Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Tuesday, February 28, 2017
Kimenukaa: Wabunge wamlipua Steve Nyerere baadhi wakataa kuombwa msamaha.soma zaid

Kimenukaa: Wabunge wamlipua Steve Nyerere baadhi wakataa kuombwa msamaha.soma zaid

Kusambaa kwa sauti iliyorekodiwa mazungumzo ya mwigizaji Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ na mama wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu halijafutika, mengine yamefumka kwani baadhi ya wabunge waliotajwa kwenye sauti hiyo wamelimpua Steve. Mbali na wabunge kutajwa katika sauti hiyo iliyosambaa wiki iliyokatika, wasanii pia walitajwa ambao ni Khaleed Mohamed ‘TID’, Romeo George ‘Rommy Jones’ na Ahmed Hashim ‘Petit Man’. Kwa upande wa wabunge ni Goodluck Millinga (CCM-Ulanga), Ahmed Shabiby (CCM-Gairo), Joseph Musukuma (CCMGeita Vijijini), Freeman Mbowe (Chadema-Hai) na Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo, Kigoma Mjini). Steve pia aliwataja mawaziri wawili. Steve alisikika akiwataja wabunge hao akimwambia mama Wema kuwa, aliwafuata bungeni mjini Dodoma, Februari 6, mwaka huu ili wamsaidie bintiye aliposhakiliwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar ‘Sentro’ kwa madai ya kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, ikiwemo kukutwa na bangi. STEVE AOMBA RADHI WOTE Hata hivyo, baada ya sauti hiyo kusambaa mitandaoni Februari 23, mwaka huu na kuwa gumzo, Jumamosi iliyopita, Steve alifanya mkutano na waandishi wa habari katika Jengo la Millennium Tower, Kijitonyama na kuwaomba radhi wote aliowataja huku akikiri sauti ni yake na kwamba, hakuzungumza nao kama ‘alivyomwongopea’ mama Wema bali aliwataja katika hali ya kudumisha ukaribu wake na familia ya mama huyo. UWAZI NA WABUNGE Baada ya mkutano huo, Uwazi liliwatafuta wabunge hao, kasoro Mbowe hakupokea simu, na waliopatikana walikuwa na haya ya kusema: SHABIBY: “Steve Nyerere namfahamu. Lakini sina ukaribu naye. Niliwahi kukutana naye muda mrefu kwenye hoteli yangu ya Moleno, Dodoma. “Nakumbuka alikuja na mwanamuziki Ray C (Rehema Chalamila), lakini baada ya hapo sijawahi kuonana naye popote maana hata baada ya kukutana naye sikuwahi kuwasiliana naye. “Kuhusu kunihusisha mimi katika sakata la Wema, yale mazungumzo nimeyasikia vizuri. Si kweli alichokisema eti alikuja kukutana na Musukuma kwenye hoteli yangu na mimi nikiwepo. Ni uongo mtupu. “Sijaonana na Steve Nyerere katika siku za hivi karibuni na sijazungumza naye lolote lile hata kwa njia ya simu,” alisema Shabiby. MILLI NGA: “Ninafahamu kila kitu kinachoendelea, maana Steve Nyerere ni mtu ambaye tunakutana mara kwa mara, ukizingatia ni kada mwenzangu kwenye Chama Cha Mapinduzi. Kuhusu yeye kunishawishi mimi kumtetea Wema bungeni, jambo kama hilo halipo maana sikuwahi kukutana naye kabla ya mimi kuzungumza bungeni. “Ila baada ya bunge, jioni nilikutana naye, akaniambia kuwa, nilichokiongea ni kama nilitazama kilichokuwa moyoni mwake. Hata hivyo, nimemsamehe maana ameomba radhi kwenye mkutano na waandishi wa habari!” ZITTO: “Mimi siwezi kusemea jambo hilo maana mimi kwangu halina maana yoyote.” MUSUKUMA: “Nisikilize vizuri mwandishi, mimi Steve Nyerere hana mchango wowote kwenye maisha yangu. Mimi ni Mbunge wa Geita Vijijini na sifanyi kazi yangu ya ubunge kwa kushawishiwa na mtu. “Steve Nyerere anaweza kunishawishi mimi kwa kipi? Ngoja nikwambie kitu, kinachoendelea ni kiki ya Steve Nyerere na watu wake maana kama umesikia ile ‘place’ na waandishi aliyoitisha, anasema Makonda ni rafiki yake, sasa unaweza kupima kinachoendelea hapo.” MUSUKUMA AKATAA RADHI YA STEVE Alipoulizwa kuhusu radhi aliyoiomba Steve Nyerere kwa wote aliowataja yeye ameipokeaje, alisema: “Kama ameomba radhi basi amewaomba wananchi wangu wa Geita waliyoniweka kwenye nafasi yangu kwa lengo la kuwatetea wananchi na si kufanya kazi kwa ushawishi wa mtu.” TID KWENDA KORTINI? Taarifa zaidi zilisema kuwa, Mbongo Fleva, TID anajipanga kumfikisha Steve kortini baada ya sauti yake kumtaja akisema anamchukia sana yeye huku pia kukiwa na habari kwamba, baadhi ya wanasheria jijini hapa wamepanga kujitokeza kwa waliotajwa ili kuangalia uwezekano wa kumfungulia kesi mama Wema ambaye anatajwa na Steve mwenyewe kuwa, ndiye aliyemrekodi.

Makubwa haya...Mkuu wa wilaya akataza watu kula kitimoto kisa hiki hapa.soma zaid

Makubwa haya...Mkuu wa wilaya akataza watu kula kitimoto kisa hiki hapa.soma zaid

Walaji wa nyama ya nguruwe ‘kitimoto’ wilayani Kalambo mkoani Rukwa watakikosa kitoweo hicho kwa muda usiojulikana baada ya Serikali kupiga marufuku watu kula nyama hiyo. Hatua hiyo imefikiwa baada ya nguruwe 150 kufa kwa ugonjwa wa mafua wa African Swine Fever na kuwaacha wengine wakiwa hoi. Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Julieth Binyura alisema ugonjwa huo ulijitokeza miezi mitatu iliyopita kwenye Kitongoji cha Masazi na kusambaa katika kata za Legezamwendo na Mambwe Nkoswe. Ofisa Mifugo wa Wilaya ya Kalambo, Wilbroad Kansapa alisema nguruwe wote wanaozagaa mitaani watakamatwa na mizoga yote ifukiwe.

Wema sepetu: Hiki ndio kitu ninachokipenda zaid katika harakati zangu.soma zais

Wema sepetu: Hiki ndio kitu ninachokipenda zaid katika harakati zangu.soma zais

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye wiki iliyopita amekihama chama chake cha muda CCM na kuingia CHADEMA amefunguka na kusema kuwa anaipenda sana siasa na siku akifanikiwa katika siasa atafurahi sana kwa kuwa ni kitu anachokipenda sana. Wema Sepetu kupitia account yake ya Twitter amesema ameamua kuhama CCM na kuingia CHADEMA ili kupigania uhuru pamoja na demokrasia ambayo anahisi kwamba imeanza kupotea nchini Tanzania. "Hicho ndicho tunachokwenda kupigania, uhuru tuliokuwa nao pamoja na democracy tunayoanza kuipoteza. God guide us. Hujajua tu ni jinsi gani siku nitakapofanikiwa kuwa mwanasiasa nitakavyo furahi... Naipenda siasa sana Maybe ni roots za Daddy" aliandika Wema Sepetu Mbali na hilo Wema Sepetu anasema sasa hivi amekuwa na amani na furaha moyoni mwake. " Saizi nina amani ya ajabu moyoni mwangu... I thank my Good Lord... Kweli kila kitu katika maisha hutokea kwa sababu, saizi niite kamanda " alisisitiza Wema Sepetu

Mkuu wa shule ya sekondari ajinyonga Singida sababu ni nini?.soma zaid

Mkuu wa shule ya sekondari ajinyonga Singida sababu ni nini?.soma zaid

Mkuu wa Shule ya Sekondari Tumuli katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida, Richard Makala (58) amejinyonga kwa kamba kutokana na kile kinachodhaniwa ni upweke. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, amesema mjini Singida kuwa Mkamala alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa vipande vya chandarua iliyofungwa juu ya mti umbali wa mita 130 kutoka nyumbani kwake. Aidha kamanda huyo alisema chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba hakuna mtu au watu wanaoshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuongeza kuwa polisi inaendelea na upelelezi kubaini kilichomsibu mwalimu huyo. Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mabruki Ng’ui ameliambia gazeti la Habarileo Jumatatu hii kuwa mwalimu huyo alikuwa anaishi peke yake kwa muda mrefu baada ya mkewe ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Tanzania (KKKT) Kitusha wilayani Iramba kuamua kutengana naye kutokana na unywaji pombe. “Huyu bwana amekuwa kwenye ndoa ya jina tu maana mke wake amekuwa akiishi mbali naye kwa kipindi kirefu sana, amekuwa mpweke kwa muda mrefu mno huenda hicho ndicho kilichosababisha ajitoe roho yake,” amesema Mjumbe huyo wa Bodi. Marehemu Makala ni mzaliwa wa kijiji cha Ndago, wilayani Iramba na anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake, ameacha mjane na watoto watano.

