Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Wednesday, March 15, 2017
Rais amemusimamisha katibu mkuu ofsi ya waziri mkuu( Bunge) Ule abbasi musa.soma zaid

Rais amemusimamisha katibu mkuu ofsi ya waziri mkuu( Bunge) Ule abbasi musa.soma zaid

Wednesday, March 8, 2017
Hii ndilo jina jipya la pombe za viroba ambapo jina hilo jipya ni Nguruka ni wapi hapo.soma zaid

Hii ndilo jina jipya la pombe za viroba ambapo jina hilo jipya ni Nguruka ni wapi hapo.soma zaid

WAFANYABIASHARA wa vileo mkoani Morogoro, wamebadili jina la pombe inayofungashwa katika mifuko ya plastiki maarufu viroba kwa kuiita ‘nguruka’ kukwepa mkono wa sheria. Nguruka ni jina ambalo linatumika kwa wenyeji kuogopa kutaja jina la kiroba na linajulikana kwa wengi katika Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake. Katika baadhi ya mitaa, MTANZANIA limebaini kwa sasa watumiaji wa pombe hizo wamebuni jina hilo waweze kuendelea na biashara hiyo bila kujulikana na vyombo vya dola na mamlaka nyingine zinazohusika na ukamataji huo. Mmoja wa watumiaji wa kinywaji hicho aliyejitambulisha kwa jina la Majaliwa Masepu, mkazi wa Msamvu, alisema: “Sasa hivi ukienda baa au dukani unatakiwa kusema naomba ‘nguruka’, muuzaji atakuuliza unataka nguruka wakubwa au wadogo, maana kuna aina mbili za ujazo wa viroba.” Masepu alisema hatua ya Serikali kuzuia pombe hiyo imeathiri wafanyabiashara na watumiaji kwa kuwa imekuwa ghafla mno kiasi cha kutishia wafanyabiashara wengi kufilisika ikizingatiwa walikuwa na mzigo mkubwa katika maghala yao. “Ni vema Serikali ingetupatia muda hata wa miezi mitatu kumaliza mzigo wetu,” alisema mfanyabiashara mmoja. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urlich Matei, alisema msako huo wa viroba unaendelea na watachukuliwa hatua wafanyabiashara wanaokaidi agizo hilo kwa kuendelea kuuza viroba.

Tuesday, March 7, 2017
Uhuru kinyatta kuongea na Trump kwa simu.soma zaid

Uhuru kinyatta kuongea na Trump kwa simu.soma zaid


Rais wa Marekani Donald Trump anategemea
kufanya mazungumzo na rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta kwa njia ya simu....
Uhuru Kenyatta atakuwa rais kwanza kutoka
AFRIKA MASHARIKI kuzungumza na rais huyo
kutoka taifa lenye uwezo mkubwa duniani .
Miongoni mwa maswala wanayotarajiwa kugusia
ni swala la usalama ,Somalia na ukame
unaendelea kukumba eneo zima la Afrika
mashariki.

Bosi aliyempa Makonda Hekari 1500 amehojiwa na polisi.soma zaid

Bosi aliyempa Makonda Hekari 1500 amehojiwa na polisi.soma zaid

Mkurugenzi wa kampuni ya Azimio Housing Estate, Mohamed Ikbal, ambaye hivi karibuni alimgawia ardhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amehojiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka za Serikali. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alithibitisha jana kwamba mfanyabiashara huyo aliitwa kwa ajili ya mahojiano, lakini aliachiwa kwa dhamana baada ya muda kuonekana hautoshi. “Alikuja na wakili wake, lakini ameachiwa kwa dhamana ataripoti siku nyingine (hakutaja siku),” alisema Sirro. “Anatuhumiwa kughushi nyaraka za Serikali na sasa upelelezi unaendelea.” Mfanyabiashara huyo inadaiwa kuwa aliripoti polisi jana saa tano asubuhi na kuhojiwa kabla ya kuachiwa kwa dhamana jioni. Kuhojiwa kwa Ikbal, ambaye kampuni yake iliwahi kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika miradi kadhaa tata ya ujenzi, kumekuja siku chache baada ya kumgawia Makonda eneo la ekari 1500 katika kitongoji cha Ligato kijiji cha Kisarawe II wilayani Kigamboni kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo. Siku mbili baadaye, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliibuka na kueleza kwamba eneo aliloligawa mfanyabiashara huyo si lake bali linamilikiwa na serikali na wanakijiji. “Eneo lile ni la Serikali si la yule mtu aliyejitangaza anampa Makonda na kwa sababu amemdanganya na mimi ndiye msimamizi wa ardhi, nitamsaidia Makonda kuchukua hatua ili watu wasijipendekeze kusafisha maovu yao kwa kutumia migongo ya viongozi,” alisema Lukuvi. “Hadi siku ile alipokuwa anajipendekeza kwa Makonda, ardhi ile haikuwa yake, wananchi walishashinda kesi mahakamani kwa sababu hakuwa na vielelezo. Ukimdanganya Mkuu wa Mkoa umeidanganya Serikali. Makonda hakuomba ile ardhi ila yeye (Ikbal) ndiye alikwenda kumgawia na amemgawia akijua kwamba alishashindwa kesi,” alisema Lukuvi. Kwa mujibu wa hukumu ya kesi hiyo Na 147 ya mwaka 2015 iliyofunguliwa na Ikbal katika Baraza la Ardhi la Wilaya ya Temeke dhidi ya Baraza la Ardhi la Kijiji, mfanyabiashara huyo alishindwa. “Maombi haya yanatupiliwa mbali pamoja na gharama,” ilisema hukumu hiyo ya Januari 13, 2016. Ijumaa iliyopita mtu aliyejitambulisha kuwa ni mwakilishi wa Ikbal, Kamugisha Katabaro aliibuka na kudai Lukuvi amewasikitisha Watanzania na wataalamu mbalimbali wanaofahamu ukweli wa jambo hilo. Katabaro alidai Ikbal anamiliki ardhi yenye ukubwa wa ekari 3,500 ambayo aliinunua tangu mwaka 2005 kutoka kwa wananchi wa eneo la Lingato. “Wananchi waliliuza hilo eneo bila ya kushurutishwa kwa kufuata taratibu za kisheria na umiliki wa ardhi,” alidai. Mwananchi lilimfuata siku hiyo, Waziri Lukuvi aweke wazi kuhusu mmiliki halali wa eneo hilo naye alisema, “Kama mfanyabiashara huyo anaona ameonewa akate rufaa mahakamani.” Alisisitiza kuwa eneo hilo ni la serikali na watu waliodhulumiwa wameanza kuorodhesha majina yao na wataalamu wa ardhi wapo kwenye eneo hilo wakiendelea na upimaji. “Hiyo ardhi ataipateje wakati mimi ninayo, na kama ana nyaraka zinaonyesha ameshinda mbona hataki kuonyesha anataka kuudanganya umma?” alihoji Lukuvi. Juhudi za kumpata Ikbal hazikuzaa matunda lakini alipoulizwa Katabaro kuhusu mkurugenzi huyo kuitwa polisi alisema ni kweli alitii wito kama alivyotakiwa na polisi. Taarifa kwamba alikamatwa siyo za kweli kwani alihojiwa na kutoka jana jioni baada ya kuwasili kituoni hapo saa tano asubuhi jana,” alieleza. Eneo jingine ambalo Azimio ilizua utata ni umiliki wa ardhi na uthaminishaji wake kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa uitwao Dege Eco Village, Kigamboni. Ulisimama Februari mwaka jana kutokana na utata wa ubia.

