Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Tuesday, January 24, 2017
Ikiwa imebaki miezi michache nchi ya Kenya kufanya uchaguzi sintofahamu na tuhuma zimeanza kutolewa.soma zaid

Ikiwa imebaki miezi michache nchi ya Kenya kufanya uchaguzi sintofahamu na tuhuma zimeanza kutolewa.soma zaid

kumekucha Kenya...
kiongozi wa upinzani Raila Odinga ametoa madai
mazito kwa shirika la ujasusi nchini Kenya {The
National Intelligence Service}
-Amesema kitengo cha ujasusi nchini Kenya
kimeingilia zoezi la kuandikisha wapiga kura
linaloendelea nchini Kenya ambapo wafanyakzi
wa kitengo hicho wamekuwa wakiandikisha raia
kutoka Uganda na Ethiopia nakupewa
vitambulisho vya Kenya ili siku ya kupiga kura
waweze kushiriki kwenye zoezi la uchaguzi ..
-Raila Odinga ametoa ujumbe kwa mkurugenzi
wa shirika hilo la ujasusi nchini Kenya Bw; Philip
Wachira Kameru kuacha kuaingilia kazi ya tume
ya uchaguzi kwasababu wananchi wa Kenya
hawatakubali matokeo ya uchaguzi ambayo
yatapatikana kwa njia ya wizi..
Raila Odinga amesema shirika hilo litasababisha
machafuko makubwa nchini Kenya kama
wataendelea kuingilia uchaguzi kwasababu
hatakubali matokeo ya wizi kama ya mwaka 2007
na 2013...
kwenye picha ni Bw: Philip Wachira Kameru
mkurugenzi wa shirika la ujasusi nchini Kenya

