Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Monday, October 10, 2016
Stephen Wasira ameendelea kupinga ushindi wa Ester Bulaya mahakamani.soma zaid

Stephen Wasira ameendelea kupinga ushindi wa Ester Bulaya mahakamani.soma zaid

Shahidi wa tatu katika kesi namba moja ya
mwaka 2015 ya kupinga matokeo ya ubunge wa
jimbo la Bunda Mjini, Stephen Wasira leo
amepanda katika kizimba cha mahakama kuu
kanda ya Mwanza, inayoketi mjini Musoma kutoa
utetezi wake, huku ulinzi mkali wa askari polisi
wenye silaha za moto, mabomu ya machozi na
mbwa ukiwa umeimarishwa.
Wasira ambaye alitumia muda wa saa 2 na
dakika 26 kutoa ushahidi wake huku akihojiwa na
wakili wa mlalamikiwa wa kwanza Ester Bulaya,
ameiambia mahakama kuu chini ya jaji Noel
Chocha kwamba uchaguzi katika jimbo la Bunda
mjini ulikuwa haramu kutokana na kugubikwa na
ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni
kulikofanywa na msimamizi wa uchaguzi kufuatia
kuwepo kwa ongezeko la vituo vya kupigia kura
kutoka 190 hadi 199, sambamba na ongezeko la
idadi ya wapiga kura kutoka watu 69,369 hadi
164, 794 bila taarifa yoyote.
Mwanasiasa huyo mkongwe, ambaye aliangushwa
na mgombea wa chama cha demokrasia na
maendeleo ( CHADEMA ), katika uchaguzi mkuu
uliopita kwa kura 19,000 dhidi ya 28,568
alizopata mshindi Ester Bulaya, amemlalamikia
msimamizi wa uchaguzi jimbo la Bunda mjini
kuongeza vituo 9 kwenye kata za kabasa, Bunda
mjini, Bunda stoo, Manyamanyama,
Nyamakokoto, Wariku na Guta pamoja na
kuhamisha kituo cha Mchalo na kukipeleka
mahali kusikojulikana bila kuvishirikisha vyama
vitano vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi huo.
Mapema wakili Tundu Lissu, baada ya kupitia
kiapo cha shahidi huyo Stephen Wasira aliiomba
mahakama hiyo kuondoa aya ya 3b, kirumi i (ii),
( iii ) na ( iv ) pamoja na 3c, ambazo
zingewezakuleta mambo mapya katika shauri hilo
kinyume na masharti ya 23 ya kanuni za
uendeshaji wa uchaguzi za mwaka 2013 kama
zilivyofanyiwa marekebisho, hoja ambayo
ilikubaliwa na jaji Noel Chocha.
Mara kwa mara jaji chocha alilazimika kuingilia
kati kwa kumtaka wasira kujibu maswali ya wakili
Tundu Lissu, huku Wasira akionekana dhahiri
kuwa na majibu ya kujiamini; ambayo wakati
mwingine yaliwafanya wasikilizaji kuangua
kicheko hasa pale alipodai kuwa hamfahamu
katibu mkuu wa Chadema Dk. Vincent Mashinji
zaidi ya Dk. Wilbroad Slaa, ili kujiridhisha iwapo
Ester Bulaya aliwahi kujaza fomu ya bajeti za
gharama za uchaguzi ambayo kisheria hupelekwa
kwa msajili wa vyama vya siasa mwenye uwezo
wa kumwekea pingamizi mgombea aliyekiuka
utaratibu.
Kipindi cha mchana kilianza kwa mawakili
Costantine Mutalemwa, Yasin Memba na Hajra
Mungula wanaowatetea wapiga kura wanne wa
jimbo la Bunda mjini waliofungua kesi hiyo
mahakama kuu kanda ya Mwanza kumhoji shahidi
huyo wa tatu Stephen Wasira baada ya wakili
Tundu Lissu kuhitimisha maswali yake.