TANZIA:Mama wa Rais mstaafu jlJakaya kikwete amefariki dunia.soma zaid

TANZIA:Mama wa Rais mstaafu jlJakaya kikwete amefariki dunia.soma zaid

Kupitia ukurasa Instagram wa Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete ameandika ujumbe Kuhusu kifo cha Bi Nuru kama unavyosomeka hapo chini... "TANZIA Ndugu na Marafiki nasikitika kuwatangazia Msiba/Kifo cha Bibi Yetu Bi.Nuru Khalfan Kikwete Kilichotokea asubuhi hii katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa Matibabu. Taratibu za mazishi tutajulishana . Innallilllah wainnaillah rajuun.#"

Monday, March 6, 2017
no image

Vurugu za wamachinga mwanza watu 9 wamejeruhiwa wakiwemo wanamgambo wa jiji.soma zaid

Watu tisa (9) wamejeruhiwa katika vurugu wakati wa kuwaondoa wafanyabiashara wadogowadogo sehemu zisizo ruhusiwa wilayani Nyamagana, mkoani Mwanza Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa w Mwanza DCP Ahmed Msangi imesema kwamba tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.03.2017 majira ya saa15:45hrs katika mtaa wa Buhongwa Center ambapo watu tisa wakiwemo askari mgambo wa jiji la mwanza saba (07), afisa mazingira mmoja (01) na dereva wa jiji mmoja (01) walijeruhiwa. Amesema watu hao walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe sehemu mbalimbali ya miili yao na wafanyabiashara wadogowadogo waliokuwa wakifanya biashara pembeni ya barabara wakishirikiana na watu wengine waliokua wakishabikia wakati wakiendelea na zoezi la kuwaondoa wafanya biashara wadogowadogo katika maeneo yasiyo ruhusiwa haswa kwenye hifadhi ya barabara ya mwanza kwenda shinyanga. Aidha, Msangi amesema katika harakati za kudhibiti vurugu hizo askari walifanikiwa kuwakamata watu tisa ambao inadaiwa kuwa walikuwa wakihusika katika vurugu hizo kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi utakapokamilika, watafikishwa mahakamani. Majeruhi wote wapo hospitali ya mkoa ya Sekou Toure wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao inaendelea vizuri.
no image

Muendesha bodaboda ameuwawa na wananchi akidhaniwa kuwa ni mwizi mkoani Arusha.soam zaid

Mtu moja ambaye jina lake hajijafahamika ameuawa na wananchi wenye hasira kali huko maeneo ya kwa Mrombo Jijini Arusha, akidhaniwa kuwa ni mwizi wa pikipiki baada ya mtu huyo kupita na kufananishwa na waendesha pikipiki hao. Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa majira ya saa saba mchana wananchi hao walimuona mtu huyo wakadania kuwa ndiye aliyewahi kumnyanyanya mwenzao pikipiki hivyo wakaanza kumshambulia na kumburuza ambapo hadi Jeshi la Polisi kufika eneo la tukio mtu huyo alikuwa tayari ameshachoka na hali yake ilikuwa mbaya wakiwa njiani kumpeleka hospitali alifariki. Kamanda Charles Mkumbo amewataka wananchi kutochukua sheria mkononi kwani wanaweza kumdhuru mtu ambaye hausiki na tukio amesema kuwa wanapomuhisi mtu kuwa ni muhalifu watoe taarifa kwa Jeshi la Polisi ili sheria ichukue mkondo wake. Hadi sasa Jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu watano ambao ni waendesha pikipiki kwa kuhusika katika tukio hilo,mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya maountmeru ukisubiria ndugu na jamaa kwenda kumtambua. Na Vero Ignatus, Arusha
Kazi wa kuwahoji wanatuhumiwa 97 kuhusika na uuzaji wa madawa ya kulevya umeanza vigogo watabo wahojiwa.soma zaid

