Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Friday, June 3, 2016
Boti iliyokuwa imebaba mamia ya wahaniaji kutoka uturuki imezama .soma zaid.

Boti iliyokuwa imebaba mamia ya wahaniaji kutoka uturuki imezama .soma zaid.

Operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea karibu
na kisiwa cha Ugiriki cha Crete baada ya boti
iliokuwa na mamia ya wahamiaji kuzama.
Walinzi wa pwani ya Ugiriki wanasema kuwa
zaidi ya watu 300 wameokolewa kufikia sasa
huku miili mitatu ikipatikana.
Kiongozi wa shirika la kimataifa kuhusu Uhamiaji
katika eneo hilo Daniel Esdras ameiambia BBC
kwamba chombo hicho kilikuwa boti ya mita 25
kwa urefu ambayo ina uwezo wa kubeba watu
700.
Vyombo vya majini vya walinzi wa pwani ,ndege
na helikopta zimehusishwa katika operesheni
hiyo ambayo inafanyika yapata kilomita 100
kutoka pwani .
Hadi kufiki sasa ni wahamiaji wachache
waliowasili Crete ambayo ipo kaskazini mwa
Libya na Misri.

Wanafunzi wa chuo cha TEKU kuhakikiwa vyeti vyao.soma zaid.

Wanafunzi wa chuo cha TEKU kuhakikiwa vyeti vyao.soma zaid.

Tume ya vyuo vikuu Tanzania(TCU)
itapitia taarifa za wanafunzi wa chuo
kikuu cha Teofilo Kisanji(TECU) hasa
vigezo vilivyotumika kudahiliwa chuoni.
Wanafunzi wote wametakiwa kuwasilisha
vyeti vyao vya shule ya sekondari kwa
vidato vya nne na sita na vyeti vya
stashahada kabla ya Juni 04, 2016.
Kushindwa kufanya hivyo kutapelekea
wanafunzi hao kuondolewa vyuoni.

Wednesday, June 1, 2016
Donard Trump aendelea kujizolea umaarufu na kukubalika na nchi nyingine.

Donard Trump aendelea kujizolea umaarufu na kukubalika na nchi nyingine.

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini
vimemsifu mgombea wa urais kupitia tiketi ya
chama cha Republican Donald Trump kuwa
mwanasiasa ''mwenye hekima'' ambaye anaweza
kuwa na ushirikiano mzuri na Korea Kaskazini.
Uhariri wa mtandao wa DPRK ulisema kwamba ni
mgombea ''anayeona mbali''.
Bw Trump hivi majuzi alisema kuwa alikuwa
tayari kukutana na kiongozi wa Korea kaskazini
Kim Jong Un na pia amependekeza kuviondoa
vikosi vya Marekani kutoka Korea Kusini.
Wachanganuzi wanasema uhariri huo sio sera
rasmi ya taifa hilo lakini huenda unaangazia fikra
za Pyongyang.
BBC Monitoring imesema kuwa DPRK ni
miongoni mwa mitandao ya propaganda
inayotumiwa na Korea Kaskazini.
Mtandao huo unadaiwa kuwakilisha maoni ya
Pyongyang lakini mwandishi wake hajulikani.

Upinzani wamewasilisha kwa sipka wa bunge hoja kumwondoa Naibu spika.soma zaid.

Upinzani wamewasilisha kwa sipka wa bunge hoja kumwondoa Naibu spika.soma zaid.