Taarifa kwa umma ya mh.Ummy Mwalimu waziri wa Afya Maendeleo Jinsia,Wazee na Watoto kuhusu hali ya upatikanaji wa Dawa Nchini.soma zaid

Taarifa kwa umma ya mh.Ummy Mwalimu waziri wa Afya Maendeleo Jinsia,Wazee na Watoto kuhusu hali ya upatikanaji wa Dawa Nchini.soma zaid

TAARIFA KWA UMMA YA MHE. UMMY
MWALIMU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA
JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.
KUHUSU HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA
NCHINI NA UFAFANUZI WA MASUALA KADHAA
YALIYOTOLEWA NA BAADHI YA TAASISI ZA
KIJAMII ZINAZOFATILIA MASUALA YA AFYA.
TAREHE 10/10/2016
Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa katika
baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari vya
ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na
mitandao ya kijamii vikizungumzia hali ya dawa
nchini hasa kufuatia taarifa zilizotolewa na
taasisi ya kiraia na baadhi ya viongozi wa
vyama vya siasa.
Taarifa hizo zilidai kwamba katika kipindi hiki
kuna upungufu mkubwa wa dawa katika bohari
kuu ya dawa , Hivyo, kusababisha kukosekana
kwa dawa katika vituo vya kutolea huduma za
Afya.
Taarifa hizi si sahihi na zinalenga kupotosha
umma na kuwatia wananchi wasiwasi. Napenda
kuwathibitishia wananchi kuwa Afya ni suala la
kipaumbele kwa Serikali ya Awamu ya Tano.
Hivyo, ningependa kutoa ufafanuzi kwa wananchi
katika masuala yafuatayo; –
Hali ya Upatikanaji wa dawa
Hali ya upatikanaji wa dawa kwa sasa iko vizuri.
Dawa muhimu zinazohitajika sana nchini
zinapatikana kwenye maghala ya Bohari ya
Dawa (MSD). Mfano kwa upande wa dawa za
antibiotics tuna Amoxycillin, Ciprofloxacin,
Cotrimoxazole na Doxycycline. Kwa upande wa
dawa za maumivu – tunazo za kutosha kama
vile paracetamol, asprin na diclofenac.
Pia tuna dawa za kutosha za malaria, Kifua
Kikuu, ukoma na dawa za kufubaza makali ya
UKIMWI (ARVs). Kwa upande wa chanjo za
watoto na wajawazito, ni kweli kulikuwa na
uhaba nchini kwa kipindi cha miezi miwili
iliyopita. Hata hivyo, wiki iliyopita Serikali
imenunua na kupokea dozi milioni 2 za chanjo
ya Kifua Kikuu (BCG), dozi milioni 1.2 za Polio
na dozi milioni za Polio. Chanjo hizi
zinasambazwa katika vituo vya afya nchini.
Dawa nyingine zitaendelea kupatikana katika
Bohari kuu ya Dawa kwa kuwa tumeagiza dawa
za kutosha kutoka kwa wazalishaji wa ndani na
nje ya nchi. Aidha, kiasi kikubwa cha dawa
zinazowasili Bohari kuu ya Dawa zikifika
zinapelekwa kwenye Kanda nane za MSD pamoja
na vituo viwili vya Mauzo kwa ajili ya
kuwasambazia wateja walioagiza. Hivyo, kipimo
cha upatikanaji wa dawa si kuangalia katika
maghala ya Bohari ya Dawa peke yake bali pia
katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Ili kuondoa mlolongo wa manunuzi ya dawa,
tunapenda kuwataarifu kuwa Bohari kuu ya Dawa
imepanua wigo wa upatikanaji wa dawa kwa
sasa kwa kutumia mikataba ya muda mrefu