Mtendaji wa kijiji anusurika kifo kwa kutetea wazi wa mifugo.soma zaid

Mtendaji wa kijiji anusurika kifo kwa kutetea wazi wa mifugo.soma zaid

Mtendaji wa Kijiji cha Iponyanholo, Kata ya
Sabasabini wilayani Kahama, Shinyanga, Elias
Mpigamamoni.
Kwa ufupi
“Kwanza sikuweza kuelewa kilichokuwa
kinaendelea, taratibu nilianza kukumbuka
kwamba nilikuwa kwenye mkusanyiko wa
walinzi wa jadi muda mfupi uliopita lakini
kumbukumbu ziliniijia kwamba nilipigwa fimbo
kichwani.”
By Shija Felician, Mwananchi
“Kama ni kuonja kifo basi mimi nilikionja ingawa
ninachokumbuka ni mtu mmoja aliyenirukia na
kuanza kunipiga fimbo kichwani... Taratibu
nilianza kuona nyota nyota zikitanda usoni na
baadaye nilishtuka nikiwa kwenye gari huku nguo
zangu zote zikiwa zimelowa damu.
“Kwanza sikuweza kuelewa kilichokuwa
kinaendelea, taratibu nilianza kukumbuka
kwamba nilikuwa kwenye mkusanyiko wa walinzi
wa jadi muda mfupi uliopita lakini kumbukumbu
ziliniijia kwamba nilipigwa fimbo kichwani.”
Ndivyo anavyoanza kueleza Elias Mpigamamoni
mwenye umri wa miaka 49 kufutia kisa cha yeye
kupigwa na wananchi wenzake kwa kile
kilichodaiwa kuwa alikuwa akiwatetea wezi wa
mifugo.
Kwa mujibu wa Mpigamamoni, baada ya kupata
fahamu aliwatambua watu wote waliokuwa ndani
ya gari hiyo na haraka akagundua kuwa kumbe
safari hiyo ni yake alikuwa akipelekwa hospitalini
baada ya kupata majeraha kichwani na usoni
kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa
wananchi.
Jinsi ilivyokuwa
Mpigamamoni ambaye ni Mtendaji wa Kijiji cha
Iponyanholo kata ya Sabasabini wilayani
Kahama, Shinyanga anasema kuwa alipata kipigo
hicho wakati akiwazuia walinzi wa jadi
sungusungu kuwaua watuhumiwa wawili wa wizi
wa ng’ombe waliokuwa wamewakamata.
Anasema mara baada ya walinzi hao kuwatia
nguvuni watuhumiwa hao walianza kuwapiga kwa
lengo la kuwaua ndipo alipotokea yeye na
kupinga kitendo hicho ambapo alitaka wafikishwe
katika vyombo vya sheria.
“Nilikuwa nikitekeleza agizo la Serikali kwa
viongozi wake kusimamia amani hasa maeneo ya
vijijini ambako ukiukwaji wa sheria umekithiri
kwani kwa mujibu wa taarifa Wilaya ya Kahama
inaongoza kwa mauaji ya watu wasio na hatia
ambao huuawa kwa kuchomwa moto au kukatwa
mapanga.
Mpigamanoni anasema kuwa alipigiwa simu na
diwani wa kata hiyo Emmanuel Makasi aende
kwenye tukio hilo ambalo sungusungu walikuwa
wamewazingira watuhumiwa wakitaka kuwaua
kwa kuwachoma moto.
Kutokana na hali hiyo mtendaji huyo alitumia
nguvu kubwa kuzuia wananchi hao wasifanye
mauaji hayo waliyokusudia.
Anasema baada ya kuwazuia alishtukia ameanza
kushambuliwa kwa fimbo kichwani huku akisikia
sauti za watu zikidai mtendaji huyo pamoja na
watuhumiwa wa wizi wa ng’ombe wauwawe kwa
kuchomwa moto na kazi hiyo ilianza.
Anasema alisikia sauti zikisema
mnawachelewesha, watu hao wanapaswa
kuuawa wote na hapo kijana mmoja alichomoka
kwenye kundi na kuanza kumshambulia mmoja
wa watuhumiwa.
Pamoja na juhudi za kumuokoa kushindikana
kibao kilimrudia yeye na kushambuliwa kwa
kipigo na watu hao mpaka alipopoteza fahamu na
hajui ni nani aliyemuokoa.
Anasema baada ya shambulio hilo alipoteza
fahamu na kupelekwa hospitali ya Halmashauri
ya Mji wa Kahama ambako alipatiwa matibabu.
Mganga mfawidhi katika hospitali hiyo Dk Joseph
Ngowi anasema mtendaji huyo alifikishwa hapo
akiwa na majeraha kichwani ambayo yalionyesha
yalitokana na kupigwa na vitu vizito.
Ngowi anasema hivi sasa hali yake ni nzuri
ingawa ataendelea kufanyiwa uchunguzi
kutokana na majeraha hayo ya kupigwa yalikuwa
kichwani hali ambayo inaweza kuwa na madhara
kwa ndani.
Mtendaji wa kata ya Sabasabini Christopher
Lyogelo anasema mtendaji huyo alipigwa akiwa
kwenye majukumu yake ya kutekeleza agizo la
Mkuu wa Wilaya na mkakati mzima wa kata hiyo
kuzuia matukio ya wananchi kuua watu
wanaowatuhumu kwa wizi wa mifugo.
Diwani wa kata hiyo Emmanuel Makashi
anasema mtendaji huyo alipigwa baada ya
kutokea ugomvi kati yake na mtu mmoja
aliyejulikana kwa jina la Nkinga Nzinza ambaye
hata hivyo alikimbia kusikojulikana. Mpaka sasa
polisi mjini Kahama wanaendelea kumsaka kwa
RB Namba KAH/RB/7721/2016.
Makashi anasema baada ya mtendaji kupigwa na
yeye kufika kwenye tukio alituliza vurugu hizo na
watuhumiwa wote aliwatoza faini za jadi ambapo
kwa pamoja walilipa Sh150,000 na ng’ombe
mmoja ambaye alirejeshwa kwa mwenyewe na
fedha hizo ziligawanywa zote kwa
wanasungusungu.
Kutokana na hali hiyo baadhi ya wadau wa
maendeleo wilayani Kahama akiwamo Jackson
Mpejiwa wameeleza kuwa Serikali inapaswa
kuangalia upya ulinzi wa sungusungu vijijini
kutokana na uamuzi wao kutozingatiwa.
Polisi wazungumza
Kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro
Jumanne amekiri kutokea kwa tukio hilo na
kusema kuwa uchunguzi unaendelea juu ya tukio
hilo.
“Ni kweli tumepokea taarifa juu ya kujeruhiwa
kwa mtendaji huyo wakati akijaribu kuzuia
sungusungu wasiwaue watu wanaotuhumiwa kwa
wizi wa mifugo.
“Nataka kutoa wito kwa wananchi waache
kujichukulia sheria mikononi kwani si jambo
jema. Endapo watakamata watuhumiwa ni vyema
wawafikishe katika kituo cha polisi kwa taratibu
za kisheria,” anasema Kamanda Jumanne.
Awali diwani Makashi alisema sungusungu hao
wamekubaliana kufanya kikao cha mazungumzo
ya kulimaliza tatizo hilo mezani.
Agizo la Mkuu wa Wilaya
Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Basil
Nkurlu alifanya mkutano wa pamoja na watendaji
wa kata na vijiji na kuwaeleza kwamba yeyote
yule ambaye atabainika kwamba kwenye eneo
lake kuna mtu ameuawa na wananchi ataanza
kuwajibika nae kwanza.

