Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Monday, November 7, 2016
FBI imesema Hillary Clintoni hana hatia.soma zaid

FBI imesema Hillary Clintoni hana hatia.soma zaid

Mkurugenzi wa FBI,James Comey ameliambia
bunge la Marekani kuwa baada ya kupitia barua
pepe zilizogundulika kutoka kwa Hillary Clinton,
wakati alipokua waziri wa mambo ya nje
wamegundua kuwa hana hatia yoyote na
hawatamfungulia mashtaka.
Kampeni za Clinton ziliingia doa wiki iliyopita
baada ya mkurugenzi huyo wa FBI kusema kuwa
watazipitia barua pepe zake zilizopatikana katika
kompyuta ya msidizi wa zamani wa mume wake.
Kauli hiyo imeonekana kumfurahisha mkuu wa
mawasiliano wa kampeni za Clinton Jennifer
Palmieri
Donald Trump,mgombea urais nchini Marekani
Wakati upande wa Bi Clinton wakifurahia hatua
hiyo kwa upande wake Donald Trump amesema
Hillary Clinton analindwa na mfumo wa wizi wa
kura, amesema Bi Clinton angetakiwa
kuchunguzwa kwa muda mrefu.
Na hivi sasa tunaunana moja kwa moja na
Zuhura ebu tuambie baada ya FBI kusema
hawatamshtaki Hilary Clinton, hali ikoje kwa sasa
ikiwa ndio imebaki takribani siku moja uchaguzi
ufanyike. BBC

Asikali nchini Canada wanachunguza kelele za ajabu kutoka bahari ya Antarct

Asikali nchini Canada wanachunguza kelele za ajabu kutoka bahari ya Antarct

Kelele hizo ziliripotiwa na watu wa eneo hilo
kwamba zimewatisha wanyama na kuwafanya
wakimbie mbali katika kipindi cha miezi
michache iliyopita.
Jeshi la Canada limechunguza kelele za ajabu
zenye mlio mkali zinazotoka kwenye sakafu ya
bahari katika eneo lisiloweza kufikiwa kwa
urahisi la kanda ya Arctic, maafisa wameiambia
BBC
Kelele hizo za ajabu ziliripotiwa na watu wa
eneo hilo kwamba zimewatisha wanyama na
kuwafanya wakimbie mbali katika kipindi cha
miezi michache iliyopita.
Ndege ya kijeshi imefanya msako wa aina mbali
mbali wa kunasa sauti hizo, wamesema maafisa
siku ya Ijumaa.
Hata hivyo jeshi hilo la Canada limesema hadi
sasa haliwezi kuelezea sababu ya "sauti hizo za
ajabu".
" Mhudumu wa ndege hiyo amesema
hawakuweza kubaini kitu chochote cha ajabu
kwenye uso wa bahari ama chini ya uso wa
bahari ," imesema taarifa ya jeshi iliyotolewa
kwa BBC.
" Kile ambacho alikiona ni makundi mawili ya
nyangumi na sili wa bahari wenye pembe sita
katika eneo lililochunguzwa''
Msemaji wizara ya usalama wa taifa mjini
Ottawa amesema kuwa sababu ya kelele hizo -
amazo wakazi wanasema zinaweza kusikika
hata kupitia kuta za maboti zimesalia kuwa
vigumu kutambuliwa.
Eneo ambalo llimekumbwa na kelele za ajabu
Sauti hizo ambazo zimekuwa zikisika katika
kipindi chote cha majira ya joto katika maeneo
ya baridi, mbunge Paul Quassa ameiambia CBC,
yapata kilomita 120 kaskazini-magharibi mwa
kijiji kidogo cha Igloolik.
Eneo hilo ni njia ya vijito vya maji katika
Nunavut, eneo ambalo ni makazi mapya ,
makubwa na yenye kukaliwa na idadi ndogo ya
watu nchini Canada, karibu na Greenland.
" Ni moja ya maeneo maarufu zaidi kwa
shughuli za uwindaji nyakati za majira ya joto
na baridi kwasababu ni eneo pana zaidi la maji
lililozingirwa na barafu ambayo ina wanyama
wengi wa baharini ," Amesema Bwana Quassa.
" Na wakati huu, majira haya ya joto, kulikuwa
hakuna mnyama yoyote. Na hili likawa suala la
kushangaza."
Maelezo mbali mbali kuhusu sauti hizo za
kushangaza yamekuwa yakiwasilishwa katika
vyombo vya habari nchini Canada.