Mpende anayekupenda asiyekupenda kwanini uumie kwa ajili yake? fahamu kilichomkuta huyu.soma zaid

Mpende anayekupenda asiyekupenda kwanini uumie kwa ajili yake? fahamu kilichomkuta huyu.soma zaid

Ili mapenzi yaweze kuwa bora kwa kila aliye katika mahusiano, huwa ni vyema kila mmoja kuiona thamani ya mwenzake. Ukipenda kujiangalia mwenyewe si ajabu mwenzako kupata hisia za kuwa humthamini wala humjali. Muunganiko wenu katika mapenzi maana yake tayari mmekuwa kitu kimoja. Katika mimi unaweka sisi. Ila pia ni vyema ikakumbukwa ladha na maana halisi ya mapenzi ipo kwa anayekupenda na kukuthamini. Unapokuwa na uhakika kama anakupenda na kukuthamini hapo ndipo nafsi yako itatulia na kuwa na amani. Ndani ya mapenzi na mtu wa aina hii ni amani na utulivu kwa kwenda mbele. Hakuna majuto wala majonzi ya kila siku. Unapoamua kuwa katika mahusiano na mtu ambaye hakupendi, bali unakuwa naye kwa kuwa tu unampenda jua umejiingiza katika utumwa. Mapenzi ni suala la kihisia zaidi. Mwenzako anapokosa hisia na wewe maana yake hata uwepo wako hauthamini inavyopaswa. Na hapo ndiyo tunaona yale mahusiano ya kingono yanapozaliwa na si ya kimapenzi kwa maana halisi. Yaani mwenzako anapokuwa na mihemko ya kingono ndipo anapokutafuta na si vinginevyo. Niliwahi kuongea na msichana mmoja aliyewahi kuniambia anampenda kijana mmoja ambaye anauhakika kabisa yeye hampendi. Alinambia uhakika huo kaupata kutokana na kijana huyo kumtakia kuna msichana yupo anampenda na kumjali ila si yeye. Kuonesha zaidi kumpenda msichana yule mwingine, jamaa aliwahi kumwambia kama ikitokea hata huyu msichana akagombana na yule mpenzi mwingine wa yule jamaa, kijana yule alikuwa radhi kumdhuru huyu msichana. Hata kwa matazamo wa haraka hapo unaweza kugundua ni kwa namna gani huyu msichana alikuwa haitajiki. Ila cha kushangaza msichana huyu(aliyeongea na mimi) alimwambia mvulana husika yuko radhi kuwa naye hivyo hivyo. Aliamua kuwa hivyo akiamini ipo siku jamaa atamuelewa. Kweli walikuwa pamoja. Ila unajua kinachomkuta sasa? Kila jamaa anapogombana na yule msichana mwingine anamtumia huyu kingono na mambo mengine yasiyo ya kimapenzi, na bila kutafakari mara mbili huyu msichana anafanya kwa kile anachoamini hali hiyo itamfanya huyu jamaa amfikirie zaidi. Kuna kitu cha kuangalia hapa. Suala la mapenzi si suala la kuoneana huruma wala aibu. Mapenzi ni hisia. Unapojitoa kwa mwenzako kwa kila jambo na unamuona haelekei ujue hana hisia na wewe. Kwanini unakubali kuteseka na kuumia kila siku kwa kumuangalia yeye tu? Ndiyo, unampenda sana, unamjali sana na unamuhitaji sana, ila kama yeye hakutaki wa kazi gani? Ni muda wa kujiangalia na wewe sasa. Ona thamani yako kama binaadamu, jionee huruma jinsi unavyoteseka kila siku kwa mtu asiyeona thamani yako. Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani, bila kujali muonekano wala rangi yako. Unahitaji mwenye kukuthamini na kukujali na si anayekufanya kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa utumwa wa mapenzi kwa kuiona thamani yako. Ni vyema ukalia kwa kumkosa kuliko kuonekana unaye wakati moyoni siyo wako. Hakuna sifa ya kuwa na mtu mwenye fedha au muonekano mzuri ikiwa hakujali wala haupo moyoni mwake. Mapenzi ni amani na raha. Mapenzi hufanya watu wafurahi na kusahau shida zao. Ila jiulize kwanini kwako hayako hivi? Unaenda kwa mwenzako badala afurahie uwepo wako, yeye anaona unajipendekeza. Unampigia simu na kumpa maneno mazuri ya faraja, yeye anaona unamsumbua. Sasa wa kazi gani? Siku njema wapendwa.
Sunday, February 26, 2017
no image

Mbunge wa Babati mjini CHADEMA anusurika kifi sasa yuko ICU

Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya ambapo mmbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira luhaga mpina wilayani babati mkoa wa manyara. Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mmbunge huyo na kulazimika kumsubiri naibu waziri ambaye ameingia kumuona mbunge Gekul na hapa naibu waziri Mpina anaeleza. Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira akalamika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwaajili ya kubebbea taka lenye dhamani ya zaidi ya milioni 200

Wachawi  wapanga kumuondoa Rais wa marekani Donard Trump madarakani.soma zaid

Wachawi wapanga kumuondoa Rais wa marekani Donard Trump madarakani.soma zaid

Wapinzani wengi wa rais wa Marekani Donald Trump, wanaamini kuwa itawabidi wasubiri kwa miaka minne ili aweze kuondoka madarakani. Lakini wachawi nchini Marekani hawakubaliani na hilo. Usiku wa manane siku ya Ijumaa, wale wanaoamini uchawi kote nchini Marekani, waliandaa matambiko yenye nia ya kumuondoa Trump uongozini. Hadi sasa ukurasa wa Facebook wa matambiko huyo umepata wafuasi 10,500. Hatua hizo zimezua ghadhabu kotoka kwa wakirsto ambao wamewalaumu wachawi hao wa kutangaza vita vya kiroho. Wachawi hao wanapanga kurudia tambuko hilo hadi pale Trump atakapoondoka ofisini. Tambiko lingine litafanyika machi 26. Chama cha wakiristo nacho kilitangaza tarehe 24 mwezi Februari kama siku ya maombi ya kuukabili uchawi huo. Hata hivyo Trump hajazungumzia lolote kuhusu vita hivyo kati ya kanisa na uchawi.

Saturday, February 25, 2017
Mtaalamu wa  saikologia anasema Wanaume wanaongoza kujinyonga wakishindwa kuvumilia aibu.soma.zai

Mtaalamu wa saikologia anasema Wanaume wanaongoza kujinyonga wakishindwa kuvumilia aibu.soma.zai

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa wanawake wanauwezo mkubwa zaidi wa kuvumilia wanapopatwa na aibu kuliko wanaume ambao baadhi yao huamua kujinyonga. Kauli hiyo imetolewa na mtaalamu wa saikolojia katika Chuo cha Ualimu Patandi, Tawi la Sahare Tanga, Modesta Kamoga alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu tukio la mfanyabiashara Mohammed Mohammed (46) mkazi wa Dar es Salaam kumuua mkewe, Sophia na kisha kujinyonga. Mohammed alimuua mkewe na kuacha ujumbe wenye kurasa 80 ukieleza sababu za kufanya tukio hilo, kubwa ikielezwa kuwa ni mgogoro wa kimapenzi wa muda mrefu. “Wanaume wanapokumbwa na aibu kubwa kama huyo mtu aliyegundua kuwa watoto siyo wa kwake. Angekuwa mwanamke akajua mumewe ana watoto nje ya ndoa, anakwenda kumwambia mtu wake wa karibu, wanaume hawawezi kutoa sumu moyoni,” alisema.

no image

Gari la mumbunge wa Tarime Mjini laua, mwenyewe anusurika.soma zaid

Magu. Mtumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Moses Mjuni amefariki dunia baada ya kugongwa na gari la Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko katika Kijiji cha Kishamba wilayani humo. Mkuu wa Wilaya ya Magu, Khadija Nyembo alisema jana kwamba ajali hiyo ilitokea juzi saa mbili usiku, “Gari la mbunge lilimgonga mtumishi wetu wa Hospitali ya Magu ambaye alikuwa anaendesha pikipiki na dereva wa gari hilo amekamatwa yupo polisi,” alisema Nyembo. Akizungumza kwa simu jana, Matiko alisema ajali hiyo ilitokea takribani kilomita 10 kutoka Daraja la Mto Simiyu wakati akitoka Mwanza ambako walikutana na mwendesha pikipiki na dereva wake, Kelvin Matango alikuwa akimkwepa baada ya kuingia upande wake. “Nilitoka Mwanza saa 12:00 jioni kwenda jimboni kwangu (Tarime), tulipopita mbele kidogo karibu kilomita10 kutoka daraja la Mto Simiyu, ghafla alijitokeza mwendesha pikipiki akawa anaendesha kwa kuyumbayumba na dereva alishindwa jinsi ya kumkwepa akamgonga, mimi nilikuja kuona yule mtu ameshafariki dunia,” alisema Matiko. Matiko alisema licha ya kwamba hakupata majeraha, baada ya kutokea ajali hiyo alipelekwa katika Hospitali ya CF ya jijini Mwanza ambako alipewa dawa na kuruhusiwa. Hata hivyo, Matiko alisema alikuwa akisikia maumivu makali ya mgongo na mbavu hivyo kutakiwa kwenda kufanyiwa vipimo kuona kama atakuwa amepata madhara. “Nasikia maumivu makali ya mgongo na mbavu za kulia, nahisi mkanda wa gari ulinibana zaidi, nilitakiwa kwenda hospitali ya CF kufanyiwa uchunguzi lakini nimeshindwa kwa sababu hapa tunapozungumza naenda Magu kumaliza masuala ya polisi kwani dereva na gari vipo polisi,” alisema Matiko. Alisema baada ya kumaliza kushughulikia masuala hayo ndipo atarudi tena hospitali kufanya uchunguzi wa afya yake. Mwanajeshi afa, 10 wajeruhiwa Arusha Katika ajali nyingine iliyotokea mkoani Arusha, askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), George Ngwegeta alifariki katika Kijiji cha Oldonyosambu wilayani Arumeru. Watu wengine 10 wamejeruhiwa katika tukio hilo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema jana kuwa mwanajeshi huyo pamoja na majeruhi hao, walikuwa wamepanda gari dogo la abiria aina ya Nissan Caravan wakitoka Namanga kuelekea Arusha. Alisema gari hilo lilipinduka mara tatu baada ya kupasuka tairi la mbele likiwa katika mwendo wa kasi na dereva gari hilo linalofanya safari zake kati ya Arusha na Namanga, Pailoti Pamphili alishindwa kulidhibiti. Kamanda Mkumbo alisema dereva huyo anashikiliwa. Kuhusu majeruhi, Kamanda Mkumbo alisema hadi jana jioni, walikuwa wamelazwa katika Hospitali za Selian na Mount Meru na watano kati yao hali zao hazikuwa nzuri.