Kauli ya Uhuru Kinyatta imetoa mwanga kwa wapinzani.soma zaid

Kauli ya Uhuru Kinyatta imetoa mwanga kwa wapinzani.soma zaid

Alisema hayo alipokuwa anazungumza na
waandishi wa habari katika Ikulu Ndogo ya
Sagana, akiwa kwenye ziara maeneo ya
Murang’a, Nyeri, Laikipia, Meru na Isiolo kuhimiza
wananchi wajiandikishe kwenye kitabu cha
kupigia kura
Nairobi. Rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba
atakabidhi madaraka kwa amani ikiwa
atashindwa na mgombea urais wa upinzani
kwenye Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika Agosti
8 mwaka huu.
Alisema hayo alipokuwa anazungumza na
waandishi wa habari katika Ikulu Ndogo ya
Sagana, akiwa kwenye ziara maeneo ya
Murang’a, Nyeri, Laikipia, Meru na Isiolo kuhimiza
wananchi wajiandikishe kwenye kitabu cha
kupigia kura
“Nitakubali lolote litakaloamuliwa na wananchi
kwani enzi za marais kung’ang’ania madaraka
zimeshapita,’’ alisema.
Aliongeza, “Enzi hizo zilipita. Enzi hizo haziko
tena kwa sababu katiba inasema Rais anatakiwa
kutawala kwa vipindi viwili vya miaka mitano kila
kimoja,” alisema.
Kuiba kura
Rais Kenyatta alisema kauli za viongozi wa
upinzani wanaosema kwamba Jubilee inapanga
kuiba kura kwa sababu haitaki kuondoka
madarakani siyo za kweli.
‘’Baadhi yao wanadai huenda Jubilee ikabadilisha
katiba ili kuirudisha Kenya katika enzi za chama
kimoja cha kisiasa, hasa baada ya vyama tanzu
vya muungano wa Jubilee kuvunjwa kuunda
Jubilee Party’,’ alisema.
Rais Kenyatta aliwahimiza vijana wajisajili kwa
wingi kuwa wapigakura ili waweze kushiriki
Uchaguzi Mkuu ujao.
Rais aliitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka
(IEBC) izishinde kwenye vituo bali wazunguke
kuwaandikisha watu wanaoishi kwenye maeneo
ya wafugaji.
Mudavadi
Akiwa Busia, kiongozi wa chama cha Amani
National Congress (ANC), Musalia Mudavadi
alitoa changamoto kwa Rais Kenyatta aagize
idara ya kusajili watu itoe vitambulisho katika
muda wa siku tatu.
Alisema agizo hilo linatakiwa kutekelezwa kote
nchini wala si katika ngome za Jubilee pekee ili
kuwe na usawa kwenye Uchaguzi Mkuu wa
Agosti 8.
Akiwa Baringo, Naibu Rais William Ruto alisema
chama cha Jubilee kitashinda urais kwa sababu
ya rekodi yake ya maendeleo, aliwataka wafuasi
wa chama hicho wasiwe na wasiwasi.