Kazi wa kuwahoji wanatuhumiwa 97 kuhusika na uuzaji wa madawa ya kulevya umeanza vigogo watabo wahojiwa.soma zaid

Kazi ya kuchunguza majina 97 yaliyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa Kamishna wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, imeanza kufanyiwa kazi kwa vigogo watano waliotajwa kuhojiwa. Februari 13, Makonda alimkabidhi Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Rogers Sianga orodha ya majina 97 ikiwa ni awamu ya tatu ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya. Kamishna wa Intelijensia wa Mamlaka hiyo, Fredrick Kibula alisema jana kuwa wanawahoji na wanafanya uchunguzi dhidi ya watuhumiwa hao kabla ya kuwafikisha mahakamani. “Tuna watu muhimu watano wanaotoka katika orodha ile ya mkuu wa mkoa. Tunao kwa ajili ya uchunguzi zaidi na muda ukifika tutawatajia mtawafahamu,” alisema Kamishna Kibula na kuongeza: “Hatukamati ovyoovyo ni lazima tujiridhishe bila shaka kwamba wahusika wana sifa ya kukamatwa. Pia hatutangazi ingawa tunafanya operesheni za kiuchunguzi ambazo zinafanyika mara kwa m

Rais Trump amesain upya sheria ya kupinga wahamiqji wa nchi sita za kiislam kuingia Marekani.soma zaid

Rais Trump amesain upya sheria ya kupinga wahamiqji wa nchi sita za kiislam kuingia Marekani.soma zaid

Rais wa Marekani, Donald Trump ametia saini sheria mpya ya kuzuia wahamiaji kutoka nchi sita za kiislamu kuingia Marekani, katika sheria iliyotolewa mwanzoni na kuzuiwa na mahakama ilizitaja nchi saba, lakini kwasasa Iraq imeondolewa kwenye orodha hiyo. Serikali ya Marekani imesema nchi zilizo orodheshwa zinafadhili ugaidi au zimeshindwa kupambana na magaidi wanaofanya shughuli zao ndani ya nchi zao. Aidha, Nihad Awad wa Baraza la Kiislamu nchini Marekani linalotafuta kujenga mtazamo chanya wa dini ya kiislamu nchini humo, amesema watapambana dhidi ya Amri hiyo Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika linalotetea haki za wamarekani " American Civil Liberties Union "Lee Gelernt amesisitiza kuwa sheria hiyo itaiingiza Marekani kwenye matatizo. ''Hatufikirii kuwa sheria hii ni muhimu kwa usalama wa taifa, lakini si sisi tunaosema hivyo , ni wataalam wa masuala ya usalama na wanadiplomasia wanaoheshimika kutoka kwenye uongozi wa Democratic na Republican ambao mwanzoni walichukua hatua za kufungua kesi mahakamani kupinga sheria hii wakisema haita tufanya kuwa salama,"amesema Lee Gelernt. Nchi zilizoorodheshwa kwenye sheria hiyo mpya ya Donald Trump ni Iran, Sudan, Syria, Libya, Somalia na Yemen. aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jeff Sessions ameviambia vyombo vya habari kuwa nchi tatu kati ya zilizotajwa zinafadhili ugaidi na nyingine tatu zimeshindwa kabisa kupambana na wanamgambo kama vile Islamic State na Al Qaeda
Ujio wa serikali waigusa Udom.

Ujio wa serikali waigusa Udom.

Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimewapa watumishi wake wanaoishi eneo la Kisasa maarufu nyumba 300 miezi mitatu kujaza upya maombi ya nyumba, lengo likiwa ni kuwawezesha kukatwa asilimia 10 ya mshahara kama kanuni za utumishi zinavyoelekeza. Akizungumza ofisini kwake jana, Naibu Makamu Mkuu wa Udom (Mipango, Fedha na Utawala), Profesa Ahmed Mohamed Ame alisema habari zinazoenezwa katika mitandao ni za uongo na kwamba hakuna profesa anayefukuzwa katika nyumba. “Muda wote hawa wanaokaa katika nyumba hizi wamekuwa wakikaa bure tangu mwaka 2007. Kilipoanzishwa chuo hiki iliamuliwa wafanyakazi wakae bure kama motisha kulingana na mazingira ya wakati ule,” alisema Profesa Ame. Hivi karibuni kumekuwa na taarifa katika mitandao ya jamii kuwa watumishi wa chuo hicho, wameanza kufukuzwa kwenye nyumba walizokuwa wanaishi tangu mwaka 2007 ili kuwapisha watumishi wa Serikali wanaohamia mjini hapa, jambo ambalo limewaathiri kisaikolojia. Hata hivyo, alisema sasa kuna ongezeko la wafanyakazi kutoka 200 wakati chuo kilipoanzishwa hadi 1,407 na kwamba, imefika wakati wafanyakazi wote kutendewa haki kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.

