Mwanafunzi akamatwa akimfanyia mtihani fomu four ndugu yake.
Jeshi la polisi mkoani kagera linamshikilia Ashraf Amin Kaitaba mwanafunzi wa kidato cha tatu anayesoma katika shule ya sekondari ya Bukoba iliyoko mkoani humo aliyekamatwa jana na maofisa wa jeshi hilo wakati akijaribu kufanya jitihada za kuingia kwenye chumba cha mtihani kilichondaliwa katika Chuo cha walimu cha Nshambya kwa ajili ya kituo cha watahiniwa binafsi wanaofanya mtihani wa kidato cha nne unaoendelea sasa aliyekuwa na lengo la kuingia katika chumba hicho kwa lengo la kumfanyia kaka yake mtihani huo ambaye ni miongoni mwa watainiwa binafsi. Akizungumza juu ya tukio hilo mbele ya waandishi wa habari akiwa ofisini kwake,Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Kamishina Mwandamizi, Augustine Ullomi amesema mwanafunzi huyo alikuwa na nia ya kuingia katika chumba hicho kwa lengo la kumfanyia mtihani kaka yake aliyemtaja kwa jina la Amir Amin Kaitaba ambaye amesema naye anashikiliwa na jeshi hilo. Kufuatia tukio hilo Kamanda Ullomi amesema jeshi hilo litahakikisha mitihani ya kidato cha nne inayoendelea sasa inafanyika kulingana na kanuni na taratibu zilizopo na ametoa onyo kwa walimu, wazazi na wanafunzi watakaojihusha na vitendo vya udanganyifu wakati wa zoezi la kufanya mitihani hiyo. Chanzo: ITV