(miaka miwili) na washitiri wa ziada wa ndani
(Prime Vendors) ili kuhakikisha dawa
zinapokosekana MSD zinapatikana kwa haraka
kwa Washitiri wa ndani waliothibitishwa katika
kila mkoa.
Katika muktadha huo huo, Bohari ya Dawa
imefungua maduka ya ziada kwa ajili ya
kuongeza upatikanaji wa dawa zaidi ya aina 600
kupitia mfumo wa maduka katika mahospitali
kama vile Muhimbili, Mbeya na Arusha.
Bajeti ya dharura kwa ajili ya dawa
Ni muhimu wananchi wakajua kuwa fedha
zilizotengwa kwa ajili ya manunuzi ya dawa
katika mwaka wa fedha 2016/17 zinatosha
kuhudumia mahitaji ya dawa kwa mwaka mzima.
Hivyo hakuna sababu ya kuwa na bajeti ya
dharura.
Niwakumbushe bajeti zilizotengwa kwa ajili ya
kununulia dawa na vifaa tiba katika miaka
michache iliyopita mpaka hivi sasa, kama
ifuatavyo: -.
Mwaka 2011/2012 bajeti iliyotengwa ilikuwa
shilingi Bilioni 23.7
Mwaka 2012/2013 bajeti ilikuwa shilingi Bilioni
34
Mwaka 2013/2014 ilikuwa shilingi Bilioni 34
Mwaka 2014/2015 ilikuwa shilingi Bilioni 60
Mwaka 2015/2016 ni shilingi Bilioni 30
Na mwaka huu 2016/17 ni shilingi Bilioni 251.5
Mkakati wa Wizara kwa sasa ni kuhakikisha
kuwa fedha hizo zinapatikana kwa wakati kutoka
Hazina kulingana na makusanyo ya nchi.Vilevile
ieleweke kwamba tayari serikali imeshatoa kiasi
cha shilingi bilioni 20 katika kipindi cha robo ya
kwanza ya mwaka wa fedha 2016/17, kwenda
Bohari kuu ya Dawa kwa ajili ya ununuzi wa
dawa na chanjo. Hali hii inathibitisha kuwa
suala la upatikanaji wa dawa ni la kipaumbele
kwa Serikali ya Awamu ya tano.
Kulipa Deni la Bohari ya Dawa (MSD)
Napenda kuwafahamisha kuwa Serikali
imedhamiria kulipa deni lote la Bohari ya Dawa
(MSD) ambapo katika mwaka huu wa fedha
2016/17 tayari Bilioni 85 imekwishatenga kwa
ajili ya kulipa deni hilo. Jambo ambalo
halijawahi kutokea huko nyuma. Kulipwa kwa
deni hilo kutasaidia kuhuisha mtaji wa MSD
(revolving fund) na hivyo kuiwezesha MSD kuwa
na dawa na vifaa tiba kwa kiwango kikubwa.
Aidha serikali imekwisha kuviagiza vituo vyote
vinavyotoa huduma za Afya kupitia Halmashauri
zao, kuhakikisha zinakuwa na fedha ya
mzunguko kwa ajili ya kununulia dawa (revolving
fund) na hivyo kupata dawa kwa kulipa fedha
taslimu kutoka Bohari ya Dawa badala ya
kukopa.
Fedha hizo zitapatika kutoka kwenye vyanzo
vyao vingine vya mapato kama vile Bima ya
Afya (NHIF, CHF) na gharama wanazochangia
wananchi katika kupata huduma. Hii itawezesha
kutoendelea kukuza deni kutoka Bohari ya Dawa
na kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wakati
wote.
MSD Kupata Mshindani
Katika mwaka 2015, Serikali ilimpa kazi mshauri
mwelekezi wa kampuni ya ushauri iliyobobea
kimataifa ya Deloitte ya kulitazama jambo hili
kwa ajili ya kuifanyia tathmini MSD pamoja na
mambo mengine ikiwemo kuangalia suala ya
kutafutiwa mshindani katika manunuzi na
usambazaji wa dawa.
Napenda kuwajulisha kuwa tathmini hiyo
ilionyesha kuwa MSD kutafutiwa mshindani