Machangodoa Dar kuanza kushughulikiwa nazo baa zinazowahifadhi kuchukuliwa hatua.soma zaid

Machangodoa Dar kuanza kushughulikiwa nazo baa zinazowahifadhi kuchukuliwa hatua.soma zaid

MKUU wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Ali Hapi, ametoa onyo kwa wamiliki wa baa wanaowahifadhi watu wanaojihusisha na biashara ya ngono ‘Machangudoa’ kuwa watafutiwa leseni. Ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata ya Kijitonyama waliodai kuwa kuna baadhi ya baa zimekuwa zikiwahifadhi wanaouza miili, hali ambayo ni hatari kwa mazingira na makuzi ya watoto. Hapi amesema haiwezekani serikali iwe inapambana na biashara hiyo haramu lakini kuna baadhi ya baa zinawafuga machangudoa. "Tutashughulika na changudoa na tutashughulika na wenye baa zinazowahifadhi machangudoa, kwa sababu hili ni suala lililo kinyume cha sheria, serikali inapambana na hili tatizo halafu mwingine analikumbatia, hilo haliwezekani, tutawachukulia hatua za kisheria," amesema. Awali, akitoa malalamiko yake kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete, mkazi wa Kijitonyama alidai kuna baa zilizogeuka kero kwao. Ameitaja baa iitwayo Kona ya Sinza imekuwa ikiwahifadhi machangudoa hivyo kuhatarisha makuzi ya watoto kwa kuwa wanaweza kuiga tabia zisizofaa. "Hii baa iko hapo Afrika Sana, machangudoa wako pale wanajiuza hadharani, sasa kwa kweli hii ni kero kubwa kwetu, watoto wanaweza kuiga na matokeo yake tutakuwa na kizazi kibaya ," amesema mwananchi huyo.chanzo muungwana blog

Serikal imesema kila mtoto mwenye uwezo wa kwenda shule anaenda.soma zaid

Serikal imesema kila mtoto mwenye uwezo wa kwenda shule anaenda.soma zaid

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema ili kuwa na taifa lenye ustawi, jamii haina budi kuwekeza kwenye makuzi mema ili kuepuka kuwa na taifa la vijana wasio na maadili. Aidha, amesema serikali inapopambana na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, matumizi holela ya pombe za viroba, mimba za utotoni na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ili kuboresha huduma za jamii, lengo lake ni kujenga kesho iliyo bora kwa vijana. Waziri Mkuu aliyasema hayo juzi usiku katika hafla ya chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia maadhimisho ya siku ya Skauti Afrika na miaka 100 ya Uskauti Tanzania, iliyoandaliwa na Chama cha Skauti Tanzania. Alisema nusu ya Watanzania ni vijana, hivyo ni muhimu kuweka mazingira mazuri kwa ajili yao. Chama cha Skauti kama moja ya taasisi kongwe nchini ni wadau muhimu katika malezi ya vijana. "Tunaposhuhudia makundi kama Panya Road, ongezeko la vijana wenye uraibu wa dawa za kulevya na ongezeko la mimba za utotoni, sanjari na kuhoji nafasi ya wazazi kwenye malezi ya watoto wetu, tunadhani ni wakati mwafaka pia kwa Chama cha Skauti nacho kujitathmini endapo bado kina ushawishi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na endapo kuna jambo linaweza kufanyika ili kurekebisha hali hiyo," amesema Waziri Mkuu Majaliwa. Alisema serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwa ajili ya kuhakikisha kila mtoto mwenye uwezo wa kwenda shule anafanya hivyo, bila kikwazo. Alifafanua kuwa serikali imekuwa ikitoa Sh bilioni 18.7 kila mwezi ambazo zimesaidia kuondoa ada na michango yote kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne. Pia alishauri kamati inayoandaa shughulli hizo kubuni njia mbalimbali za kupata michango kama kuwa na mechi za soka, mabonanza ya muziki, bahati nasibu na kampeni za uchangiaji kupitia makampuni ya simu za mkononi. Aidha, alishauri kamati hiyo kuona uwezekano wa kuunganisha matukio ya maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania na Siku ya Skauti Afrika kuyafanya kwa pamoja na kwa bajeti ndogo, ili fedha zitakazookolewa zitumike katika shughuli mbalimbali za kuhamasisha uskauti nchini. Awali, Rais wa Chama cha Skauti nchini na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema, chama hicho kimekuwa msaada mkubwa katika kuwajenga vijana katika mazingira bora. Alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuwahamasisha vijana kuwa raia bora wenye kuwajibika ipasavyo. Alisema maadhimisho hayo yanahitaji Sh milioni 600 ili yaweze kukamilika, kwani yatashirikisha na nchi nyingine mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika. Katika chakula hicho cha hisani, fedha zilizopatikana kwa ahadi na taslimu ni Sh milioni 265.1, hivyo wananchi kuombwa kuendelea kuwasilisha michango yao kwa ajili ya maadhimisho hayo.
POSTA kudhibiti dawa za kulevya.soma zaid

POSTA kudhibiti dawa za kulevya.soma zaid

KATIKA kupambana na uhalifu wa dawa za kulevya, Shirika la Posta Tanzania (TPC), linasimika mfumo wa kisasa utakaogharimu Sh. Milioni 200 wa kudhibiti usalama na kurahisisha utambuzi wa vitu na matukio hatarishi na haramu yanayopitishwa au kujitokeza kupitia mtandao wa shirika hilo. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo, Dk Haruni Kondo amesema leo alipokuwa akizungumza jijini Dar es Salaam. Dk Kondo alisema mfumo huo unajumuisha ufungaji wa kamera za kiusalama (CCTV), katika Posta Kuu ya Dar es Salaam, na tayari mzabuni aliyeusimika ameshakamilisha kazi yake na ataukabidhi kwa shirika wiki ijayo. Utazinduliwa rasmi wakati wowote kuanzia hapo. "Aidha tumesimika mifumo ya kisasa ya kiusalama ikiwa ni pamoja na mashine za ukaguzi wa mizigo katika ofisi zenye uwezekano wa kuwa uchochoro wa uhalifu wa aina hii ikiwa ni pamoja na ofisi za Zanzibar, Kigoma, Dar es Salaam na Arusha," amesema. Amesema hatua hizo zimechukuliwa na shirika ili kuhakikisha linashiriki na kuchangia kikamilifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kupambana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na usafirishaji, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, usafirishaji na utakatishaji wa fedha haramu, ugaidi, udaganyifu katika utambulisho pamoja na uhalifu mwingine wa kimtandao wa kitaifa na kimataifa. Mwenyekiti huyo alisema Bodi ya Wakurugenzi ya shirika imedhamiria kuongeza msukumo wa kasi ya usimamizi ili kupambana na uhalifu huo ambao una madhara makubwa kwa jamii. Amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa kuzingatia kuwa matukio ya uhalifu uliopangwa yamekuwa ni changamoto kubwa kwa mashirika ya Posta duniani. Ametaja vitu visivyoruhusiwa kusafirishwa katika mtandao wa Posta kwa mujibu wa sheria kuwa ni pamoja na dawa za kulevya, bidhaa za kemikali zenye sumu, silaha za moto na milipuko, wanyama hai, nyara za serikali, vifaa vya mionzi, vyakula vinavyooza, betri za aina mbalimbali, vimiminika, fedha haramu, utakatishaji wa fedha na vitu vyovyote hatarishi. Shirika hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usimamizi wa sheria, kwa hivi sasa limeimarisha uhakiki wa mifumo yake na pia ukaguzi wa barua, vifurushi, vipeto na mizigo ili kujiridhisha juu ya usalama na uzingatiaji wa sheria.

Friday, February 24, 2017
TCRA yaviadhibu vituo vinne vya utangazania.soma zaid

TCRA yaviadhibu vituo vinne vya utangazania.soma zaid

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu kali kwa vituo vinne vya utangazaji kwa kukiuka maadili ya utangazaji kwa mujibu wa sheria na kuvitaka viombe radhi siku tatu mfululizo kuanzia leo (Ijumaa) kupitia taarifa ya habari. Akitoa adhabu hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valerie Msoka amesema vitio hivyo vimepewa onyo kali ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na kuomba radhi wasikilizaji wake. Amevitaja vituo hivyo kuwa ni Star TV,Channel ten, Clouds FM na Times FM.chanzo muungwana blog

Thursday, February 23, 2017
Tetemeko la Ardhi la ukubwa wa 7.5 limekumba maeneo ya Ziwa Tanganyika.soma zaid

Tetemeko la Ardhi la ukubwa wa 7.5 limekumba maeneo ya Ziwa Tanganyika.soma zaid

Tetemeko la ardhi ya ukubwa wa 5.7 kwenye vipimo vya Richter limekumba maeneo ya Ziwa Tanganyika mapema Ijumaa. Tetemeko hilo lilitikisa maeneo ya kaskazini mwa Zambia na mitetemeko hiyo ikasikika maeneo ya kusini mashariki mwa Tanzania. Kitovu cha tetemeko hilo, kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani, kilikuwa kilomita 10 chini ya ardhi umbali wa kilomita 45 kutoka mji wa Kaputa nchini Zambia. Mji huo unapatikana katika mpaka wa nchi hiyo na Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na mbili usiku (0032 GMT). Tetemeko la ardhi la ukubwa kama huo huchukuliwa kuwa la kadiri lakini wataalamu wanasema kutokana na hali kwamba kitovu chake chakikuwa chini sana ndani ya ardhi, huenda hilo lilisababisha mitikisiko kuwa mikubwa. Desemba mwaka 2005, tetemeko kubwa la ardhi lilitokea eneo la Ziwa Tanganyika. Tetemeko hilo la nguvu ya 6.8 lilitikisa majumba katika miji maeneo ya Afrika mashariki na kati. Sehemu kubwa ya maeneo ya Afrika Mashariki huwa katika Bonde la Ufa, bonde kubwa lililoundwa kutokana na kuhama kwa maeneo makubwa ya ardhi na milipuko ya volkano. Hilo huyafanya kuwa hatarini ya kukumbwa na mitetemeko ya ardhi. Septemba mwaka 2016, tetemeko jingine la ardhi lililotokea eneo la Bukoba, mkoani Kagera kaskazini mwa Tanzania. Watu 16 walifariki na wengine 250 kujeruhiwa kutokana na tetemeko hilo. Mamia wengine walibaki bila makao. Tetemeko hilo la ukubwa wa 5.7 kwenye vipimo vya Richter, lilitajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kukumba taifa hilo la Afrika Mashariki katika kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja. Chanzo: BBC
Rais Magufuli amewapongeza Maktari wa muhimbili kwa kumtibu Neema Mwita.soma zaid

Rais Magufuli amewapongeza Maktari wa muhimbili kwa kumtibu Neema Mwita.soma zaid