Rais Trump ameanza kukoroga mambo amefanya maamzi haya.soma zaid

Rais Trump ameanza kukoroga mambo amefanya maamzi haya.soma zaid

TRUMP aiondoa MAREKANI kwenye mkataba wa
kibiashara wa PACIFIC
Rais DONALD TRUMP wa MAREKANI ametia
saini kuiondoa MAREKANI kwenye Mkataba wa
Makubaliano ya Kibiashara kwa nchi za PACIFIC,
unaojulikana kama TPP.
Jambo hilo ni moja ya agenda muhimu alizokuwa
akizungumzia wakati wa kampeni na hivyo
kuamua kusaini kuiondoa MAREKANI kwenye
biashara na nchi hizo na kusema hatua hiyo ni
neema kubwa kwa wafanyakazi wa MAREKANI.
Mkataba huo ulikuwa unazihusisha nchi 12
zikiwemo AUSTRALIA, BRUNEI, CANADA, CHILE,
JAPAN, MALAYSIA, MEXICO, NEW ZEALAND,
PERU, SINGAPORE, MAREKANI na VIETNAM.

Mtu mmoja amefari kwa ajali ya basi ya Vitu Laini mkoan Iringa.soma zaid

Mtu mmoja amefari kwa ajali ya basi ya Vitu Laini mkoan Iringa.soma zaid

MTU mmoja amefariki dunia katika ajali
ya basi la kampuni ya Vitu Laini lenye namba za
usajili T910 linalofanya safari zake kati ya
Lulanzi Kilolo na Iringa Mjini baada ya kuligonga
lori lenye namba T724 AVV scania lililokuwa
limebeba Mbao.
Ajali hiyo imetokea asubuhi leo hii eneo la
Tagamenda Mjini Iringa wakati basi hilo likitokea
Kilolo kwenda Iringa mjini na kuelekea mwelekeo
wa Lori hilo.
Chanzo kimeelezwa ni mwendo kasi wa basi hilo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
amefika eneo La tukio pamoja na kamati yake ya
ulinzi na usalama.

Monday, January 23, 2017
Morogoro hapatoshi polisi watumia mabomu kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA.soma zaid

Morogoro hapatoshi polisi watumia mabomu kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA.soma zaid


Jeshi la polisi mkoani Morogoro
limelazimika kutumia mabomu ya machozi
na mbwa kuwatawanya wananchi wa kata
ya Kiwanja cha ndege waliofika katika
kituo cha kutangazia matokeo ya
uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata
hiyo.
Hali hiyo imeibuka mara baada ya
mgombea wa udiwani kwa tiketi ya
CHADEMA Salum Milindi kufika katika
kata hiyo akiwa amenyanyua mikono juu
na kutaka kuingia ndani ya chumba cha
matokeo kwa mujibu wa sheria huku
akizuiliwa na jeshi la polisi.
Mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM
Isiaka Sengo aliibuka kidedea kwa kupita
mpinzani wake wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo CHADEMA Salum Milindi
kwa kura 192 ambapo msimamizi
msaidizi wa uchaguzi Shabani Duru
amemtangaza Isiaka Sengo kuwa diwani
wa kata hiyo.
Awali wakizungumza na ITV wasimamizi
katika vituo wameeleza changamoto zilizo
kuwepo ikiwa nipamoja na wananchi
kutojitokeza kwa wingi.chanzo itv

Magari ya kifahari wapigwa stop uwanja wa Ndege Gambia.

Magari ya kifahari wapigwa stop uwanja wa Ndege Gambia.

IKULU Gambia imeamuru na kuzuia
magari yote ya kifahari yaliyobaki
yaliyokuwa yakimilikiwa na Yahya Jammeh
yaliyopelekwa Airport ya Gambia
iliyasisafirishwe kumfuata kiongozi huyo
aliyeenda kuishi uhamishoni nchini
Guinea ya Ikweta.

Back To Top