itakuwa ni kuongeza gharama kubwa kwa
serikali kutokana na kurudufisha (duplication)
majukumu. Pia ilibainika kuwa suala la dawa ni
muhimu, hivyo Serikali haiwezi kuliacha kwenye
mikono ya watu binafsi.Jambo ambalo
lilipendekezwa ni kuifanyia maboresha makubwa
MSD ili iweze kutekeleza majukumu yake
ipasavyo. Utekelezaji wa mapendekezo hayo
tayari umeshaanza.
Nchi ambazo zinaiuzia dawa na vifaa tiba MSD
MSD inaagiza dawa na vifaa tiba nje ya nchi
zaidi ya asilimia 80 kwa sababu viwanda
vilivyoko ndani ya nchi havikidhi mahitaji ya
nchi kwa ubora na kiasi. Hivyo, MSD hununua
dawa na vifaa tiba kutoka nchi za India, China,
Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Ujerumani,
Marekani, Ufaransa na sehemu nyingine duniani.
Kwa mfano, tuna dawa zaidi ya aina nne ambazo
zinanunuliwa kutoka Kenya (Dawa ya kutibu
malaria kwa akina mama wajawazito ijulikanayo
kama Sulfadoxine Pyrimethamine (SP), dawa ya
kutibu magonjwa ya maambukizi ya
Cotrimoxazole ya watu wazima na watoto
pamoja, Amoxicilline na Paracetamol ya maji
kwa ajili ya watoto.
Ikumbukwe kuwa MSD hununua dawa hizi
kupitia mchakato wa zabuni, ikiwa baadhi ya
vigezo ni kuangalia usajili wa dawa nchini
pamoja na ushindani wa bei. Hata hivyo, ili
kukuza viwanda vya ndani, watengenezaji wa
dawa wa ndani hupewa hadi 15% ya upendeleo
katika mchakato wa tathmini ya zabuni dhidi ya
dawa zinazotoka nje ya nchi (Domestic
preference).
Kwa upande mwingine mkakati wa serikali sio
kuendelea kutegemea dawa kutoka nje ya nchi,
kwani kwa kufanya hivi uchumi wa nchi
hautakuwa. hivyo basi serikali iko katika hatua
za mwisho za utaratibu wa kuwakaribisha
wawekezaji wa viwanda vya kuzalisha dawa
kuwekeza nchini kwa mpango wa kuwashirikisha
wadau wengine katika masuala ya dawa (PPP).
Hitimisho
Wizara ya afya inapenda kuwahakikishia
wananchi kuwa itasimammia ipasavyo
utapatinaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba nchini
kwa wakati na kwa bei nafuu kwa kuwa Sera ya
afya inawataka wananchi kuchangia huduma.
Aidha vituo vya kutolea huduma za Afya
vinahimizwa kupeleka mahitaji na maoteo yao ya
dawa kwa wakati badala ya kusubiri hadi dawa
zote muhimu zimeisha kabisa katika vituo vyao.
Pia wanakumbusha kulipa madeni wanayodai na
bohari ya dawa sambamba na kuhakikisha fedha
inayopatikana katika shughuli za utoaji huduma
inatumika kwa ajili ya dawa, vifaa na vifaa tiba.
Ili kuondoa vikwazo kwa wananchi katika kupata
dawa na huduma za afya kwa ujumla wananchi
wanahimizwa kujiunga na mifuko ya Bima ya
Afya kwani hakuna anayejua leo hama kesho
ataugua na Magonjwa hayapigi hodi na wakati
mwingine yanakukuta hauna
akiba ya fedha, ila ukiwa na bima wakati
wowote unapata matibabu.
Mwisho, Wizara itaendelea kuhakikisha kuwa
kuna dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya
maabara vya kutosha kwenye vituo vya umma
vya kutolea huduma za Afya nchini