Upinzani
wamewasilisha kwa Spika
wa Bunge hoja ya
kumwondoa madarakani
Naibu Spika, Dk Tulia
Ackson kwa kutokuwa na
imani naye.
Hatua hiyo imefikiwa na
wabunge hao kufuatia
kutoridhishwa na
mwenendo wa uongozi wa
Dk Tulia anapokalia kiti cha
Spika.
Tangu Jumanne wiki hii,
wabunge hao wamekuwa
wakisusa vikao
vinavyoongozwa na
kiongozi huyo kwa madai
anaminya demokrasia.
Walifikia uamuzi huo baada
ya Dk Tulia kuzuia
kujadiliwa hoja ya
kufukuzwa kwa wanafunzi
zaidi ya 7,000 wa Chuo
Kikuu cha Dodoma (Udom)
iliyowasilishwa na Mbunge
wa Arumeru Mashariki,
Joshua Nassari na
kukatisha mjadala wa
bajeti ya maji.
Kitendo hicho kiliwafanya
wabunge wote wa upinzani
kupingana na maamuzi ya
Dk Tulia, jambo
lililosababisha watolewe
bungeni.
Kutokana na hali hiyo
wabunge hao kupitia
Mbunge wa Simanjiro,
James Ole Millya
akisindikizwa na Mbunge
wa Kibamba, John Myika
wa Chadema na Mbunge
wa Konde wa CUF, Khatibu
Said Haji waliwasilisha hoja
hiyo kwa Katibu wa Bunge,
Dk Thomas Kashilillah
baada ya Spika, Job
Ndugai kutokuwapo
bungeni.
Hoja hiyo iliwasilishwa kwa
mujibu wa Kanuni ya 138
(1) ambayo inaeleza
utaratibu wa jinsi ya
kumwondoa Naibu Spika.
Kanuni hiyo inasema,
“Utaratibu wa kumwondoa
Naibu Spika madarakani
chini ya Ibara ya 85(4)(c)
ya Katiba utakuwa kama
ule wa kumwondoa Spika,
isipokuwa tu taarifa ya
kusudio la kumwondoa
Naibu Spika madarakani
inayoeleza sababu kamili
za kuleta hoja hiyo,
itapelekwa kwa Spika
ambaye ataiwasilisha
kwenye Kamati ya Haki,
Maadili na Madaraka ya
Bunge kwa ajili ya
kuijadili.”
Fasili ya pili ya Kanuni hiyo
inasema: “Endapo Kamati
ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge
itaridhika kuwa zipo
tuhuma mahususi dhidi ya
Naibu Spika zinazohusu
uvunjaji wa Katiba, Sheria
au Kanuni zinazoongoza
Shughuli za Bunge, basi
Kamati hiyo itaidhinisha
kuwa hoja hiyo ipelekwe
bungeni ili iamuliwe.”
Kwa mujibu wa Ibara ya
85(4)(c), Naibu Spika
atakoma kuwa Naibu Spika
na ataacha kiti cha Naibu
Spika endapo ataondolewa
kwenye madaraka ya Naibu
Spika kwa azimio la Bunge.
Akizungumzia uwasilishwaji
wa hoja hiyo, Millya
alisema taarifa zaidi
watatoa leo kuhusu
msimamo wao huo.
Dk Tulia aliwataka
wabunge wenye
malalamiko juu ya utaratibu
wa uendeshaji wa shughuli
za Bunge kukata rufaa kwa
kufuata Kanuni za Bunge.
Alisema kanuni ndogo ya
5(2) inasema Spika
atawajibika kutilia nguvu
kanuni zote za Bunge na
5(3) inasema Spika
anaweza kumtaka mbunge
yeyote anayekiuka kanuni
hizi kujirekebisha mara
moja.
Alisema kwa hiyo mbunge
yoyote asiyeridhika, kanuni
za Bunge zinamruhusu
kukata rufaa na
zinamweleza nini cha
kufanya.
Je, Una
Habari,Picha,Tang
azo,Makala,
Ushauri n.k.?Basi
Wasiliana Nasi
Simu/WhatsApp
0757478 553 ,0625
918 527
Hifadhi blog hii
kwenye simu yako
ili upate habari
zetu kwa urahisi
zaidi Bofya HAPA
U Download sasa
App ya Malunde1
blog
Malunde
Like Page
Facebook Blogger Plugin by
Labels: siasa
- Print Email 
×
02
Jun 2016
Share to:
Previous
Jambazi
Auawa
Akipamba
na na
Polisi Jijini
Mwanza
Rais Magufuli Amteua
Anne Makinda Kuwa
30 May 2016
Search

Watumishi 5 wasimamishwa kazi wilayani nzega mkoani tabora.soma zaid.

Watumishi 5 wasimamishwa kazi wilayani nzega mkoani tabora.soma zaid.


BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Wilaya
ya Nzega, mkoani Tabora limewasimamisha kazi
watumishi watano kwa tuhuma za ubadhirifu wa
zaidi ya Sh milioni 190, ambazo ni fedha za
Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) pamoja na fedha
za chanjo.
Watumishi hao wanatuhumiwa kughushi nyaraka,
kukosekana kwa baadhi ya nyaraka za fedha,
kuidhinisha malipo hewa pamoja na kukiuka
taratibu na kanuni za utumishi wa umma na
kukiuka matumizi ya fedha za umma.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa
Tabora, Aggrey Mwanri na Mwenyekiti wa
halmashauri hiyo, Kiwelle Bundala. Kiwelle
aliwataja watumishi waliosimamishwa kazi
kupisha uchunguzi kuwa ni Katibu wa Afya
Wilaya, Kisasu Sikalwanda, Mhasibu wa
Halmashauri ya Wilaya, Denins Gombeye, Mratibu
wa Chanjo wa Wilaya, Joel Mjondela, Mganga
Mkuu Hospitali ya Wilaya, Emmanuel Mihayo na
Mweka Hazina, Stanslaus Kalokola.
Alisema uchunguzi utakapofanyika na kubaini
watumishi hao hawana hatia wataendelea na kazi
na ikiwa tofauti hatua nyingine za kinidhamu
zitachukuliwa.
Mwanri alilipongeza baraza hilo kwa kuchukua
maamuzi magumu ya kulinda maslahi ya
wananchi na kuongeza kuwa ataendelea
kusimamia sheria na taratibu za utumishi wa
umma. Aliwataka watumishi wa Serikali
kuhakikisha wanasimama katika nafasi zao za
kufanya kazi kwa uandilifu na kuepuka ubadhirifu
ambao hauna faida ndani yake.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG), Mkoa wa Tabora, Mohamed Msangi
alisema sababu za watumishi hao kusimamishwa
kazi ni kughushi nyaraka za malipo, kukosekana
kwa baadhi ya nyaraka pamoja na kufanya
malipo hewa.
Alisema taarifa ya CAG inaonesha kukiuka
taratibu nyingi za matumizi ya fedha za umma.