Raisi Magufuli Atoapongezi kwa Madaktari Muhimbili Na Amsaidia Neema Mwita Wambura Aliyeunguzw Dada Neema Mwita Wambura (32) akizungunza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu akimshukuru kwa msaada aliompatia wa kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia Rais Dkt. Magufuli ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo pamoja na watoto wake watatu ambao kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpatia msaada Dada huyo kiasi cha Shilingi laki tano. Dada Neema Mwita Wambura aliungua vibaya mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa unachemka jikoni na mume wake katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapongeza Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa juhudi kubwa walizofanya kunusuru maisha ya Neema Mwita Wambura ambaye alijeruhiwa kwa kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi. Pongezi hizo za Mhe. Dkt. Magufuli zimetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Bw. Gerson Msigwa muda mfupi baada ya kumfikisha Neema Mwita Waitara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako Rais Magufuli ameagiza apelekwe kwa mara nyingine kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa maendeleo ya afya yake. Katika Pongezi hizo Mhe. Dkt. Magufuli amesema Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefanya kazi kubwa na ya kizalendo kuhakikisha Neema anapona licha ya majeraha makubwa aliyoyapata miaka miwili iliyopita na ambayo yalitishia uhai wake. Pia Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mama Mariam Amir (Bibi Mwanja) kwa upendo wake wa kumchukua Neema na kisha kumpa hifadhi nyumbani kwake huko Tandika Devis Kona Jijini Dar es Salaam. “Nakushukuru sana Mama na ninakupongeza, umeonesha mfano mzuri wa kujali umoja na upendo kwa Watanzania wenzako bila kujali dini, kabila wale kanda unayotoka na hivi ndivyo Watanzania wote tunapaswa kufanya” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Ulinzi mkali utaimalishwa dhidi ya mechi kati ya Simba na Yanga.soma zaid

Ulinzi mkali utaimalishwa dhidi ya mechi kati ya Simba na Yanga.soma zaid

Jeshi la Polisi yasema limejipanga kikamilifu
kuimarisha ulinzi na amani katika pambano la
watani wa jadi.
Homa ya pambano la watani wa jadi
litakalopigwa jumamosi imezidi kupanda huku
pande zote mbili zikitamba kuondoka na ushindi
na jeshi la polisi likijinasibu kuimarisha ulinzi.
Nelsoni Mandela Madiba alikuwa kinara wa
kuandika barua za mapenzi akiwa gerezani,rejea
barua yake ya april 27 iliyosheheni majonzi
kwenda kwa Winnie ikisema picha yako
naipangusa kila asubuhi ninashaka na hofu juu ya
kodi ya nyumba na hata chakula kwa watoto,siku
moja kablaya pambano la watani hawa nami
naadika barua ndefu kwenda kwa wanayanga
nikiwambia teke la mwisho la farasi anayekufa
huwa na nguvu na wasidaishwe na rangi
kwakuwa utamu wa chai sukari.
Tambo zimetamalaki kila pembe ya nchi wayanga
wakisema imma faima mnyama haponi simba
nao wajibu supu ya mawe i tayari kuwapa yanga
zaidi sana jeshi la Polisi nalo lasema litayari
kukabiliana na uhalifu.
Homa ya pambano la watani wa jadi
litakalopigwa jumamosi inazidi kupanda huku
pande zote mbili zikijigamba kuondoka na ushindi
wapo Dar es Salaam eneo la kigamboni,wacha
nikaskilize wimbo mtoto wacha kupiga mayowe.

Mbunge wa Longudo Onesmo Ole Nangole CHADEMA  ashida kesi ya uchaguzi.soma zaid

Mbunge wa Longudo Onesmo Ole Nangole CHADEMA ashida kesi ya uchaguzi.soma zaid

Mahakama ya Rufaa nchini imetupilia mbali rufaa ya kupinga hukumu ya kesi ya uchaguzi katika jimbo la Longido mkoani Arusha, yaliyompa ushindi Onesmo Ole Nangole (Chadema), iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Stephen Kiruswa, Uamuzi huo umesomwa leo (Alhamisi) na msajili wa Mahakama ya Rufaa nchini, Amir Msumi na kusema kwamba wakata rufaa waliwasilisha rufaa mpya badala ya kurekebisha baadhi ya vipengele kama walivyoagizwa na mahakama. Msumi amesema badala ya kuwajumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na msimamizi wa uchaguzi kwenye rufaa hiyo, wakata rufaa walifanya kitu ambacho hawakuruhusiwa kukifanya na mahakama na hivyo rufaa hiyo imetupwa na wanapaswa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.
Maneno ya Dayna Nyange kuhusu wasanii wa Bongo hawajui kutongoza yamemtoa povu Bill Nas.soma.zaid

Maneno ya Dayna Nyange kuhusu wasanii wa Bongo hawajui kutongoza yamemtoa povu Bill Nas.soma.zaid

Bill Nas ameijibu kauli ya Dayna Nyange kuwa mastaa wa Kibongo hawajui kutongoza. Dayna aliiambia Bongo5 kuwa hiyo ndio sababu moja wapo ya kwanini hana uhusiano na staa mwenzake. Lakini Bill ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo wa Dayna, Komela, ameipinga vikali kauli hiyo. “Hapaswi kujumuisha wasanii wote wa Bongo Flava, kama kuna washkaji wawili watatu wamewahi kumtongoza au watano, bado umma wa Bongo Flava ni mkubwa sana,” Bill Nas alikiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Jumatano hii. “Kama kuna watu wawili watatu, aseme hao hao asijumuishe watu wengine,” ameongeza rapper huyo na kudai kuwa kwakuwa yeye hajawahi kutoka na msichana wa Bongo Flava, hawezi kuhitimisha kuwa hakuna msichana anayemvutia. Awali kwenye interview ya Bongo5, Dayna alisema, “”Sijawahi kudate na staa na si kwamba wakaka wazuri hawapo, na sio kwamba hawanitokei, labda hawajui kutongoza vizuri. Kwa sababu sijawahi kushawishika kutembea na staa na sipendi kutembea na staa, so wakati mwingine unaweza ukawa haupendi kitu lakini ukashawishika kuingia lakini mimi bado hajatokea.”

Msanii Wema Sepetu anatalajia kujiunga rasimi CHADEMA hii leo.soma zaid

Msanii Wema Sepetu anatalajia kujiunga rasimi CHADEMA hii leo.soma zaid


CHADEMA kupitia Mwenyekiti wa Chama
Taifa Freeman Mbowe, baada ya kesi ya
kikatiba namba 1 ya mwaka 2017
inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama
Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia
waandishi wa habari na kuwakaribisha
wanachama wapya waliojiunga leo
akiwemo msanii Wema Sepetu.
Mbowe na Lissu leo wanawasilisha ile
hati ya mashitaka iliyorekebishwa na
kumuongeza Mwanasheria Mkuu. Wema
Sepetu yupo Katikati ya Esther Bulaya na
Mbowe hii leo. Kutoka Mahakama Kuu:
Kesi ya Mbowe dhidi ya RC Makonda, RPC
Sirro na ZCO Wambura
Baada ya hapa Mbowe ataongea na
Waandishi.
Ikumbukwe kwamba Lissu ambaye pia ni
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA)
na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, jana
alijitokeza mahakamani kuwa wakili wa
Wema na wenzake wawili akiwamo
mfanyakazi wa ndani. Msanii maarufu wa
fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu
anakabiliwa na kesi ya kukutwa na bangi.
Kesi hiyo ya Wema iliahirishwa hadi
Machi 15.

jeshi la polisi zanzibar linaendelea kuwahoji watuhumiwa 42 wa dawa za kulevya.soma zaid

jeshi la polisi zanzibar linaendelea kuwahoji watuhumiwa 42 wa dawa za kulevya.soma zaid

hatimae kuvuuka maji hadi viasiwani Zanzibar. Mkoa wa Mjini Magharib Unguja jeshi la polisi linaendelea na mahojiano na watuhumiwa 42 wa madawa ya kulevya na kuwafanyia upekuzi wa nyumba zao. Akizungumza na blog ya habrikwanza Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa wa mjini magharib Unguja Hassan Nassir Ali. Aliamesema wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao,ingawa hakua tayari kusema niniwamewakuta nacho na kuahidi taarifa rasmi itatolewa hapo badae. Alieleza kuwa jeshi hilo limeanza harakati hizo kufuatia kauli za Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Mh,John Pombe Maagufuli ambae ndie amriri jeshi mkuu wa Nchi katika kupambana na dawa za kulevya. ‘’Tunawaita na kuwahoji watuhumiwa na kisha kufanya upekuzi kwenye nyumba zao ingawa ni mapema kusema nini tumegundua’’alisema Afisa huyo wa juu wa polisi. Pamoja nahayo ameiasa jamii kutoa ushirikiano wa kina na jeshi hilo mara wanapogundua vitendo vya aina hio kwenye maeneo yao. Alieleza kuwa kuna tatizo kubwa linalotokana na jamii hususani wananchi wa Zanzibar kila mmoja kujifanya anajua licha ya kuwa sheria ipo na inaelekeza kila kitu kwenye maisha yetu. Aliasa jamii kuacha tabia ya kulihusisha jeshi hilo na rushwa na anapenda kuihakikishia jamii kuwa wanafanya kazi kwa weledi mkubwa . ‘’Kuna baadhi ya watu wamekuwa mstari wa mbele kulalamika watuhumiwa tunapowapa dhamani licha ya kuwa ni haki yao kisheria,jamii inapaswa kujua dhamana ni haki ya kila mtu inategemea na tuhuma wenyewe’’alifafanua zaidi Nassir. Akitolea ufafanuzi zaidi kamishna msaidi huyo aliesema mara watakapomaliza upelelezi wao na wale wote watakaogundulika na kuonekana na hatia watafikishwa mahakamani kusomewa kesi zao.
Wednesday, February 22, 2017
RC.Poul Makonda ameshindwa ashindwa kufika Chouds Fm.soma zaid

RC.Poul Makonda ameshindwa ashindwa kufika Chouds Fm.soma zaid

Jana Redio ya Clouds kupitia kipindi cha Power Breakfast walitangaza kuwa siku ya Leo Atakuja mkuu wa Mkoa Paul Makonda kutolea ufafanuzi mambo mbali mbali kuhusu yeye ambayo yamekuwa yakiongelewa na kushutumiwa bila yeye kutoa majibu. Sasa asubuhi ya Leo kipindi hicho kimeomba radhi kuwa Leo Mh Paul Makonda hata weza kuja kwenye kipindi hicho kutokana na majukumu ya kiserikali yanayomkabili siku ya leo

Hukumu ya kesi inayo mkabili wakurugenzi wa jamii forums imeahilishwa.sima zaid.

Hukumu ya kesi inayo mkabili wakurugenzi wa jamii forums imeahilishwa.sima zaid.

