


Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Josephat Gwajima, amesema mafisadi
walioinyonya nchi katika Serikali ya awamu ya
nne, ndiyo wanaoona utawala wa Rais Magufuli
haufai.
“Wasikukatishe tamaa endelea hivyo hivyo kuna
wanyonyaji walipenyeza mirija yao katika serikali
iliyopita wakati wao umefika, sasa
wanatapatapa.”

Vitendo vya uchomaji moto makanisa vitaisha lini? hili limetokea mkoani kagera.soma zaid.

Vitendo vya uchomaji moto makanisa vitaisha lini? hili limetokea mkoani kagera.soma zaid.

Ni kanisa la Pentecostal linaitwa
Cornerstone Assemblies of God Tanzania
liko kijiji cha Kihanga, kata ya Kihanga
wilaya ya Karagwe, Kagera. Kanisa
lilichomwa moto na watu wasiojulikana
usiku wa kuamkia alhamisi ya tar
14 .4.2016
Wiki moja kabla pia wahalifu hao
walitumia ufunguo bandia na kuingia
ndani na kuchoma vitambaa vya
madhabahu na vitabu vya dini kanisani.
Matukio yote mawili yaliripotiwa polisi.chanzo jamii forums.

Back To Top