Watu 14 wameuwawa baada ya bomu kulipuka Afughanistani.soma zaid

Watu 14 wameuwawa baada ya bomu kulipuka Afughanistani.soma zaid

A suicide car bombing has killed 14 people,
including 10 Afghan police officers, as the
Taliban announced it had launched a large-scale
attack on the capital of southern Helmand
province.
The armed group has expanded its footprint
across most of the province in recent months
and has been at the gates of Lashkar Gah city,
the provincial capital, for weeks.
According to police official Haji Marjan, the
vehicle explosion happened at about 11:30am
after the Taliban earlier targeted police
checkpoints across the city.
Marjan said at least 10 police officers, including
his brother, and four civilians died in the attack
in the Mukhtar area of Lashkar Gah. He warned
the death toll was likely to rise as it was unclear
how many people remain unaccounted for after
the blast.
'Fifteen wounded'
A doctor at the international emergency hospital
in Lashkar Gah said 14 bodies had been brought
to the clinic.
Speaking on condition of anonymity - as he was
not authorised to speak to the media - the
physician said 15 wounded were also brought in,
including 14 who were victims of the car
bombing and one person who suffered gunshot
wounds.
Play Video
Inside Story - Targeting the Taliban
In the Afghan capital of Kabul, Sediq Sediqqi, the
Interior Ministry spokesman, confirmed the
Taliban launched a large-scale attack on security
checkpoints in Lashkar Gah on Monday.
But he expressed confidence that the Afghan
security forces "will soon push them back".
Abdul Majeed Akhonzada, deputy director of
Helmand's provincial council, said the fighters
entered the city after breaching the Afghan
forces' "defence security belt".
Taliban spokesman Zabihullah Mujahid said the
fighters were advancing through Lashkar Gah.
Helmand is strategically important for the
Taliban as it is the main source of the country's
opium output, worth an estimated $4bn a year,
much of which funds the war.
Provincial officials have said the Taliban now
control 85 percent of the province, while only a
year ago the government controlled 80 percent.
Source: AP

Sunday, October 9, 2016
Mwalimu akutwa ameuwawa nyumbani kwake mkoani Dodoma soma zaid

Mwalimu akutwa ameuwawa nyumbani kwake mkoani Dodoma soma zaid

MWALIMU Israel Mlowasa (40) wa Shule ya
Sekondari Nkuhungu katika Manispaa ya
Dodoma, amekutwa ameuawa nyumbani kwake
na kiganja chake cha mkono wa kulia kukatwa
na kuondoka na wauaji hao.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi inasema
kwamba mauaji hayo yamefanyika juzi maeneo
ya Chang’ombe Extension katika Manispaa ya
Dodoma.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nkuhungu,
Fidelis Kaishozi alisema mwalimu huyo alipotea
tangu Oktoba 2, mwaka huu na taarifa kutolewa
Polisi.
Imeelezwa kuwa maiti ya mwalimu huyo
ilikutwa katika pagala la nyumba eneo la
Nkuhungu.
Hakuna mtu aliyekamatwa kuhusu mauaji hayo,
msako mkali unaendelea ili kubaini wahusika na
mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya
Rufaa Dodoma kwa uchunguzi zaidi wa
madaktari.chanzo muungwana blog

Marekani imeionya Saudi Arabia dhidi ya shambulio la angani.soma zaid

Marekani imeionya Saudi Arabia dhidi ya shambulio la angani.soma zaid


Marekani imeionya Saudi Arabia dhidi ya
shambulio la angani lililolenga sherehe za
mazishi nchini Yemen na kuwaua zaidi ya watu
140 na wengine wengi kujeruhiwa.
Imesema kuwa, mashambulio ya angani,
yalioongozwa na majeshi ya muungano chini ya
Saudi Arabia katika mazishi hayo.
Mfanyakazi wa shirika la Umoja wa mataifa
nchini Yemen, Jamie McGold-rick, amesema
kuwa wafanyikazi wa utoaji misaada,
wameshtushwa sana na shambulio hilo,
lililofanyika katika mji mkuu Sanaa.
Waombolezaji walikuwa wakitoa heshima zao za
mwisho, kufuatia kifo cha babake kinara maarufu
wa waasi.
Marekani imesema kuwa, inatathmini kupunguza
uungaji wake mkono wa majeshi hayo ya
muungano yanayoongozwa na Saudi Arabia.
Saudi Arabia, imekanusha kuwa ndege zake
zilishambulia mkutano huo wa mazishi.

Rais magufuli amthibitisha kilaba kuwa mkurugenzi mkuu TCRA.sima zaid

Rais magufuli amthibitisha kilaba kuwa mkurugenzi mkuu TCRA.sima zaid

Rais John Magufuli amemteua Mhandisi James
Mitayakingi Kilaba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi
amesema kuwa uteuzi huo ulianza jana
Jumamosi Oktoba 8, 2016.
Mhandisi Kilaba alikuwa akikaimu nafasi hiyo,
baada ya uteuzi wa aliyekuwa mkurugenzi mkuu
wa Dk Ally Simba kutenguliwa.