Upelelezi wa kesi ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi, inayomkabili Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Jamii Media Limited, Maxence Melo (40), umekamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 13 mwaka huu, baada ya upande wa mashitaka kuomba muda wa kujipanga zaidi ili kusoma maelezo ya awali ya mshitakiwa. Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mohammed Salum amedai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hilo umekamilika. Pia aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kujipanga kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali. Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 13 mwaka huu, kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali. Melo anakabiliwa na mashitaka manne katika mahakama hiyo kwa mahakimu watatu tofauti ambao ni Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa na Hakimu Mwambapa. Inadaiwa kuwa kati ya Aprili Mosi na Desemba 13, mwaka jana maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam, mshitakiwa akiwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo inayoendesha tovuti ya Jamii Forum, alishindwa kutoa taarifa kuhusu miliki hiyo huku akijua kwamba jeshi hilo linafanya uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyochapishwa kielektroniki kwenye tovuti hiyo. Pia inadaiwa mshitakiwa alizuia jeshi hilo kufanya uchunguzi kinyume na Sheria Namba 22 (2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao Namba 14 ya mwaka 2015. Salum amedai kuwa kati ya Mei 10 na Desemba 13 mwaka jana maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, akiwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, alilizuia jeshi hilo kufanya uchunguzi kwa kushindwa kutoa taarifa zilizochapishwa na tovuti hiyo. Aidha, katika kesi ya tatu, mshitakiwa alikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo la kuendesha mtandao kwa usajili usio wa Tanzania na kuzuia jeshi kufanya uchunguzi. Wakili Salum amedai kuwa, kati ya Desemba 9, 2011 na Desemba 13 mwaka jana, maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, akiwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo, alisajili tovuti ya Jamii Forum kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Alidai alifungua kampuni hiyo kwa Sheria ya Makampuni Namba 212 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kutumia cheti namba 66333. Aidha, ilidaiwa kati ya Januari 26 na Desemba 13 mwaka jana, maeneo ya Mikocheni akiwa Mkurugenzi wa Jamii Media inayoendesha mtandao wa jamiiforums huku akijua kwamba jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa makosa ya jinai, yaliyochapishwa kwenye mtandao huo, alizuia jeshi hilo kwa kushindwa kutoa taarifa.
IPTL kulipa Benki ya Standard Chartered Gong Konv Dola zamalekani 168,800,063.87.soma zaid

IPTL kulipa Benki ya Standard Chartered Gong Konv Dola zamalekani 168,800,063.87.soma zaid

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imeiamuru Kampuni ya Kufua Umeme IPTL kuilipa Benki ya Standard Chartered Hong Kong na Benki ya Standard Chartered Malaysia Dola za Marekani 168,800,063.87. Uamuzi huo ulitolewa na mahakama hiyo baada ya kukubali kuisajili hukumu iliyotolewa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara Uingereza ikiitaka kampuni hiyo kulipa fedha hizo. Jaji Baker Sehel alitoa uamuzi huo baada ya kuisajili hukumu hiyo hivi karibuni na kuamuru IPTL kulipa fedha hizo. Alisema walalamikiwa wanaweza kuwasilisha maombi ndani ya siku 21 ya kutaka usajili huo uwekwe pambeni na taarifa ya kusajili hukumu iwasilishwe kwa walamikiwa ikionyesha haitatekelezwa mpaka zipite siku 21. Novemba 16 mwaka jana, Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara Uingereza ilisikiliza kesi hiyo baada ya walalamikiwa kushindwa kuwasilisha utetezi wao. Walalamikaji katika kesi hiyo walikuwa Standard Chartered Bank Hong Kong Limited na Standard Chartered Bank Malaysia wakati walalamikiwa ni IPTL, VIP Engeneering and Marketing Limited na Pan Africa Power Limited. Katika shauri hilo walalamikiwa walishindwa kuwasilisha utetezi kwa madai kwamba mtambo wa IPTL na yote yanayohusu kampuni hiyo yako Tanzania na kwamba kabla ya kesi hiyo kuna kesi nyingine mbili nchini. Inadaiwa msingi wa kesi hizo ni kuhusu uhalali wa Standard Chartered Bank kuwa mdai halalali wa IPTL. Katika kesi moja, IPTL na PAP wanaidai Standard Chartered Bank Sh trilioni sita na ya pili, VIP wanaidai benki hiyo Sh trilioni moja. Pamoja na kuwasilisha pingamizi, mahakama ilitupilia mbali na kusikiliza kesi hiyo upande mmoja.
Monday, February 20, 2017
Soma Simulizi tamu ya Mapenzi mwanaume punguza tamaa.soma zeid.

Soma Simulizi tamu ya Mapenzi mwanaume punguza tamaa.soma zeid.

Mwanzoni sikumpenda kutoka moyoni, nilimpenda kwa kuwa tu alikuwa mrembo haswa..kwa kifupi nilimtamani tu….yaani nilitegemea akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu itaisha na nitaachana naye. Ndio ningeachana naye kwa sababusikuona umuhimu wa kudumu na msichana ambaye sijui hata kama nitamuoa. Nilipomwambia tutaoana hakika nilidanganya Alinipenda sana, kadri siku zilivyokwenda alizidisha upendo wake kwangu. Hakuna nilichohitaji kwake akaninyima, aliwahi kumdanganya baba yake kuwa anaumwa akatumiwa pesa ilimradi anipatie mimi nilipomwambia kuwa kuna mtu ananidai na abananisumbua kwelikweli. Alisikitika kusikia vile, akaahidi kunipigania. Haikuwa kweli nilichomwambia juu ya kudaiwa, pesa ile aliyonipa niliitumia kulipia chumba nikafanya uzinzi na Fatuma. Alihadithiwa habari hiyo na marafiki walioniona nikiingia kule, akalia kwa uchungu mbele yangu, lakini neno lake la mwisho likabaki kuwa ‘NAKUPENDA SANA…..WEWE NI MWANAUME WA MAISHA YANGU’……..Nilij isikia vibaya lakini nafsi nyingine ikanikumbusha kuwa nilikuwa katika mahusiano na msichana yule kwa sababu moja tu…NGONO… na katu hakutaka kushiriki ngono na mimi. Alinikwepa sana hadi nikajisikia vibaya. Nikahisi huenda ana mtu mwingine. Hakika nilidhani kuwa anajihusisha na mtu mwingine ambaye hushiriki naye tendo hilo la ngono ambalo kwangu mimi kilikuwa kitu pekee ambacho kingeweza kuniaminisha kuwa ananipenda kweli. Msichana mrembo kama huyo kamwe asingeweza kuishi bila kufanya mapenzi. Hakika haikuniingia akilini. Wangapi wenye ,ali zao wanamtongoza, yeye ni nani hadi asiingie majaribuni?? Hapana ni uongo mtupu ananiongopea mimi. Nikaendelea na vimbwanga vya hapa na pale. Hakuchoka kunibembeleza, hakuchoka kunipenda na hakuchoka kunikumbusha kuwa ni mimi pekee nilikuwa katika moyo wake wa nyama. “Nikipotea jumla nd’o utajua kuwa nilikuwa nakupenda..” aliwahi kunambia neno hilo. Japo lilinigusa lakini sikulitilia maanani. Hatimaye tukamaliza shule, nikategemea kuwa ule muda wa kumfaidi msichana yule kingono ulikuwa umewadia. Lakini haikuwa hivyo, akaendelea kuwa mgumu huku akijitetea kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu. Mwanzoni nilidhani kuwa aliogopa kufanya mapenzi kabla hajamaliza shule, lakini ajabu hadi tulipomaliza bado alisimamia msimamo. Sasa nikajikuta katika pepo mbaya, nikaanza kumwonyesha hadharani kuwa nina wanawake wengine. Japo chozi lake liliniumiza sana lakini sikujali. Kwa nini ananinyima penzi binti huyu? Nilijiuliza. Hatimaye nikafikia uamuzi wa kuachana naye. Lakini siwezi kuachana naye bila kumjua ladha yake. Nilijiapia kuwa jambo hilo haliwezekani hata kidogo, mimi kama mwanaume kamili atanitangazaje kwa marafiki zke, kuwa sijawahi kulala naye tukafanya tendo??? Aibu kubwa!!! Nikampangia shambulizi moja la mwisho na kama ni ubaya uwe ubaya tu. Ilimradi nilishapanga kuachana naye….haitanidh uru lakini lazima nifanye naye tendo Nilimuita nyumbani kwangu, ilikuwa mida ya jioni. Alipofika nilimlaghai hapa na pale nikamgusa matiti yake madogo yaliyosimama wima yakijitahidi kunidhihaki. Na yalifanikiwa hasa hasa kunikebehi. Nikamgusa huku na kule..nilipotak a kumvua nguo akanizuia. Nilikuwa nimekunywa pombe kiasi hivyo sikuwa na aibu, nikaamua kutumia nguvu, niliamua KUMBAKA…..nikai chana sidiria yake, kisha nikaiondoa chupi yake sasa akabaki yu uchi wa mnyama. Alihaha huku na kule asiamini kile kinachotokea mbele yake. Nikamrukia ili niweze kutimiza lengo… Kamwe sikuwahi kumwona binti huyu akiwa katika uoga namna ile…alikuwa amekodoa macho yake….na alikuwa anatetemeka… Akataka kukimbia uchi, nikamdaka mkono nikamvutia pale nilipokuwa. Sikuwa nahuruma hata kidogo, nilichotaka ni itu kimoja tu..NGONO KISHA AKINICHUKIA NA ACHUKIE. Mara akatokwa na kelele kubwa sana zilizonishtua sana. Amakweli sikuzitegemea. Sikudhani kama amnaweza kufanya tendo lile “ANANIBAKAAAAA, NISAIDIEENI ANANIBAAAKA…..” ilikuwa kelele kubwa haswa, na alifanya kwa kurudia rudia Kelele zikawafikia wasamalia wema, binti akaendelea kupiga kelele. Hatimaye mlango ukavunjwa, wasamaria wakanivagaa na kuanza kunipiga……nilip igwa hadi nikapoteza fahamu. Nilipozinduka nilijikuta na pingu mkononi, pingu iliyounganishwa na kitanda. Nilikuwa na maumivu makali mwili mzima. Nikakumbuka kuwa nilifumaniwa nikitaka kufanya ubakaji. Pombe zilikuwa zimenitoka na niliona aibu wa kitendo cha kinyama nilichotaka kumfanyia Maria. Baada ya kujitambua vyema na nguvu kunrejea mwilini nilirejeshwa mahabusu. Nikaingia mahabusu nikikabiliwa na kesi mbaya ya ubakaji. SIKU NNE baadaye nilikuja kutolewa……hapak uwa na dhamana lakini ilikuwa barua tu ya kustaajabisha niliyokutana nayo. “Mpenzi Christopher mwanaume wa maisha yangu…..haikuwa nia yangu kukusababishia kipigo kikali na kuitwa mbakaji… nimefan ya haya kwa sababu nakupenda kutoka moyoni…napenda uishi miaka mingi..Chriss ni wewe mwanaume pekee niliyetokea kuvutiwa naye kihisia ukauteka moyo wangu na kujikuta nikiwa mtumwa wa mahaba yako… lakini nina mapungufu makubwa…nina kasoro kubwa ambayo hainipi hadhi ya kulala kitanda kimoja na wewe…..Chriss mimi ningekuwa muuaji iwapo ningekuruhusu unibake….hivi chriss unadhani mpapaso wako haukunisisimua? Nilisisimka haswa na nilitamani nikutimizie kwa hiari kile ulichotaka, labda mimi nilikuwa muhitaji kuliko wewe mpenzi lakini…..lakini nisingeweza kukuua, ….Chriss ninayo furaha na wala usisikitike kusikia hili, mimi nimefurahi sana kufa nikiupigania uhai wa mwanaume niliyempenda, ninayempenda na ninayekufa kwa ajili yake. Kitanzi hiki kiwe kumbukumbu yako milele kuwa NILIKUPENDA…….C hriss mimi ni muathirika wa gonjwa la UKIMWI niliambukizwa na wazzi wangu …nilizaliwa nikiwa na Ukimwi Chriss, mama kabla ya kufa alinikanya kuwa nisiwe na tabia kama ya marehemu baba ambaye alimuambukiza maksudi kutokana na taba yake ya kutotulia nyumbani, mama akanikanya kuwa ni heri nife peke yangu kuliko kuua yeyote asiyekuwa na hatia. Na huyo mtu ni wewe Chriss haukuwa na hatia na haukustahili kufa..…..laiti kama ungenibaka basi leo hii ningekufa nikiwa MUUAJI… ninafura hi kuwa nakufa kama SHUJAA. Nimeyaadika haya huku kitanzi kikiwa shingoni mwangu, nakufa leo lakini wakuache wewe huru. Huru kabisa, naenda kuungana na mama yangu nimweleze kuwa sikuwahi kuua duniani na nimeamua kuondoka ili siku moja nisije kuua yeyote. Ubaki salama Chris wangu” Nilijikuta napoteza fahamu tena baada ya kuhakikishiwa kuwa Maria alizikwa baada ya kujinyonga katika chumba chake nyumbani kwao nabaruaile ilikutwa chini ya miguu yake iliyokuwa unaning’inia……. nilipozinduka nilikuwa nyumbani kwetu…kila jicho lilinitazama kwa namna yake……wengine kwa hasira wengine dharau na baadhi kwa huzuni. AMA KWA HAKIKA nilikuwa na mpenzi aliyenipenda kwa dhati……. UPUMZIKE PEMA PEPONI Maria…..kamwe sitakusahau mpenzi……. UJUMBE; Usilipize baya kwa baya kwa kizazi kisichokuwa na hatia…..JIFUNZE kupenda kwa dhati lakini HISIA ZAKO ZISIKUFANYE MTUMWA!!!!
Hivi inawezekana masikini akaogota fedha ya tajili na kumludishia?soma kisa hichi.