Saturday, November 5, 2016
Asasi za kiraia nchini zililazimika kuanzisha mchakato wa kudai katiba mpya.soma zaid

Asasi za kiraia nchini zililazimika kuanzisha mchakato wa kudai katiba mpya.soma zaid

Asasi za Kiraia nchini jana ziliazimia kuanzisha
mchakato wa kudai katika mpya huku zikiahidi
kutowahusisha wanasiasa katika harakati hizo,
tofauti na ilivyokuwa awali.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika jijini Dar
es Salaam, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa
Haki za Binadamu, Onesmo Ole Nguruma alisema
kuwa wameazimia hayo ili mchakato huo uwe wa
wananchi na sio wa wanasiasa.
“Mwaka jana mchakato ulikuwa wa kisiasa zaidi,
sasa hivi tunataka kuanzisha mchakato
utakaokuwa wa wananchi,” alisema Ole
Nguruma.
Alisema kuwa baadhi ya wanasiasa walichangia
kukwamishwa kwa mchakato huo kwakuwa
baadhi yao mwishoni walijikuta wakitofautiana na
wengine kuzila kuendelea na harakati hizo.
Katika hatua nyingine, Rais John Magufuli jana
aliwaambia wahariri wa vyombo vya habari katika
mahojiano ya ana kwa ana Ikulu jijini Dar es
Salaam, Rais Magufuli alipoulizwa kuhusu
mpango wa kuanzisha upya mchakato wa Katiba
Mpya alisema “niacheni ninyooshe nchi kwanza.”
Rais Magufuli alisema kuwa yeye
hakulizungumzia suala hilo kwenye kampeni zake
zote.
Mchakato wa kupata katiba mpya ulianzishwa na
Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya
Kikwete na kuunda Tume iliyokuwa chini ya
uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba ambaye
alitengeneza rasimu iliyowagawanya wabunge wa
bunge la katiba, wanaharakati pamoja na Serikali.
Wanaharakati wanadai rasimu ya Jaji Warioba
iliyowasilishwa kwenye Bunge la Katiba na
mapendekezo ya wananchi ndiyo ipewe
kipaumbele, huku Serikali ikiwa imebadili baadhi
ya maeneo hali iliyoleta mkanganyiko wa
mawazo.

Walimu wahofia ushirikina wilayani ukererwe.soma zaid

Walimu wahofia ushirikina wilayani ukererwe.soma zaid

Ukerewe. Hofu ya vitendo vya ushirikina
imewafanya baadhi ya walimu wa Shule ya
Msingi Uhuru wilayani Ukerewe, Mkoa wa
Mwanza kushinikiza kuhamishwa.
Hali hiyo inatokana na mwalimu mwenzao,
Charles Bwatwa kuanguka ghafla na kupoteza
maisha akiwa njiani kurejea nyumbani.
Kabla ya kifo cha mwalimu Bwatwa kilichotokea
Oktoba 23, inadaiwa na walimu hao wamekuwa
wakifanyiwa ushirikina na hasa usiku wakiwa
wamelala.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Godwin Laurent
amesema tangu kifo cha mwenzao, walimu
wamekuwa wakiishi kwa hofu kiasi cha
kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kagera, Alfaxad
Kapole amelazimika kuitisha kikao cha pamoja
kati ya walimu na wakazi wa eneo hilo kujadili
madai ya kuwapo vitendo vya kishirikina.
Ofisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Sengerema, Reginald Richard amesema kamati
maalumu imeundwa kuchunguza ukweli wa
jambo hilo ambalo limekuwa kikwazo cha utoaji
elimu kwa wanafunzi shuleni hapo.

Tuesday, November 1, 2016
Mwalimu akithaminiwa Elimu yetu itapanda chati.soma zaid