Askari polis afariki dunia akiwa kazini.soma zaid

Askari polis afariki dunia akiwa kazini.soma zaid

Iringa/Mbeya. Konstebo Dotto (28) amefariki dunia papo hapo baada ya kuanguka kwenye gari la polisi eneo la Nyang’oro, Tarafa ya Isimani mkoani hapa alipokuwa kazini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi amesema tukio hilo lilitokea juzi jioni wakati askari huyo na wenzake walipokwenda kufanya doria eneo hilo. “Ni kweli tumepatwa na msiba, askari wetu akiwa kazini na wenzake jana jioni alipata ajali, alianguka kwenye gari na kufariki dunia. Tunajiandaa na utaratibu wa kuusafirisha mwili wa marehemu kwa maziko nyumbani kwao mkoani Tabora,” amesema Mjengi. Alisema mwili wa askari huyo aliteleza kutoka kwenye gari na kuanguka barabarani. Wakati huohuo, vijana wa bodaboda katika Kijiji cha Ushirika, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wamelaumiwa kwa kuanzisha vurugu zilizosababisha wakazi wa eneo hilo kuyakimbia makazi yao baada ya polisi wawili kujeruhiwa na gari lao kuvunjwa. Diwani wa Mpuguso, Jerad Bakize alisema vurugu hizo zilisababisha wananchi kuyakimbia makazi yao baada ya polisi kuanza kurusha mabomu na kuwasaka wahusika.

Tundu Lisi amekamatwa na jeshe la polis leo asubuh.soma zaid

Tundu Lisi amekamatwa na jeshe la polis leo asubuh.soma zaid

TAARIFA.
Mwanasheria Mkuu wa Chama Tundu Lissu (MB)
amekamatwa na Jeshi la Polisi na anashikiliwa
Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) jijini Dar
es Salaam. Hadi sasa polisi hawajasema sababu
ya kumkamata na kumshikilia Tundu muda mfupi
tu baada ya kutoka Mahakama ya Kisutu ambako
kesi dhidi yake kuhusu tuhuma za uchochezi
ilikuwa imefutwa na mahakama hiyo.
Tumaini Makene (CHADEMA).

Sunday, March 5, 2017
Rais magufuli ameipongeza serikali ya msumbiji kuwafukuza watanzania.soma zaid

Rais magufuli ameipongeza serikali ya msumbiji kuwafukuza watanzania.soma zaid

Rais Magufuli akiwa ktk ziara Mtwara amesema ni sawa tu kwa Serikali ya Msumbiji kwa kuwafukuza wahamiaji haramu. Na amewataka watanzania warudi tu nyumbani kuna kila kitu ili tujenge nchi yetu. Na ulivyokwenda ndivyo utakavyorudi kwasababu Serikali haikukupeleka Msumbiji na hata usafiri wanaopewa hauna sababu kwa sasa. Amemshanga mtanzania kutoka Shinyanga kwenye dhahabu kwenda kuchimba madini Msumbiji. Msumbiji ni marafiki wa Tanzania na wahamiaji haramu wasisababishe kuharibu mahusiano kati ya Tanzania na Msumbiji. Chanzo udaku special

Saturday, March 4, 2017
Magufuli amesema sitaki mwekezaji bandarini.soma zaid

Magufuli amesema sitaki mwekezaji bandarini.soma zaid

RAIS John Magufuli ameipiga marufuku Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kuingia ubia na mwekezaji katika uendeshaji wa bandari hiyo ujenzi wa gati namba mbili utakapomalizika kwa kuwa ujenzi huo umetumia fedha za ndani. Amesema, ujenzi wa gati jipya katika Bandari ya Mtwara utafungua milango ya kiuchumi na kukuza kipato kwa wakazi wa Mtwara na serikali kwa ujumla. Rais Magufuli ametoa agizo hilo jana alipokuwa anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa gati namba 2 katika Bandari ya Mtwara. Amesema TPA wakiingia mkataba na mwekezaji katika utendaji kazi mara baada ya ujenzi huo kukamilika watakuwa wanainyonya serikali kwa kuwa imejenga miundombinu kwa fedha za ndani. "Nisisikie hapa tena mmekaribisha mwekezaji...nitashangaa kweli yaani sisi tujenge kwa fedha zetu kisha mlete mwekezaji baada ya kukamilika kwa ujenzi, sitakueleweni kabisa,” ameonya Rais Magufuli. Rais Magufuli amesema kukamilika kwa ujenzi wa bandari ya Mtwara kutaiwezesha kuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa na nyingi kwa wakati mmoja na hivyo kuharakisha shughuli za upakiaji na ushushaji wa shehena. Amesema ujenzi wa bandari hiyo utagharimu Sh bilioni 137 na kuchukua miezi 21. “Naipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kwa kuweza kutekeleza mpango wake wa uboreshaji wa miundombinu ya bandari nchini kwa kuanza na ujenzi wa gati Bandari ya Mtwara" amesema. “Kukamilika kwa ujenzi wa gati hii kutafungua milango ya kiuchumi na kukuza kipato kwa wakazi wa Mtwara na serikali pia,” amesema Rais Magufuli. Bandari ya Mtwara ina njia ya kuingilia meli yenye kina cha mita 20 na upana wa mita 250. Meli zenye urefu unaofikia mita 175 zinaweza kutia nanga bandarini bila msaada wa kuvutwa. Hakuna masharti ya maji kupwa au kujaa kwa meli zinazoingia au kutoka bandarini. Eneo la ndani la kutia nanga lina kina cha mita 20 na uwezo wa kutia nanga meli nne kwa wakati mmoja. Bandari hiyo inayo maeneo ya kuhifadhia mizigo yaliyofunikwa na ya wazi yaliyojengewa ya mita za mraba 11,000 na 15,000 kwa mfuatano huo. Bandari hiyo pia inashughulikia bidhaa za petroli zilizosafishwa na zisizosafishwa kwa ajili ya kampuni za utafutaji wa mafuta na gesi kupitia kwenye mitambo iliyofungwa upande wa gatini. Ni kutokana na umuhimu wa bandari hiyo TPA, imeanza kuboresha miundombinu katika bandari hiyo ili kunufaika na fursa kubwa zilizopo katika mkoa huo wa Kusini. Fursa zilizopo katika mkoa huo na ambazo zinatarajiwa kuinufaisha bandari hiyo ni pamoja na shughuli za watafutaji wa mafuta/gesi, uzalishaji wa gesi asilia na kuhudumia bidhaa zitokanazo na gesi. Fursa nyingine zilizopo katika mkoa huo ni pamoja na kuhudumia bidhaa za viwanda vinavyojengwa mkoani Mtwara kikiwemo Kiwanda kikubwa cha saruji cha Dangote ambacho kinaendelea na uzalishaji na kuwa tegemeo kubwa kwa uchumi wa Tanzania. Fursa nyingine ni mazao yanayopatikana Mtwara. Ujenzi wa gati jipya la kisasa katika Bandari ya Mtwara utaiwezesha kuhudumia meli za aina zote zenye urefu wa mita 300. Ujenzi wa gati hiyopia utasaidia kuongeza ufanisi wa bandari hiyo na kuiwezesha kuhudumia shehena kubwa zaidi ya mizigo. Hadi sasa imethibitika kuwa Bandari ya Mtwara ni moja kati ya bandari zenye usalama zaidi duniani. Kuhusu utendaji wa bandari hiyo, katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2013/2014 hadi 2015/2016, shehena iliyohudumiwa katika bandari hiyo ni jumla ya tani 356,356 na 273,882. Bandari ya Mtwara iliyojengwa miaka ya 1950 ni moja ya bandari zenye maajabu makubwa kutokana na kuwa na sifa ambazo bandari nyingi nchini hazina.