Hivi inawezekana masikini akaogota fedha ya tajili na kumludishia?soma kisa hichi.

Kuna siku nilikuwa maeneo ya Mjini kati (City Center), nikaipenda suruali moja ya shilingi 15,000/= na pesa sikuwa nayo ikabidi niende kutoa kwenye ATM ya Postal. Nimefika pale sikukuta mtu hivyo niliingia moja kwa moja, nimefika mle ndani nikakuta Pesa Kibao zimemwagika pale kwenye kitundu cha kutolea pesa, ATM Card ilikuwepo pale imetokezea na Pembeni kulikuwa na Pochi ya Kike iliyoonekana kutuna vilivyo. Kwa woga mimi huku nikitetemeka mapigo ya moyo yakiwa yameongezeka nikatizama nyuma yangu sikuona mtu, nikachukua zile Pesa harakaharaka, ATM na ile pochi. Ile natoka nje kuna dada mmoja alikuwa anakuja kwa kasi maeneo yale nikapata uoga nikamuuliza “Samahani dada, kuna kitu umesahau humu”, yule dada hakunijibu kitu kaingia kwenye chumba cha ATM akachomeka Kadi kutoa hela mi nikaondoka zangu fasta kuelekea home. Nimefika home nikajifungia ndani na kuzibwaga zile pesa kitandani, nikafungua wallet nikakuta imejaa dollar, Vipodozi, iphone na ki-Nokia kidogo cha tochi, ATM Card mbili za Benki tofauti ambazo zilikuwa zimezungushiwa karatasi iliyokuwa na namba za siri za ATM zote, moyo ukanilipuka paaaa!!! Nikaona bora Nipumzike kwanza kitandani!! Muda si mrefu ile iphone ikaanza kuita, nilipoangalia halikutokea jina nikaona bora nipokee nimsikilize anasemaje, ilikuwa sauti ya kike iliyoongea kwa huzuni kwa kubembeleza huku akilia na alijitambulisha vizuri kuwa ile mali ni ya kwake! Huruma ilinijia nikamwelekeza nilipo aje kuchukua... Hakuchukua muda akawa amefika nami nikamkabidhi vitu vyote naye akavihakiki na kukuta viko sana: Milioni 3 za Kibongo na Dollar 500. Dada kanishukuru na kunipa ile Millioni 3 ya kibongo mi nikazikataa kwasababu ni mali yake na alizisahau tu. Alinitoa hofu kwa kunisihi nichukue tu, mi kama binadamu mwenyezi Mungu atanilipa, nikakataa... Mwishowe akaomba namba yangu na kuondoka zake, akawa ameniacha ndani huku njaa sasa nikaanza kuisikia, nilikuwa na buku mbili nikaenda kula viepe kavu na soda nikawa powa. Sasa jana kanipigia simu kuwa anakuja nimsubiri, dakika tano tu akanipigia tena kuwa ameshafika yupo nje yupo ndani ya Prado mpyaa nikaingia tukaondoka akaenda kunionyesha kwake kisha tukaelekea kwenye nyumba nyingine iliyokuwa ndo imekamilika kujengwa akaniambia hii itakuwa yako akanikabidhi baadhi ya nyaraka na funguo zote sikuamini...!! Akanisindikiza kwangu, kufika home ananiambia hiyo gari (Prado) nayo ananiachia ni kwa mema tu niliyomfanyia, ndani ya ile gari kulikuwa na brifcase iliyokuwa na pesa akaniambia pia hii pesa itakuwa yako ya kuanzia maisha, na kumbe yule dada alikuwa kanipenda akanikumbatia kwa nguvu nikiwa pale kwenye seat oooh!! umasikini baibai... Akiwa kanikumbatia akihema kwa kasi juu ya kifua changu nikahisi mtu akinishika begani na kuniita kwa sauti. “Anko ankoo we ankoo... amka rafiki yako Salim anakuita!!!”. “ALIKUWA MTOTO WA SISTA ALIKUWA ANANIAMSHA !!”. Kumbe muda wote nilikuwa nikiota Dah...!!
Watu 66 watiwa mbaroni kwa tuhuma ya madawa ya kulevya.soma zaid

Watu 66 watiwa mbaroni kwa tuhuma ya madawa ya kulevya.soma zaid

Taarifa ya 66 walionaswa na Dawa za kulevya Morogoro http://www.muungwana.co.tz/2017/02/taarifa-ya-66-walionaswa-na-dawa-za.html Watu wanne wamefariki na saba wameokolewa
baada ya kufukiwa na kifusi wakat wanachimba
dhahabu katika machimbo yaliyopo Kijiji cha
Itumbi, Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.

Maafa mgodini watu 4 wamefariki na 7 wameokolewa.soma zaid

Maafa mgodini watu 4 wamefariki na 7 wameokolewa.soma zaid

Watu wanne wamefariki na saba wameokolewa
baada ya kufukiwa na kifusi wakat wanachimba
dhahabu katika machimbo yaliyopo Kijiji cha
Itumbi, Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.chanzo mwananch

Zitto ziarani nchini Kenya kukagua miradi ya( IMF)soma zaid

Zitto ziarani nchini Kenya kukagua miradi ya( IMF)soma zaid


Zitto Ziarani Nchini Kenya
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto yupo nchini Kenya kwa
ziara ya ukaguzi wa miradi ya Benki ya Dunia na
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Ziara hii ni
sehemu ya kazi za Mtandao wa Wabunge wa
Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia
(WB). Katika ziara hii kuna jumla ya wabunge 25
kutoka nchi mbalimbali duniani. Tanzania
inawakilishwa na Mbunge wa Kigoma Mjini na
Mbunge wa Sikonge ndugu Joseph Kakunda.
Katika ziara hiyo wabunge wanakagua miradi
mbali mbali inayotekelezwa na mashirika hayo na
namna gani miradi hiyo inachochea maendeleo
ya nchi husika. Benki ya Dunia Ina miradi ya
thamani ya USD 2.3 bilioni (sawa na wastani wa
Shilingi Trilioni 5) nchini Kenya. Wabunge
watakutana na Asasi za kiraia na sekta binafsi ya
Kenya. Upande wa Serikali watakutana na Waziri
wa Fedha, Gavana wa Benki Kuu na tume ya
mipango.
Asubuhi ya Leo ndugu Zitto alimtembelea
bungeni Spika wa Bunge la Kenya, Mheshimiwa
Justin Bedan Njoka Muturi. Pichani akiwa pamoja
na Spika Muturi (katikati) pamoja na Mbunge wa
Bunge la Uganda, mheshimiwa Nandala Nandala -
Mafabi (kulia) ambaye pia ni Katibu Mkuu wa
Chama cha Forum for Democratic Change (FDC)
cha Uganda kinachoongozwa na ndugu Kizza
Besigye. Mafabi naye ni mjumbe wa Mtandao wa
Wabunge wa IMF na Benki ya Dunia (WB).
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu
Zitto, ni mwanachama mwandamizi wa Mtandao
wa Wabunge wa IMF na Benki ya Dunia (WB)
kwa muda wa miaka 8 Sasa.
Imetolewa na Ofisi ya Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
Februari 20, 2017

Tuesday, February 7, 2017
Simulizi ya ERIC SHIGONDO DIMBWI LADAMU sehemu ya 15.soma zaid