Wabunge wa upinzani waliosimamishwa watakutana na  kitanzi kingine.

Wabunge wa upinzani waliosimamishwa watakutana na kitanzi kingine.

Wabunge saba wa upinzani waliosimamishwa
bungeni, watakumbana na kibano kingine cha
kukatwa mshahara na posho kwa kipindi chote
cha kutumikia adhabu.
Dodoma. Wabunge saba wa upinzani
waliosimamishwa bungeni, watakumbana na
kibano kingine cha kukatwa mshahara na posho
kwa kipindi chote cha kutumikia adhabu.
Wabunge hao ambao Jumatatu walisimamishwa
kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda tofauti
kwa madai ya kukiuka kanuni ni Zitto Kabwe
(Kigoma Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki),
Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini)
, John Heche (Tarime Vijijini) na Godbless Lema
(Arusha Mjini).
Adhabu hiyo ilitolewa kama azimio la Bunge
baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka
ya Bunge kupendekeza wabunge hao waadhibiwe
kutokana na kuomba mwongozo wa kiti cha
Spika kwa jambo ambalo tayari lilishatolewa
uamuzi.

Watuhumiwa 6 wa ubakaji morogoro wanyimwa dhamana mahakamani.soma zaid.

Watuhumiwa 6 wa ubakaji morogoro wanyimwa dhamana mahakamani.soma zaid.

Washtakiwa sita wanaokabiliwa na
makosa tofauti yakiwemo ya kubaka,
kulawiti na kusambaza picha chafu na za
ngono wameendelea kusota rumande kwa
kukosa dhamana, baada ya mvutano mkali
wa mawakili wa upande wa mashtaka na
upande wa washtakiwa kuibuka
mahakamani hapo, na hakimu
anayesikilisha shauri la dhamana
kuahirisha shauri hadi Juni 15 mwaka
huu kutoa uamuzi juu ya dhamana.
Miongoni mwa washtakiwa hao,
wawili,Iddi Adam Mabena (21) mkazi wa
Njombe na Zuberi Thabit (30) mkazi wa
Mbarali Mbeya wanaokabiliwa na shtaka
la kumbaka na kumlawiti binti mwenye
umri wa miaka 21 mkazi wa Wami
Dakawa,wilayani Mvomero wanalodaiwa
kutenda Aprili 27 mwaka huu majira ya
usiku katika nyumba ya kulala wageni ya
titii iliyopo wami dakawa wilayani
mvomero,shauri lao linalosikilizwa faragha
limeahirishwa tena mbele ya Hakimu
mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya mkoa
wa Morogoro Mary Moyo.
Upande wa mashtaka katika shauri hilo
linalosikilizwa faragha kwa mujibu wa
sheria, umewakilishwa na waendesha
mashtaka Gloria Rwakibalila,Edgar
Bantulaki,Calistus Kapinga na Mohamed
Mkali na limepangwa kufikishwa tena
mahakamani hapo Juni 15 mwaka huu
kwaajili ya kuanza usikilizwaji wa awali
baada ya upelelezi kukamilika.
Uamuzi wa dhamana itolewe ama
isitolewe umeshindwa kufikia muafaka
baada ya mvutano wa kisheria wa
mawakili wa utetezi na wa Jamhuri, katika
shtaka la kusambaza picha chafu na za
ngono kwa njia ya mtandao kinyume na
sheria ya makosa ya mtandao no 14 ya
mwaka 2015, linalosikizwa mbele ya
hakimu Ivan Msaki,wa Mahakama ya
Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro,dhidi
ya washtakiwa sita,iddi Mabena na Zuberi
Thabit,wanaotetewa na wakili Mohamed
mkali,na Rajab Salehe,Ramadhani Ally
Makunja, Muhsin Ngai na John Peter
Thabiti maarufu kama paroko, wakazi wa
wami dakawa wilayani Mvomero
wanaotetewa na wakili Ignas Punge.
Upande wa mashtaka umeendelea kutetea
uamuzi wake wa kuwasilisha kiapo cha
kupinga dhamana kwa vile shauri hilo
limevuta hisia ya watu, usalama wao
utakuwa mashakani wawapo uraiani hasa
ikizingatiwa wanadaiwa kudhalilisha utu
wa mwanamke na kutoharibu upelelezi
kwa vile bado haujakamilika,na kwamba
taarifa za kiintelijensia zimebainisha
wakiachiwa huru wanaweza wakadhuriwa
na jamii.
Hata hivyo upande wa utetezi
uliowasilisha hati kupinga kiapo hicho
umedai dhamana ni haki ya
mshtakiwa,hakuna raia aliyewasilisha
kiapo kuhusu hasira kali alizonazo dhidi
ya washtakiwa isipokuwa labda ni hisia za
mkuu wa upelelezi wa mkoa.
Hakimu Ivan Msaki ameahirisha shauri
hilo hadi Juni 15 mwaka huu ambapo
uamuzi wa washtakiwa kupewa dhamana
au kunyimwa dhamana utajulikana.

Back To Top