Thursday, March 2, 2017
Wanafunzi 11 wajeruhiwa baada ya jengo wanalosomea kuezuliwa na mvua.soma zaid

Wanafunzi 11 wajeruhiwa baada ya jengo wanalosomea kuezuliwa na mvua.soma zaid

Wanafunzi kumi na moja wanaosoma shule ya KASISI ëAí iliyopo kata ya ILOLANGULU wilayani UYUI mkoani TABORA wamejeruhiwa baada jengo wanalosomea lenye vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja wa walimu kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha katika baadhi ya maeneo ya kata hiyo. Akizungumza na channel ten diwani wa kata ya ILOLANGULU MOHAMED LINSO amesema wanafunzi wawili kati ya kumi na moja waliojeruhiwa walilazimika kupelekwa hospitali ili kupatiwa matibabu zaidi. Kutokana na changamoto hii wanafunzi sasa wanalazimika kutumia vyumba viwili tu vya madarasa hali ambayo itaathiri maendeleo yao ya elimu. Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya UYUI SAIDI NTAHONDI amewataka wananchi wa kata ya ilolangulu kushikiana ili waweze kurejesha jengo katika hali yake na asiwepo atakayekwamisha zoezi hilo

Watu 14 wanaodhaniwa kuwa Raia ya Burundi wakamatwa nyumbani kwa mbunge jimbo la kiteto.

Watu 14 wanaodhaniwa kuwa Raia ya Burundi wakamatwa nyumbani kwa mbunge jimbo la kiteto.

:Watu 14 wanaodhaniwa kuwa Raia wa
Burundi wakamatwa nyumbani kwa mbunge wa
jimbo la Kiteto mkoani Manyara Mh.Emmanuel
Papian wakiwa wanafanyakazi kwa Mbunge huyo.chanzo itv

Wednesday, March 1, 2017
Mbowe kizimbani kwa kushindwa kutumia mashine za EFD.soma zaid

Mbowe kizimbani kwa kushindwa kutumia mashine za EFD.soma zaid

Mahakama ya wilaya ya Ilala imewaita
mahakamani Freeman Mbowe na mkewe
pamoja na aliyekuwa meneja wa klabu ya
Bilicanas, Steven Miligo kwa maombi ya
mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) baada
ya kushindwa kuwapata kwa kutumia
barua za wito.
-TRA inawashutumu kwa kushindwa
kutumia mashine za EFD kutoa risiti,
kutoa nyaraka za uongo kwa TRA na
kushindwa kutekeleza matakwa ya
usimamizi wa kodi.