Simulizi ya ERIC SHIGONDO DIMBWI LADAMU sehemu ya 15.soma zaid


ERIC SHIGONGO
DIMBWI LA DAMU-15
Tayari Manjit alishaingia �mikononi mwa polisi
na �alikuwa ndani ya gari akipelekwa kituoni,
hiyo ilitokea baada ya kumweleza Patrick ukweli
kuwa asingeweza kumlipa pesa alizokuwa
akimdai,Victoria aliumia sana moyoni mwake
wakati Manjit akiondolewa ndani ya ofisi ya
Patrick huku akiliita jina lake, alishindwa
angemsaidia vipi Manjit mtu pekee aliyekuwa
akimtegemea kwa wakati huo.
Walitoka ofisini Patrick akiwa amemshika mkono
Victoria na kumuongoza hadi mahali lilipokuwa
gari lake la kifahari aina ya Potsche, na kuingia
ndani, Patrick alikaa kwenye usukani na Victoria
alikaa kushoto kwake, ilikuwa ni safari kwenda
nyumbani kwa tajiri Abdulwakil ambako Victoria
alikuwa akipelekwa kuongea na tajiri huyo
aliyemiliki visima vingi vya mafuta ili ajaribu
kumshawishi asimfunge Manjit kwani ndiye
alikuwa tegemeo lake maishani.
“Akiniona katika hali hii ya upofu ni lazima
atabadili nia yake ya kumfunga Manjit, Mungu
yupo pamoja na mimi ninaamini atanihurumia!”
Aliwaza Victoria wakati gari likipita kwenye mitaa
ya katikati ya jiji la Baghdad kuelekea nyumbani
kwa tajiri Abdulwakil kilometa kumi na tano nje
ya jiji.
“Hivi baba yangu atakubali kweli? Sina uhakika
anachotaka yeye ni pesa na kama hakuna pesa
lazima Manjit atafungwa tu!”
“Mwanangu niache nikaongee naye akikataa basi
lakini nitakuwa nimejaribu!”
“Sawa mama!”
Gari lilizidi kwenda kwa kasi na dakika kumi na
tano baadaye liliacha barabara na kukata kona
kuingia kulia likipita chini ya miti mirefu, mbele
zaidi kama nusu kilometa lilikata tena kushoto na
kuzidi kutokomea ndani! Hatua kama mia mbili
mbele Victoria alisikia honi ikipigwa na mlio wa
geti likifunguliwa ulisikika, akafahamu walikuwa
wamefika mahali walipokuwa wakienda.
“Asalam alekum!”
“Aleikum salam!”
Alisikia maneno hayo kila walivyozidi kusonga
mbele hatimaye gari likasimama kabisa na
Patrick alifungua mlango na kuzunguka hadi
upande wa pili ambako pia alifungua mlango na
kumsaidia Victoria kushuka.
“Tumefika!”
“Kumbe sio mbali?”
“Kwa kweli sio mbali sana!”
Patrick akiwa amemshika mkono Victoria
waliongozana na kuanza kupandisha ngazi
taratibu, aligundua walikuwa wakiingia ndani ya
nyumba, kila mahali walikopita salamu zilisikika
na milango ilifunguliwa na wakaingia hadi ndani
ambako Victoria alisaidiwa kuketi kitini.
“Karibu mama hapa ndio nyumbani kwetu!”
“Ahsante sana mwanangu, kikubwa naomba
unisaidie nikutane na baba yako!”
“Basi nisubiri hapa nikaongee naye” Alisema
Patrick, alionekana kumwonea huruma sana
Victoria lakini hakuwa na uwezo wa kumsaidia
kwa sababu mwenye amri alikuwa ni baba yake
mzazi.
“Haina matatizo!” Aliitikia Victoria na baadaye
akasikia mlio wa viatu ukiondoka mahali alipokaa.
Alisubiri kwa muda mrefu mno bila Patrick
kurejea, alishindwa kuelewa ni kitu gani
kilichokuwa kikiongelewa huko ndani! Hofu yake
kubwa ilikuwa ni tajiri Abdulwakil kukataa
kuonana naye alimwomba Mungu wake hilo
lisitokee. Mawazo yake yote wakati akisubiri
yalikuwa juu ya Manjit ambaye alikuwa polisi,
hakujua ni kitu gani wangekuwa wamemtenda!
Alizidi kumwomba Mungu amwepushe Manjit na
mabaya yote, hakuwa tayari kushuhudia Manjit
akipatwa na tatizo kwani maisha bila yeye
yasingewezekana, alikuwa tayari kufa pamoja
naye.
Baadaye akiwa sebuleni alianza kusikia
minong’ono kutoka upande wa pili, ilikuwa ni
sauti nzito ya kizee ikifoka! Hakuelewa ni nini
kilichokuwa kikiongelewa kwa sababu maongezi
yalifanyika katika lugha ya Kiarabu.
Kadri dakika zilivyozidi kwenda ndivyo sauti ya
mzee akifoka ilivyozidi kuongezeka na kukikaribia
chumba alichokuwa amekaa, hofu kubwa ilimpata
moyoni mwake akijua kitu kibaya kilikuwa
kikimfuata! Alianza kulia akimwomba Mungu
abadilishe mawazo ya wabaya wake.
“Ee Mungu wangu naomba unisai........!” Alisema
Victoria lakini kabla hajaimalizia sentensi yake
mlango ulifunguliwa na nyayo za watu wengi
zilisikika zikiingia, alikaa kimya akisubiri sauti ya
Patrick iongee lakini badala yake alisikia sauti
nzito ya mzee ikifoka.
“Yuko wapi huyo? Hawa watu wanafikiri sisi
tunafanya mchezo na biashara, ikibidi hata huyu
mama tutamfunga pamoja na Manjit!” Alifoka
mzee huyo, sauti yake pekee ilitosha kumtisha
Victoria.
Victoria aliposikia kauli hiyo aliinamisha kichwa
chake na kuuficha uso wake katikati ya miguu
yake miwili, kwa maneno yaliyosemwa na mzee
huyo alijua taabu kubwa ilikuwa inakuja! Aliumia
sana moyoni mwake, alifikiri shida zilikuwa
zimekwisha katika maisha yake kumbe haikuwa
hivyo alitakiwa kupambana na matatizo mengine
tena.
“Hebu mleteni hapa!” Aliamrisha mzee huyo na
Victoria alibebwa juujuu na kupelekwa moja kwa
moja hadi mahali mzee huyo alipokaa.
“Nisamehe sana mzee, naomba unisikilize
kwanza ninachotaka kusema!”
“Onyesha uso wako kwanini unaficha sura? Hebu
mnyanyueni sura yake niione ingawa ukitaka
kumuua nyani usimwangalie usoni!” Alisema tajiri
Abdulwakil na vijana kama watatu walimshika
Victoria shingoni na kuanza kukinyanyua kichwa
chake.
“Khaa! Victoria ni wewe?” Tajiri Abdulwakil
alisikika akipiga kelele.
Victoria alishangaa kusikia mtu aliyemhofia
akimwita kwa jina, hakuwa maarufu kiasi cha
kujulikana kwa tajiri Abdulwakil!
“Wewe ni nani unayeniita jina?”
Tajiri Abdulwakil hakujibu kitu kwa mshtuko
alioupata alilegea na kuanguka moja kwa moja
sakafuni! Ikawa hekaheka ndani ya chumba, watu
wote hawakuelewa ni nini kimempata ikabidi kwa
haraka haraka abebwe na kutolewa moja kwa
moja hadi nje ambako alipakiwa ndani ya gari na
kukimbizwa hospitali! Hakuna mtu aliyeelewa
kilichotokea, kilibaki ni kitendawili.
“Au yule bibi ni mchawi nini?” Aliuliza Patrick
wakiwa ndani ya gari kuelekea hospitali.
“Kwanini unafikiri hivyo Patrick?”
“Maana amening’ang’ania sana nimlete kwa baba
sasa baada tu ya baba kumwona ameanguka na
kupoteza fahamu. Kama baba akifa kwa hakika
nitamuua huyu bibi kizee! Hawezi kuniulia baba
yangu hivi hivi nikamwacha hai” Aliendelea
kusema Patrick huku machozi yakimtoka.
Walipofika hospitali walipokelewa na tajiri
Abdulwakil akiwa hajitambui alikimbizwa moja
kwa moja hadi chumba cha wagonjwa mahututi,
iligundulika baadaye kuwa mmoja wa mishipa
yake katika ubongo ulipasuka sababu ya mshtuko
mkubwa alioupata. Jambo hilo lilimfanya Patrick
aamini Victoria alikuwa na majini na alimpiga
baba yake na moja ya majini yake.
“Nitamuua! Hakyanani nitamuua! Nikirudi
nyumbani tu lazima afe na atafukiwa ardhini
hakuna mtu atakayejua”
**************
Kwa sababu ya kuchanganyikiwa na tukio
lililotokea Patrick alimsahau Victoria ndani ya
nyumba yao na kuondoka mbio kwenda hospitali,
alibaki sebuleni akiwa katika dimbwi la mawazo
na maswali yasiyokuwa na majibu, alishindwa
kuelewa ni nani aliyemwita kwa jina, aliamini
hapakuwa na mtu yeyote aliyemfahamu katika
nchi ya Iran.
Alivuta kumbukumbu zake kwa muda akijaribu
angalau kuikumbuka sauti aliyoisikia lakini
hakupata jibu na kilichomchanganya zaidi ni
kitendo cha kumsikia Patrick akimtupia lawama
juu ya matatizo yaliyompata baba yake! Aliogopa
na kuamini lazima Patrick angemfanyia kitu.
Ni wasiwasi huo ndio uliomfanya atoke taratibu
sebuleni na kutembea hadi nje akishika ukuta,
nyumba nzima ilikuwa kimya iliashiria watu wote
hawakuwepo, aliamini wote walimkimbiza tajiri
Abdulwakil hospitali.
Nyumba ya tajiri Abdulwakil ililindwa kila upande,
ilikuwa si rahisi kutoka wala kuingia ndani ya
nyumba hiyo bila kuonekana lakini kwa tukio
lililotokea siku hiyo, walinzi wote walikusanyika
sehemu moja na kuanza kujadili juu ya
kilichompata tajiri wao.
“Sijui kapatwa na nini?”
“Hata mimi sifahamu, nimeona tu akitolewa ndani
na kupakiwa ndani ya gari na kwa haraka gari
likaanza kuondoka!”
“Labda mama yumo ndani tumuulize?”
“Hata yeye hayupo amekwenda hospitali!”
“Atapona kweli mzee?”
“Kwa hali niliyomwona nayo kwa kweli nina
wasiwasi!”
Wakati maongezi hayo yakiendelea Victoria
alikuwa akiupapasa ukuta kwa kuuzunguka
akitafuta mahali pa kutokea, alikuwa ameamua
kutoroka kwenda mahali kusikojulikana, mwili
wake ulihisi mabaya! Alijua kama Patrick
angerudi kutoka hospitali na kumkuta ni lazima
angemdhuru na hata kumuua kabisa, Victoria
hakuwa tayari kwa hilo.
Alipapasa kwa dakika ishirini nzima ndipo
akafanikiwa kulifikia lango, kubwa lilikuwa
limefungwa lakini alipopapasa pembeni
alifanikiwa kugusa kitu kama komeo, alipokishika
na kujaribu kukifungua na kisha kuvuta
alishangaa kuona lango dogo likifunguka!
Akamshukuru Mungu na kwa taratibu pamoja na
uzee wake alinyata na kutoka nje bila kuonekana
na mtu yeyote.
Sababu ya upofu alisimama bila kujua aelekee
wapi, aliusikiliza moyo wake kwa muda na
akakumbuka maneno aliyoambiwa kanisani miaka
mingi akiwa mtoto mdogo kuwa Mkono wa kulia
ulikuwa mkono wa Kuume ambao uliaminika
kuwa na baraka! Bila hata kujadili mara mbili
Victoria alikata kulia akachuchuma na kuanza
kutambaa akielekea vichakani bila kujua mahali
alikokuwa akielekea.
Kwa saa nzima alitambaa ardhini akipita katikati
ya nyasi zilizomuwasha mwili mzima, hakujali
kwa sababu alishaamua kujiokoa, machozi
yaliendelea kumtoka sababu ya Manjit aliyekuwa
polisi! Kwa mara nyingine alikuwa
ametenganishwa na mtu aliyempenda na
aliyekuwa msaada pekee kwake!Kumbukumbu
zake zilimrejesha tena kwa kaka yake Nicholaus.
“Yaani kila mtu anayejitolea kunisaidia
anaondolewa kwangu! Wa kwanza alikuwa
Nicholaus, akaja Leah, baadaye Manjit lakini hata
yeye wameninyang’anya! Nitaishije mimi
Victoria? Ni heri kufa kuliko mateso haya!”
Aliwaza akizidi kutambaa kwenda mbele zaidi
katikati ya vichaka.
Mpaka masaa matatu baadaye alikuwa bado
akitambaa porini, alikuwa bado hajaonekana wala
kukutana na mtu yeyote! Alimshukuru Mungu
kwa hilo mbele zaidi alichoka na kuamua kulala
chali ardhini na kuamua kuifungua ncha moja ya
nguo aliyojifunga na kutoa kipande cha noti
walichogawana na kaka yake, alikuwa bado
akikitunza! Hakuwa tayari kukipoteza kwake
ilikuwa ni bora apotee yeye lakini si kipande
hicho cha noti alichokichukulia kama kaka yake.
“Hivi kweli ipo siku nitakutana na Nicholaus na
kuiunganisha noti yetu?” Aliwaza Victoria akiwa
amelala chali ardhini, alikuwa amechoka hoi bin
taaban na njaa ilimsumbua, si njaa tu kulikuwa
na mbu wengi waliomuuma kila sehemu ya mwili
wake, ingawa alikuwa kipofu hali ilimuonyesha
kuwa tayari usiku ulishaingia.
Hakuwa na matumaini ya kumwona Manjit tena!
*************
Taarifa za tajiri Abdulwakil kuanguka ghafla
nyumbani kwake baada ya kumwona mwanamke
mzee zilitapakaa kila sehemu ya mji wa
Baghdad! Watu wengi walifurika hospitali
kushuhudia kilichompata mtu waliyeamini alikuwa
tajiri kuliko wote nchini humo.
“Ni jini!”
“Kweli eh?”
“Hakuna kitu kingine! Si ajabu maadui zake
walimtuma bibi kizee nyumbani kwake wakiwa
wamemvalisha jini chinjachinja!”
“Lakini kweli inawezekana!”
Hayo ndiyo yalikuwa maneno ya kila mtu aliyefika
hospitali, hawakuruhusiwa kumwona mgonjwa
watu wote waliongea na Patrick na kumpa pole
na alivyowasimulia yaliyotokea wote waliamini
bibi alitumwa.
“Huyo bibi yuko wapi?” Aliuliza mmoja wa
wafanyakazi kwenye visima vilivyomilikiwa na
tajiri Abdulwakil.
“Tulimwacha nyumbani!”
“Kwa hiyo atakuwa bado yuko nyumbani kwenu?”
“Naamini hivyo!”
“Jamaniee!” Alipiga kelele mfanyakazi huyo na
wafanyakazi zaidi ya mia tatu waliokusanyika
walikaa kimya kumsikiliza yeye, alikuwa ni
kiongozi wao katika visima vya mafuta.
“Ni lazima huyu bibi tukamuue, hawezi
kumuumiza tajiri yetu na ushirikina au
mnasemaje?”
“Sawaaaaaaaaa!”Wafanyakazi wote waliitikia.
Kama walioamrishwa waliingia ndani ya magari
yaliyokuja nayo kutoka kwenye visima vya mafuta
na kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa
tajiri Abdulwakil kwa lengo la kwenda kumkamata
Victoria na kumuulia mbali. Walipokelewa na
walinzi na walipomuulizia bibi walinzi hawakuwa
na jibu kwa sababu hawakutaarifiwa kuwa
kulikuwa na mtu aliyebaki ndani ya nyumba!
“Ingieni muangalie!”
Kiongozi wa wafanyakazi hao na wenzake wawili
waliingia hadi sebuleni na kuanza kumsaka
Victoria bila mafanikio, walinyanyua hadi viti na
meza na kumwangalia chini yake lakini bado
hakupatikana.
Walitoka nje na kuwataarifu wenzao juu ya
kutoonekana kwa mtu waliyekuwa wakimtafuta
ndani ya nyumba, waliamua kuacha ili wafanye
msako asubuhi iliyofuata, baadaye Patrick alirudi
kutoka hospitali na kuungana nao! Yeye ndiye
aliwajaza jazba zaidi wafanyakazi wake pale
alipowaeleza wazi kuwa mwanamke
aliyemsababisha baba yake matatizo alistahili
kufa.
Wafanyakazi walilala nje ya nyumba ya akina
Patrick na asubuhi ilipowadia, nyumba nzima kwa
msaada wa Patrick ilianza kupekuliwa lakini
mpaka hatua ya mwisho hawakuweza kumwona
ndipo ukatolewa uamuzi watafutwe nje ya
ngome.
“Hatakuwa mbali na hapa, si ajabu alifanikiwa
kutoka na yupo porini!” Patrick aliwaeleza
wafanyakazi wake, alikuwa amedhamiria kumuua
Victoria kabisa akiamini alimpiga baba yake na
jini! Hakuna mtu kati yao aliyeelewa kwanini
Abdulwakil alipoteza fahamu mara tu baada ya
kumwona mwanamke huyo na kilichowashangaza
zaidi ni kitendo cha Abdulwakil kumtaja
mwanamke huyo kwa jina kabla ya kupoteza
fahamu.
“Jamani hizi ni nyayo za nani? Lazima kuna kitu
kimepita hapa kikijivuta!” Alipiga kelele mmoja
wa wafanyakazi waliokuwa wakimsaka Victoria.
Mchana kabla Victoria hajapelekwa nyumbani
kwa tajiri Abdulwakil mvua kubwa sana ilinyesha
ni hiyo ndiyo iliyofanya nyayo na alama za
Victoria akitambaa ardhini zionekane.
“Ni yeye ndiye kapita hapa!”Patrick alisema na
kuwaongoza wafanyakazi wake kuzifuata nyayo
hizo porini,walitembea karibu masaa mawili
wakizifuata nyayo hizo porini, ghafla walimsikia
mtu aliyekuwa mbele yao akipiga kelele kwa
sauti.
“Huyu hapa! Huyu hapa!” Wafanyakazi wote
walikimbia kwenda mbele kila mtu na silaha
yake, mwenye rungu, mwenye jiwe, mwenye
panga, mwenye nondo tayari kwa kumuua
Victoria.
Alikuwa usingizini lakini kelele hizo zilimzindua
alishindwa kuelewa ni akina nani waliokuwa
wamemzunguka.
Je, nini kitaendelea?
Tukutane kesho hapahapa