Mwalimu akithaminiwa Elimu yetu itapanda chati.soma zaid

Mwaka 1966, Mwalimu Julius Nyerere alisema,
nanukuu.
“Wale wenye wajibu wa kufanya kazi na vijana
wa umri mdogo wana nguvu kubwa zisizozidiwa
na nguvu za yeyote yule kwa kutilia maanani hali
ya baadaye ya jamii yetu. Nguvu hizi zipo katika
makundi mawili, wazazi na walimu.”
Ukisoma hotuba zake nyingi, zimezungumzia kwa
kina masuala ya elimu kama mkombozi. Mwalimu
alieleza wazi kuwa, lengo la kwanza la elimu ni
kumkomboa mtu binafsi na taifa kutoka kwenye
kutegemea mataifa yaliyoendelea kiuchumi na
kiutamaduni.
Aidha, elimu inapaswa kumjengea mhitimu
maarifa, stadi na uwezo wa kukabiliana na
changamoto za maisha halisi anayoishi.
Katika kufanikisha lengo hili la elimu, mwalimu
alitaja katika nukuu hapo juu kuwa kuna makundi
mawili ambayo yana nguvu kubwa ya kuwafanya
wanafunzi kufikia malengo ya kuwapo shuleni.
Makundi haya ni wazazi na walimu.
Tafiti nyingi zilizofanyika katika kubaini sababu
za kushuka kwa ubora wa elimu zimekuwa
zikijikita katika kuangalia masuala kama
miundombinu isiyofaa ya kufundishia na
kujifunzia. Ni tafiti chache zilizolenga kuangalia
ubora wa walimu na mazingira yanayomzunguka.
Pia, tafiti hizo zinaonyesha wazi kuwa watoto
wetu hawajifunzi licha ya kuwa wanakwenda
shuleni. Kwa mfano, siyo jambo la kushanganza
kuona watoto wakimaliza darasa la saba bila
kujua kusoma na kuandika.
Jitihada zilizofanyika kujaribu kuinua kiwango cha
ubora wa elimu haziwezi kupuuzwa hata kidogo.
Serikali na wadau mbalimbali wamekuwa
wakifanya jitihada kubwa kuinua kiwango cha
ubora wa elimu yetu, lakini bado hatujaweza
kupata matokeo yanayotakiwa kama ambavyo
wadau wengi walitarajia.
Lazima tukubali kutafuta mzizi halisi wa tatizo la
kushuka kwa elimu yetu. Pengine tatizo
linafahamika lakini nia ya kushughulikia tatizo
siyo makini.
Kimsingi, tumechelewa kushugulikia kiini cha
tatizo kiasi kwamba Tanzania ya viwanda na ya
uchumi wa kati tunayoitaka kufikia mwaka 2025,
inaweza kuishia midomoni kama hatutaamua
kuchukua hatua mapema.
Wadau wengi wa elimu wameshasema kuwa
kuwathamini walimu ni moja ya hatua ya
kurejesha ari ya ufundishaji kama ilivyokuwa
miaka ya nyuma, yaani enzi za Mwalimu Nyerere.
Kuanzia ngazi ya taifa mpaka familia, walimu
hawaonekani tena kama watu muhimu;
wanachukuliwa kama watu maskini waliokosa
cha kufanya na ndiyo maana wapo huko.
Mwalimu mmoja aliwahi kusema: “Kuna wakati
wanafunzi wananiuliza, “Mwalimu, una akili, lakini
sasa kwa nini uliamua kuwa mwalimu?” Maswali
ya aina hii yanakera. Ina maana wanaamini
mwalimu ni mtu aliyefeli, asiye na akili.
‘’Ninapowaambia, nilipenda tu kuwa mwalimu”,
wananiambia huoni kwamba unachelewa katika
maisha? Haya ndiyo maisha tunayoishi katika
shule hii.’’
Ni dhahiri kuwa huu ndiyo mzizi wa tatizo la
kushuka kwa ubora elimu yetu. Miundombinu ni
muhimu katika kujifunza na kufundisha, lakini
pasipo walimu bora wenye moyo na hamasa ya
kufundisha kamwe hatutofikia elimu bora
tunayoitaka.
Utafiti uliofanywa na shirika la HakiElimu mwaka
2011 usemao: Je? Walimu wana sifa za ualimu
na hamasa ya kufundisha?, pamoja na mambo
mengine ulibianisha kuwa mwalimu kuwa na sifa
nzuri za kitaaluma pekee bila kuwa na hamasa
na moyo wa kujitolea hakusababishi kiwango cha
ufaulu wa mwanafunzi kitaaluma kuimarika’
Benedicta Mrema ni ofisa programu Idara ya
Habari na Utetezi, HakiElimu media@
hakielimu.org.chanzo mwananch

Bunduki  11 zakamatwa nyumbani kwa Mubunge Dar.

Bunduki 11 zakamatwa nyumbani kwa Mubunge Dar.

Dar es Salaam. Kikosi kazi maalumu
kilichoundwa na Serikali kupambana na tatizo
sugu la ujangili, kimenasa bunduki 11 ambazo
zinasadikiwa kutumika kufanya ujangili na
kukamata watu wanne zaidi.
Taarifa zilizopatikana jana zimelidokezea gazeti
hili kuwa bunduki hizo zilikamatwa nyumbani kwa
mbunge wa CCM (jina tunalihifadhi) ambaye
bado anasakwa na kikosi kazi hicho.
Matukio hayo yamekuja siku chache baada ya
Rais John Magufuli kutaja jina la mtu anayeitwa
Mpemba kuhusika na ujangili kwa muda mrefu
wakati alipotembelea ofisi za Wizara ya Maliasili
na Utalii na kushuhudia pembe 50 za ndovu
zilizokamatwa na watumishi wa wizara hiyo.
Siku hiyo, Rais aliwaambia watu aliowaita
“vijana” waendelee na kazi yao ya kukamata
wauaji wa tembo, akiwahakikishia kuwa Serikali
ipo na kuwataka wasiogope mtu yeyote yule.chanzo mwananch

Mali za Kampuni ya Mohamed Trans ltd zitapigwa mnada na TRA baada ya.soma zaid

Mali za Kampuni ya Mohamed Trans ltd zitapigwa mnada na TRA baada ya.soma zaid

Mali za kampuni ya Mohamed Trans
Limited zitapigwa mnada na Mamlaka ya
Mapato Tanzania(TRA) baada ya
kushindwa kulipa limbikizo lake la kodi
analodaiwa.
Kampuni hiyo pamoja na mali nyingine,
inamiliki mabasi ya Mohamed Trans
yanayofanya safari zake kwenye mikoa
mbalimbali.
Mnada huo utafanyika tarehe 4/11/2016.
Mnada huo utaendeshwa na Kampuni ya
udalali ijulikanayo kama Sukah Security
Company Limited Auction Mart & Court
Broker.
Mnada huo utafanyika mkoani Shinyanga
katika Yard ya Mohamed Trans.
MY TAKE: Ni mwendo wa kuisoma
namba. Watu walishazoea vya kunyonga!
- 5 people

Back To Top