Rais Trump aapa kufufua ari na bidii ya wamarekani.soma zaid

Rais Trump aapa kufufua ari na bidii ya wamarekani.soma zaid


Rais Donald Trump amehutubia wabunge wa
Marekani muda mfupi uliopita ambapo ameahidi
kufufua nguvu na bidii ya Wamarekani.
Amesema kwa muda mrefu, Wamarekani wa
kipato cha kati wamekuwa wakipungua na
miundo mbinu imedorora, huku maovu kama vile
uhalifu na ulanguzi wa dawa za kulevya kupitia
mipaka ya Marekani yakiendelea kushamiri.
Bwana Trump amesema ataliomba bunge
kuidhinisha bajeti ya dola trilioni moja kwa lengo
la kuwekeza katika miundo mbinu ya taifa hilo.
Ameahidi kupunguza kodi inayotozwa kampuni za
Marekani, na pia kupunguza kodi kwa
Wamarekani wa kipato cha kati.
Aidha rais Trump amesema kwamba atabadilisha
mfumo wa uhamiaji ulioko sasa ambapo watu
walio na ujuzi wa chini wanaruhusiwa kuingia
Marekani, na kusema kwamba wahamiaji
wanaoonekana kwamba wana ujuzi wa hali ya juu
na wanastahili kuingia Marekani, wataruhusiwa.
Anasema kazi yake si kulinda ulimwengu, bali ni
kulinda Marekani.
Amesema ataunga mkono muungano wa mataifa
yanayojihami ya NATO.
Amesisitiza kwamba Marekani itafanya kazi na
washirika wake kuangamiza kundi la kigaidi la
Islamic state.
Wakati wabunge wa Republican wakishangilia na
kufurahia hotuba hiyo, wabunge wa democrat
waliketi kimya bungeni, na baada ya hotuba
kukamilika, mmoja wao akasema hotuba ya
Trump haikuwa ya kuunganisha.

Leo ndio tareh 1 march.kama unataka kuhama mtandao mwingine bila kubadili namba njia hizi hapa.soma zaid

Leo ndio tareh 1 march.kama unataka kuhama mtandao mwingine bila kubadili namba njia hizi hapa.soma zaid

Mobile Number Portability (MNP) Ni Huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP), ina maana kuwa mtumiaji anabaki na namba yake ya awali iwapo ataamua kuhamia mtandao mwingine wa simu za kiganjani nchini Tanzania. Huduma hii ya MNP itaanza rasmi tarehe 01 Machi 2017. Huduma ya MNP ina faida zipi? Ni Huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP), ina maana kuwa mtumiaji anabaki na namba yake ya awali iwapo ataamua kuhamia mtandao mwingine wa simu za kiganjani nchini Tanzania. Huduma hii ya MNP itaanza rasmi tarehe 01 Machi 2017. • Utaendelea kutumia namba yako ya awali unapohama kutoka mtoa huduma mmoja kwenda mwingine na hivyo kufurahia uhuru na huduma za mtoa huduma mpya. • Utapokea simu na meseji bila kujali ni mtandao upi umehamia na bila kuwa na haja ya kuwataarifu marafiki, familia na wafanyakazi wenzako au washirika katika shughuli zako kwamba umebadilisha mtoa huduma wako. • Utaokoa fedha kwa kuwa hutakuwa na haja ya kununua laini mpya kwa kila mtoa huduma au kuwa na simu ya kiganjani zaidi ya moja. • Utaweza kuchagua mtoa huduma ambaye unaona anatoa huduma bora zaidi, anakidhi matarajio yako na ana ubunifu katika kutoa huduma. Ni Nini Unatakiwa Kufanya Ili Kupata Huduma Hii? 1. Nenda vituo vya mauzo au kwa wakala anayetambuliwa wa mtoa huduma unakotaka kuhamia na umueleze mhudumu kwamba ungependa kuhama na namba yako. 2. Mhudumu atakutaka ujaze fomu maalum ya maombi (fomu moja). 3. Sehemu ya Fomu ya maombi ya kuhama ni tamko rasmi kwamba unakubali kuwa utawajibika kwa madeni yoyote ambayo yanatokana na huduma ulizokuwa unapata kutoka kwa mtoa huduma wako wa awali kama yapo. 4. Utatakiwa kutoa vitu vifuatavyo: – a) Kitambulisho chenye picha yako – kinaweza kuwa Kitambulisho cha Taifa, Kadi ya Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au pasipoti au kitambulisho chochote rasmi kinachotambulika. b) Simu ya kiganjani inayofanya kazi yenye namba unayotaka kubaki nayo. 5. Iwapo una salio katika akaunti ya pesa mtandao utashauriwa kutoa pesa kabla ya kuhama. 6. Utatakiwa kutuma meseji yenye neno “HAMA” kwenda namba ‘15080’ ambayo ni namba maalum ya kuhama. 7. Utapokea meseji kukujulisha kwamba maombi yako yamepokelewa. 8. Iwapo namba yako haikuzuiliwa au kusimamishwa kwa muda kutokana na sababu mbalimbali ikiwapo madeni maombi yako yatashughulikiwa na utajulishwa kwa meseji kuhusu maendeleo ya mchakato huu. 9. Mtoa huduma wako mpya wa huduma za simu za kiganjaji atakupatia laini mpya. 10. Ili kuzuia kupokea mihamala ya fedha mtandao wakati wa kuhama, huduma za kifedha zitasitishwa kwa muda mpaka namba ikapohamishwa kwa mtoa huduma mpya. 11. Katika hali ya kawaida uhamaji utakamilika haraka, iwapo utachelewa si zaidi ya saa 48. Utatumiwa ujumbe mfupi kuwa uhamaji umekamilika na ubadilishe laini. 12. Ikifikia hapo, weka laini mpya uliyopewa na mtoa huduma wako mpya kwenye simu yako. Iwapo huna uhakika wa nini cha kufanya, unaweza kwenda kwa mtoa huduma wako mpya au wakala wake au kuwapigia simu na wataweza kukusaidia. 13. Mchakato umekamilika. Huduma hii ya MNP itaanza rasmi tarehe 01 Machi 2017.