Waandishi wa habari wakamatwa wilayani Arumeru mkoani Arushanisoma zaid

Waandishi wa habari wakamatwa wilayani Arumeru mkoani Arushanisoma zaid

ARUMERU, ARUSHA: Waandishi Bahati
Chume(Mwananchi) & Doreen Aloyce
(Sunrise Radio) wakamatwa kwa amri ya
DC - Wapo kituo cha Usa River.
Taarifa kwa hisani ya JamiiForums
Twitter;

Wednesday, February 1, 2017
Hii ni nini tena Bombadier Q dash400 soma zaid

Hii ni nini tena Bombadier Q dash400 soma zaid

Zaidi ya abiria 70 wa ndege ya Bombadier Q
dash 400,waliokuwa wakisafiri kutoka jijini
Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam jana majira
ya saa moja usiku,wameshindwa kusafiri kwa
kutumia ndege hiyo kutokana na kupata hitilafu
kwenye moja ya injini zake.
Kaimu Meneja wa uwanja wa ndege Mwanza
David Matovolwa amesema kutokana na ndege
hiyo yenye namba za usajili 5H TCB, kupata
hitilafu ikiwa inataka kunyanyuka kwenye
barabara ya kutulia na kurukia ndege ( runway ),
ilibidi abiria kubadilishiwa ndege iliyotoka Dar es
salaam ambapo waliweza kuondoka majira ya saa
saba kasorobo usiku huo huo.
Akithibitisha ndege hiyo kupata hitilafu,
Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la ndege Tanzania
( ATCL ), Mhandisi Emmanuel Koroso ameiambia
ITV kwa njia ya simu kwamba ndege hiyo
imeondoka uwanja hapo hii leo majira ya saa
4.30 asubuhi kuelekea jijini Dar es salaam ikiwa
haina abiria baada ya mafundi kuifanyia
matengenezo ya awali.
Shirika la ndege Tanzania lilizindua rasmi safari
za ndege zake aina ya Bombadier Q dashi 400
kati ya Dar es Salaam na Mwanza Oktoba mwaka
jana, ambapo ndege hiyo iliwasili mwanza kwa
mara ya kwanza saa 10.45 jioni ikiwa Katibu
mkuu wa Wizara ya ujenzi,uchukuzi na
mawasiliano Leonard Chamriho na kupokelewa na
mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.chanzo redio one.

Back To Top