Aliyetaka mwamunyange apindue nchi ashinda kesi.soma zaid

Aliyetaka mwamunyange apindue nchi ashinda kesi.soma zaid


MWANAFUNZI wa mwaka wa tatu wa Chuo cha
Maendeleo ya Jamii (CDTI) cha mkoani Arusha,
Allan Mbando, ameibwaga Serikali katika kesi ya
kudaiwa kusambaza ujumbe kupitia Mtandao wa
Facebook akimtaka Mwamunyange apindue nchi.
Katika mtandao huo wa kijamii, Mbando,
anadaiwa kutuma ujumbe uliosomeka kwamba:
“Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote
wawe nje, halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya
kukalia kile kiti.”
Kutokana na madai hayo, Jeshi la Polisi mkoani
hapa lilimfungulia mashtaka Mbando ya kudaiwa
kusambaza ujumbe huo uliokusudia kueneza na
kufanya uchochezi.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo mjini hapa juzi,
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Augustine
Rwizile, alisema mahakama hiyo imepitia kwa
kina hoja na ushahidi wa pande zote mbili katika
kesi hiyo.
Hakimu Rwizile alisema baada ya kupitia ushahidi
katika kesi hiyo, mahakama imejiridhisha kuwa
upande wa Jamhuri katika kesi hiyo haukuweza
kuwasilisha ushahidi unaoweza kumtia hatiani
mshtakiwa.
Alisema mbali na ushahidi huo kutojitosheleza,
pia hapakuwapo na jambo lolote lenye nia ovu ya
kusababisha au kufanya uchochezi katika ujumbe
uliosambazwa na mshtakiwa.
“Sasa mahakama hii inamwachia huru mshtakiwa
baada ya upande wa Jamhuri kushindwa
kuthibitisha mashtaka yake pasipo kuacha shaka
yoyote.
“Lakini pia kama kutakuwa na upande ambao
haujaridhika katika hukumu hii unaweza kukata
rufaa,” alisema Rwizile.
Akisoma hukumu hiyo, alisema ujumbe
uliosambazwa haukuwa na umuhimu wowote kwa
kuwa haukumwelezea Mwamunyange ni nani
katika nchi anayotakiwa kuipindua huku pia
ujumbe huo ukiwa haukutaja nchi iliyolengwa
kupinduliwa.
“Ujumbe ulioandikwa katika Facebook
haumtambulishi Mwamunyange ni nani. Lakini
ujumbe hauonyeshi jambo la msingi lenye
uhusiano wa kisiasa katika Taifa linalodaiwa,”
alisema Rwizile.
Kutokana na sababu hizo ikiwamo ushahidi
uliowasilishwa mahakamani hapo kushindwa
kuthibitisha ujumbe uliosambazwa na mshtakiwa,
mahakama ililazimika kumwachia mshtakiwa.
Mshtakiwa huyo katika kesi hiyo alikuwa
akitetewa na Wakili Moses Mahuna.
Mbando anaongeza idadi ya watu walioshtakiwa
mahakamani kutokana na makosa ya mtandaoni
baada ya Aprili, mwaka huu mkazi mwingine wa
Arusha, Isack Habakuki (40), kufikishwa
mahakamani na kusomewa mashtaka ya
kusambaza lugha ya matusi na dhihaka kwa Rais
Dk. John Magufuli. Baada ya kesi hiyo kuendelea
kusomwa mahakamani hapo, Isack alihukumiwa
kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya
Sh milioni saba na yeye alikubali kuzilipa kwa
awamu.
Mtu mwingine aliyeshtakiwa Aprili, mwaka huu
kwa makosa ya mtandaoni ni kondakta wa
daladala, Hamimu Seif (42), aliyepandishwa
kizimbani kwa kosa analodaiwa kulifanya Machi
10, mwaka huu alipotishia kumuua Rais Magufuli
kwa maneno akiwa katika Baa ya Soweto iliyopo
Makumbusho, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam.chanzo mtanzania digi5l

Back To Top