Katika msako unaoendelea TFDA leo imekamata boksi za Viroba 4600 Dar.soma zaid

Katika msako unaoendelea TFDA leo imekamata boksi za Viroba 4600 Dar.soma zaid


MSAKO WA VIROBA: TFDA leo imekamata zaidi
ya boksi 4600 za pombe aina ya viroba
zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala eneo la
Mabibo wilayani Kinondoni.

Uchungu w Njaa:Upungufu wa chakula Tanzani.Ripot ya Twaweza.soma zaid

Uchungu w Njaa:Upungufu wa chakula Tanzani.Ripot ya Twaweza.soma zaid


Wiki na miezi iliyopita kumekuwepo na
mijadala mizito ya kisiasa na kitaifa juu ya
masuala ya upungufu wa chakula
Tanzania. Taaarifa za upungufu wa
chakula mwanzoni zilikataliwa na viongozi
wa juu wa serikali lakini baadae walikiri
kuwepo kwa upungufu wa chakula nchini.
Mwishoni mwa mwezi Januari 2017,
Waziri wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Dk.
Charles Tizeba aliliambia bunge kwamba
utafiti uliofanywa na Wizara kwa
kushirikiana na wadau kadhaa 1 ,
umegundua kwamba Wilaya 55 (kati 169
za Tanzania Bara na Visiwani) zilikumbwa
na njaa, na tani “35,491 za nafaka
zinahitajika kusambazwa kati ya mwezi wa
pili na wa nne mwaka 2017 ili kukabiliana
na upungufu huo uliowakumba watu
1,186,028” 2 katika Wilaya hizo.
Waziri Tizeba alilalamikia kupanda kwa
bei za vyakula katika maeneo mengi na
alisema hii inasababishwa na
wafanyabiashara wasio waaminifu
wanaotumia mianya ya njaa, pamoja na
uhitaji mkubwa wa mahindi katika nchi
jirani. Matokeo yake ni kusababisha bei
za ndani kupanda. Aliongeza kwamba
“Serikali imeanza kuchukua hatua
kudhibiti hali hiyo ambayo ni pamoja na
kutoa chakula kutoka hifadhi za taifa na
kuuza kwa bei nafuu katika maeneo yaliyo
athirika.”
Sintofahamu hii juu ya hali ya chakula
nchini imetokea katika kipindi ambacho
uchumi wa Tanzania umekua kwa kasi
nzuri ya asilima saba kwa mwaka. Lakini
ukuaji huu haujafanikiwa kuondoa
umasikini kwa kiwango kilichotarajiwa na
wengi. Asilimia 68 ya wananchi bado
wanaishi chini ya kiwango cha umasikini
cha $1.25 kwa siku 3 . Pamoja na hayo
kiwango cha udumavu kimeendelea
kuonekana kwa watoto chini ya miaka 5
4 , ukiachilia mbali mafanikio madogo
yaliyopatikana katika miaka ya karibuni
kwenye utoaji wa lishe nchini. Ofisi ya
Taifa ya Takwimu ya Tanzania (NBS) na
UNICEF wanakadiria kuwa robo tatu ya
watoto wote wa Tanzania asilimia 74)
wanaishi kwenye umasikini mkubwa 5 .
Muhtasari huu unawasilisha takwimu za
maoni ya wananchi na uzoefu wao katika
hali ya upungufu wa chakula na sababu
zake. Ni kaya ngapi na jamii zipi ambazo
zimekumbwa na njaa? Ni vyakula vipi
vilivyo adimu kupatikana? Na ni kwa
namna gani bei za vyakula zimepanda
ikilinganishwa na miezi michache
iliyopita?
Takwimu za muhtasari huu zimetokana na
utafiti wa Twaweza wa Sauti za Wananchi.
Sauti za Wananchi ni utafiti wenye
uwakilishi mkubwa unaotumia simu za
mkononi. Uwakilishi huu ni wa Tanzania
bara. Maelezo zaidi juu ya utafiti huu
yanapatikana katika tovuti ya
www.twaweza.or.tz/sauti . Takwimu za
muhtasari huu zilikusanywa katika awamu
ya pili ya kundi la pili la Sauti za
Wananchi.
1. Wahojiwa 1,800, awamu ya 13 ya
kupigiwa simu kwa kundi hili la
wahojiwa, kati ya tarehe 14 - 26
Septemba 2016.
2. Wahojiwa 1,610, awamu ya 16 ya
kupigiwa simu kwa kundi hili la
wahojiwa, kati ya tarehe 9 - 15
Februari 2017.
Matokeo makuu ni:
Kaya nane kati ya kumi (asilimia 80)
zimeripoti kwamba kipato chao
hakikidhi mahitaji yao ya kila siku.
Kaya nane kati ya kumi (asilimia 79)
huweka akiba ya chakula kwa ajili ya
kijitosheleza ifikapo vipindi vya njaa.
Wahojiwa wengi wa Sauti za Wananchi
(asilimia 78) wanaripoti upungufu wa
chakula katika maeneno wanayoishi
Bei ya mahindi imepanda mara mbili
katika kipindi cha miaka miwili na
kusababisha ongezeko la bei katika
bidhaa.
Kaya saba kati ya kumi (asilimia 69)
zilihofia kukumbwa na njaa katika
kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Hali ya upungufu wa chakula imekua
mbaya zaidi katika kipindi cha mwezi wa
Septemba mwaka 2016 hadi Februari,
2017.
Mambo nane muhimu kuhusu hali ya
chakula Tanzania
Jambo la 1: Kaya nane kati ya kumi
zimeripoti kwamba kipato chao hakikidhi
mahitaji yao ya kila siku.
Mwezi Septemba mwaka 2016 kaya nane
kati ya kumi (asilimia 80) ziliripoti kuwa
na kipato kisichokidhi mahitaji yao ya kila
siku. Takwimu hizi zinatofautiana kidogo
katika kaya za mijini na zile za vijijini au
kati ya kaya masikini na kaya tajiri.
Kielelezo cha 1: Je kipato
kinachopatikana katika kaya kinatosha
kukidhi mahitaji ya kila siku ya nyumbani?
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za
Wananchi - Awamu ya 13 (Septemba
2016)
Kaya tano kati ya sita (asilimia 85)
zinasema kwamba kipato kinapopungua
wanalazimika kubana matumizi. Idadi
ndogo inasema watakopa bidhaa (asilimia
6) na wengine huripoti kwamba watakopa
fedha zaidi (asilimia 2).
Walipoulizwa kukadiria ni kiasi gani cha
fedha kingetosha kwa ajili ya mahitaji ya
kaya ya kila siku, wastani wa makadirio
yote yalikua shilingi 1,777 kwa
mwanakaya au shilingi 10,662 kwa kila
kaya 6 . Kwa mwanakaya anaeishi mjini
makadirio yalikuwa juu kidogo (shilingi
2,247) kuliko kijijini (shilingi 1,579).
Makadirio pia yalikuwa makubwa zaidi
kutoka kwenye kaya zenye uwezo
(asilimia 20 ya waliokuwa na utajiri wa
juu sana - Shilingi 2,304) ukilinganisha na
kaya masikini (asilimia 20 ya waliokuwa
na umasikini wa chini kabisa - Shilingi
1,577).
Jambo la 2: Wananchi tisa kati ya kumi
wanaona ni jukumu lao wenyewe
kuhakikisha wana fedha za kutosha za
kukidhi mahitaji ya kaya zao
Idadi kubwa ya wananchi (asilimia 87)
wanasema iwapo watakosa fedha za
kukidhi mahitaji ya chakula kwa ajili ya
familia zao, hawatarajii watu wengine
kulichukua jukumu hilo. Hata hivyo,
asilimia 17 ya wanawake na asilimia 9 ya
wanaume wangetarajia msaada kutoka
nje.
Kielelezo 2: Iwapo ungekuwa huna pesa
za kukidhi mahitaji ya chakula kwa ajili ya
familia yako pamoja na kaya yako, je
unadhani ni jukumu la mtu kukusaidia au
ni jukumu lako mwenyewe?
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za
Wananchi - Awamu ya 13 (Septemba
2016)
Miongoni mwa wale wananchi wachache
(asilima 13) wanaofikiri kwamba ni
jukumu la mtu mwingine kuwasaidia
katika hali hiyo, nusu yao (asilimia 49)
wamesema ni wajibu wa serikali kutoa
msaada. Idadi ndogo wamesema ni wajibu
wa wanandugu (asilimia 36) au marafiki
na majirani (asilimia 7).
Jambo la 3: Katika kipindi cha mwaka
mmoja uliopita kaya moja kati ya nne
imepokea fao, faida au pesa kutoka
kwenye miradi ya serikali
Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita
kuanzia mwezi wa tisa 2015 mpaka mwezi
wa tisa 2016, asilimia 25 ya kaya
zimepokea fao, faida au pesa kutoka
katika vyanzo vifuatavyo:
Sare za shule, kadi ya matibabu, chakula
na kadhalika kutoka kwenye Mpango wa
Watoto Wanaoishi kwenye Mazingira
Magumu
Nafaka za bure kutoka kwa viongozi wa
kijiji na Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi Ya
Chakula (NFRA)
Chakula cha shule kinachotolewa na
Mpango wa Chakula Shuleni
Kazi za jamii zinazotolewa na Tanzania
Social Action Fund (TASAF)
Pesa zinazotolewa na TASAF kwa ajili ya
kunusuru kaya masikini
Vocha za mbolea/mbegu zinazotolewa
na Mpango wa Taifa wa Ruzuku na
Kilimo
Malipo ya mafao kutoka Mfuko wa
Pensheni wa Taifa (NSSF)
Malipo ya mafao kutoka Mfuko wa
Pensheni wa Watumishi wa Umma
(PSPF)
Kielelezo 3: Mafao au faida
zilizopokelewa ndani ya kipindi cha miezi
12 iliyopita
(Asilimia ya kaya zinazopokea mafao
haya)
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za
Wananchi - Awamu ya 13 (Septemba
2016)
Jambo la 4: Kaya nane kati ya kumi
huweka akiba ya chakula
Kaya nane kati ya kumi (asilimia 79)
zimeripoti kwamba wana hifadhi chakula
kwa ajili ya dharura au kuepukana na
njaa. Wananchi wengi zaidi wa vijijini
huhifadhi (asilimia 87) kuliko wa mijini
(asilimia 61) na kaya masikini huhifadhi
kuliko kaya tajiri. Uhifadhi wa chakula pia
uko juu kwa kaya ambazo hutegemea
zaidi kilimo kama sehemu kubwa ya
kipato chao (asilimia 92) kuliko kaya
ambazo hutegemea vyanzo vingine vya
mapato kama vile biashara au ajira
(asilimia 49).
Kielelezo cha 4: Je, kaya yako huhifadhi
chakula kwa ajili ya matumizi wakati wa
dharura au njaa?
(Asilimia iliyojibu ndiyo)
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za
Wananchi - Awamu ya 16 (Februari 2017)

Back To Top